Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasiyo ya Muungano

kelele tu, kipindi cha bunge la katiba alianza moto mwiso wa siku akasujudu kwa mtemi chenge
 
*tuachieni kipande chetu muone kama hatuwezi mlipa balozi mmoja*
 
Kwangu mie binafsi muungano ni km koti km kuna upande unaona limewabana ruksa kuvua sio kwa kukashifiana na kejeri km hzi siungi mkono hoja za kibaguzi
 
Hapana, ni mbunge ana mawazo yake.

Sioni tatizo akizungumza anachokiona sawa,kwenye caucus hilo ni suala jingine.

Mbona Bashe amesema maneno machungu kwa CCM haionekani kama amekosea.

Pili, wale wabunge wa znz linapokuja suala la muungano huwa upande wao

Vuai alisimama kudai mafao. Hana tofauti na wa CUF, hamsemi kakiuka 'uCCM'

Mwacheni Kessy azungumze kwa niaba ya wananchi, kasema ukweli mtupu

Hata kama ni uCCM, kuna hoja hapa.

Wizara ya afya si ya muungano, vipi mznz aliyetibiwa nje kwa kupelekwa na SMZ bili atupiwe Mtanganyika? Kessy kakosea wapi kusema hilo?

Wanataka mabalozi nusu kwa nusu, Kessy anauliza, ni ubalozi gani unaohudumiwa na SMZ? Na kwanini wao wajali vyeo na si huduma za balozi? Kakosea wapi Kessy!

Wznz wanadai mabalozi nusu kwa nusu, hilo jema, Kessy ana mantiki na gharama watakubali nusu kwa nusu kwa maana balozi hizo 10 walipie?

Wizara ya Tamisemi si ya muungano, mznz anajadili nini kuhusu wizara hiyo?

Wizara ya Kilimo si muungano, mznz anachangia nini na ili iweje katika wizara hiyo

Nadhani hoja ya Kessy ni kuwa, midhali hawana wizara nyingi za kuchangia, waje kwa wizara za muungano tu zikipangwa kwa utaratibu wa kufuatana.Baada ya hapo warudi

Hili lina maana kubwa sana, kwamba kwavile wanakuja kwa kodi za Watanganyika, basi watusaidie kubana matumizi.

Tena Kessy kasema, BLW lina wajumbe takribani 50, wanaokuja Dodoma ni zaidi ya 80. kwanini iwe hivyo?

Hawana sababu za kukaa miezi 2 wakijadili wizara 5-7. Wanaweza kukaa wiki moja

Kama wanataka kukaa Dodoma muda mwingi na kusikiliza habari zisizowahusu, wahudumiwe na SMZ katika gharama. Kessy kakosea wapi?

Hatuwezi kutafuta wafanyakazi hewa, tukiwa na ''Wabunge hew''

Tubane matumizi au wachukue jukumu la wabunge wao.

SMZ ikiwalipia gharama hata kama wanataka kukaa miezi 6 haina tabu.
 
Huwa mnapata 4%
 
Hii kauli ni ya ubaguzi wa hali ya juu kwa sababu wao hwakubisha hodi bungeni hapo bali walikuja kwa muibu wa sheria.

huwezi kuwa attack kivile bali muhimu ni kuusakama mfumo uliopo.
Halafu nilishangaa bunge kukaa kimya nikajiuliza inhgekuwaje Kessy angekuwa mbunge wa upinzani
Ndugu zangu tunakoelekea si kwema kabisa mbegu hizi zilizooteshwa mh!
 

Mkuu lile ni bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania, jamhuri ya muungano ni muungano wa nchi mbili tanganyika na znz.

Wale wabunge wamekula kiapo cha jamhuri ya muungano wa tanzinia.
Vitu vyote vinavyo tumika mule ni vya jamhuri ya muungano wa tanzania mpaka dua inyo ombwa asubuhi kabla kuanza kwa kikao.

Wabunge wote waliomo mule walio kula kiapo cha utii wa bunge la jamhuri ya muungano wanahaki ya kujadili na kuhoji lolote lile linalo husu jamhuri ya muunano bila kujali atokapo mbunge..

