kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Simba na Yanga ni timu kubwa zenye wafuasi wengi wenye hadhi tofautitofauti, zinahitaji wasemaji mahiri sio wasema chochote wanachojisikia wao hata kama hakina maana wala uhalisia.
Hata kama ni utani lakini unawezaje kusema Yanga woooote hawana akili isipokuwa watu wawili tu kwenye timu ambayo ina wafuasi wenye madaraja mbalimbali ya elimu, viongozi, umri, uchumi na kiroho?
Ally Kamwe alikuwa na tabia ya kuwapa baadhi ya wachezaji wa timu hiyohiyo sifa nyingi sana na wakati mwingine sifa zisizo wastahili ambazo ziliwasababishia kukamiwa uwanjani na kuumizwa au kuwavunja moyo wachezaji wengine ndani ya kikosi.
Sio vyema baba kuwatenga watoto wake hadharani kuwa mwenzenu huyu ni mzuri kuliko nyie, ni mwaminifu kuliko nyie badala yake mwache Mchezaji anaefanya vizuri asifiwe na mashabiki wenyewe au wachezaji wenzake.
Kutoa sifa na matarajio yanayokinzana na tabia ya mpira na uwezo wa Mungu nayo ni kuwakosea mashabiki heshima hasa pale matokeo yatakapokwenda tofauti na majigambo na uropokaji wako. Ally kapunguza kama sio kuacha kabisa.
Ahmed Ally bado anazo hizo, anadharaulika mitaani na kumuuona mropokaji tu. Hivi ni kweli Onana ni Ronaldo mtupu? Hivi ni kweli Che Malone ni ukuta wa Yeriko? hivi ni kweli Miquison amerudi kwenye kiwango chake kilichowafanya Al-Ahly wamsajili?
Hivi ni kweli Simba ni lazima izifunge timu ndogo zote Tanzania kila zikikutana? Ni uropokaji au uhalisia?