Ally Kamwe na Manara nani atatangaza kikosi cha Yanga tar 4?

Ally Kamwe na Manara nani atatangaza kikosi cha Yanga tar 4?

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Kuna mchuano mkali hapa, atakayetangaza nadhani ndo picha halisi kwamba ana nguvu kuliko mwenzake ndani ya Yanga.

Hapo lazima kutakuwa na anguko la mmoja kati ya hao hapo

Labda kuondoa sintofahamu atangaze Maulid Kitenge.

Je, kwa mawazo yako nani atapewa kipaza sauti siku hiyo?
 
Lini ally kamwe amewahi kitangaza kikosi cha Yanga? Kipindi chote cha kamwe mara moja wametangaza kitenge na zembwela na mara moja haji wakati kafungiwa mpk ikaleta mzozo
 
Ali Kamwe huwa hanaga mashindano na mtu...,sidhani kama itakuwa ishu kwake!
 
Naona kuongezwa mkataba ali kamwe ni kama geresha tu, wana yanga wasichukie lakini mdogo mdogo bwana manara anachukua nafasi.
Tukienda katika uhalisia, ukiingia kwenye page official ya Yanga anayeonekana ku postwa mara kwa mara ni Ally Kamwe. Na anayeonekana kuhusishwa kwenye shughuli mbali mbali zinahusishwa na mashabiki, wanachama na jamii ni Ally Kamwe mfano kwenye zoezi la uchangiaji damu, zoezi la utoaji misaada n.k. Manara kaonekana katika zoezi la kutangaza wasanii watakaohusika na siku ya sherehe pekee. Ukiangalia jinsi mwenendo ulivyo, unaona kabisa Manara analazimisha awe mkubwa na apendwe ndio maana anatumia nguvu kubwa sana ya kwenye kauli zake ila upepo wa mashabiki wa Yanga kwasasa upo na Ally Kamwe. Tofauti na Ally Kamwe, dogo kawa mtulivu sana na busara hataki kutumia nguvu wala mashindano na Manara.
 
Siku zote manara ni miyeyusho, manara ni kirusi.
 
Haji Manara mtu mzima hovyo, Mzee wa kujipeleka location, Mzee wa kujipendekeza pasipo kualikwa. 😆🤣
 
Iyo siku Manara yuko radhi akwapue mic 🎤 maana kunamsi waligombania mic na kitenge
 
kwani kuna ubayagani mwenyekiti kumtuma yeyote kufanya kazi fulani.
 
Back
Top Bottom