Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasiyo ya Muungano

Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasiyo ya Muungano

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazowahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi(CCM), amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. Ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje. Zanzibar haina uwezo wa kumlipia hata balozi mmoja kule nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

 
Mi sikuwahi kuwapenda wabunge wanaotokana na CCM kwa kuwa huwa hawajui kujenga hoja za maana zaidi ya kusubiri kuunga mkono hoja kwa kuegemea Chama chao kana kwamba Serikali inatumia mfumo wa kibunge (parliamentary system).

Hata hivyo nimekuwa nikiliwazwa mara kwa mara kwa uropokaji mzuri wa Mbunge Kessy hasa dhidi 'ego' za wazanzibar ambao wanajidai wanataka uhuru baada ya kugunfua kuwa wana rasilimali ya mafuta. Go bhana Kessy utupe raha hata kidogo mana hatuwezi kuipata kwa wanaccm wenzako.
 
Huyu Mbunge alishawahi kusema unaweza kuizunguka Zanzibar yote kwa kutumia Baiskeli..


Hawa Wabunge kwanini wasitulie kwao????
Hiyo ni kweli unaweza kuzunguka kwa baiskeli isipokuwa utatumia muda mrefu, mimi na rafiki yangu tulizunguka zanzibar yote kwa gari tulitumia saa mbili na robo tukamalizia kwenda Tumbatu na boti
 
ni lini Zanzibar walisema wanataka Muungano na Watanganyika ? nashangaa Nyerere alivyokimbilia Zanzibar kufunga mkataba wa Muungano..

Mmesahau mlivyokua mkiingia Zanzibar kununua bidhaa ? sasahivi hela za bandari ya Zanzibar mkusanye nyinyi, utalii mkusanye nyinyi, foreign exchange kutoka Zanzibar mkusanye nyinyi , misaada ya UN, FIFA iishie kwenu..

makusanyo hayo kutoka Zanzibar mnaingiza kwenye mfuko wa Muungano kuendesha miradi ya bara na Zanzibar kuambulia mazombie ya askari kutoka bara ili kuwadhibiti...mmeizuia Zanzibar hata kujiunga na OIC ili isinufaike.

MBONA HAMUITISHI REFERENDUM ili Wazanzibar waamue kama wana hata shauku ya kuungana na machogo.
 
Back
Top Bottom