JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Baada ya tetesi za Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe kudaiwa kufungiwa (kama hukusoma bofya hapa -Inaelezwa Ali Kamwe kafungiwa miaka 2, Ahmed Ally anusurika na rungu la TFF), Mwanayanga huyo amejitokeza hadharani na kuelezea kuhusu madhara ya tetesi hizo na jinsi zilivyosababisha mama yake mzazi kupata mshtuko na kukimbizwa hospitali.
Amesema hayo wakati akizungumza na Wasafi FM, leo Machi 7, 2025 siku moja kabla ya mchezo wa Yanga dhidi ya Simba pale kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.