Kama kuna mbunge kama mzee kesy anataka mambo ya tanganyika yasijadiliwe na wabunge wa znz kwanza aitafute hiyo tanganyika kabla hajatafuta bunge la tanganyika.
Unapo sema wabunge watokao znz wajadili wizara 4 za muungano halafu watoke waache wabunge watanganyika wajadili mambo yao ya tanganyika utakuwa ww sio mtanzania na hujui hata katiba ya nchi unayo sema ni yako.

Ktk dunia hii hakuna nchi inaitwa tanganyika lakini kipo kijiji nija ya segera tanga kinaitwa tanganyika na lipo ziwa tanganyika linalo pakana na zambia congo na burundi kwa upande wa rukwa katavi na kigoma tz.
 
Sawa kabisa, sasa tuonyeshe malalamiko ya znz ya mabalozi yapo kwa mujibu wa sheria gani?

Tuonyeshe malalamiko ya mgonjwa kupelekwa nje na SMZ na bili kuletwa Tanganyika yapo kwa mujibu upi?

Alichokifanya Kessy ni kujibu kauli za wznz ambazo kila siku madai ya kuonewa ndiyo hoja

Ukisikiliza, Kessy alishangiliwa na wabunge w ikimaanisha hoja yake iliwagusa wengi

Utamaduni wa mzanzibar akitoa tuhuma au kutukana ni sawa akijibiwa ni kashfa haufai

Ndio maana tumefika hapa pa kuhoji, wenzetu katika huu muungano mnaonewa wapi?

Nasi tunajibu kwanini hamuonewi bali ni wanafuika kuliko sehemu yoyote ya JMT.

Fikiria kuwa mbunge wa znz anadai kudhulumiwa nafasi za mabalozi.

Anataka katika mablozi 21 wapewe 10. Mbunge huyu anasahau watoto 1000 wa znz wananufaika na pesa za bure za HESLB. Nani anaonewa hapa!

Mbunge wa znz anataka nafasi 10 za mabalozi, amesahau wznz maelefu wamejazana katika mambo yasiyo ya muungano. Nania anaonewa hapa!

Mbunge wa znz anataka nafasi za ubalozi, hatuwasikii wakisema, jamani tupeni balozi japo 3 tuzihudumie. Nani anaonewa hapa!

Mumedai kila kitu na kusikilizwa, sasa nasi tunasema hapana, ikifika mahali haumuwezi kulipia hata wagonjwa wenu inatisha.

Pengine imezoeleka kupeleka bili Dar kama ilivyo kwa umeme , taasisi na mambo mengine. Hili lazima tuliangalie , Watanganyika wana ukomo wa uvumilivu pia.
 
Najua yote hayo, lakini tujiulize, kama mabalozi wanateuliwa na Rais wa JMT , hoja ya wznz kutaka mabalozi 10 wakiwa ni wabunge wa JMT inatoka wapi?

Kama wanajadili mambo ya JMT, hoja ya wznz kulalamika mgonjwa wao hajalipiwa na JMT wakati amepelekwa na SMZ inataoka wapi?

Kama ni wajumbe wa bunge la JMT, hoja ya wzn kuwa wanaonewa inatoka wapi?
Wanaonewa na nani? Na Watanganyika watatewa na nani?

Wazanzibar wakisema ni haki, wakijibiwa ni makosa.

Wao wanajadili hoja kwa mtazamo wa uzanzibar, nasi tunasema midhali wanaona uzanzibar kwanza na si utanzani, basi yale yasiyowahusu wakae pembeni

Chimbuko la haya yote ni kauli za wznz zisizozingatia ukweli wala tafiti ndogo tu.

Nasi tumechoka kukashfiwa tunasema, hebu tuanze taratibu.
Kwanza wanapata haki zao kama January alivyoonyesha

Lakini pia tunatakiwa tulinde haki zetu ili isItokee watu wakadhani Uzanzibar ni sifa maalumu na kwamba katika JMT uzanzibar una hadhi fulani na mamlaka fulani ya kusema, kutukana, kukashifu, kutaka, kupewa n.k.
 
Kaka nguvuni kwani ww hujawahi kumsikia mzee ali akidai barabara za nkansi akifoka kuwa nkansi hana lami lakini kilimanjaro kuna lami kila maha?

Unajua wale wabunge ni kama wake wenza mume ni serikali kila mbunge analia wivu mwenzangu anapendelewa.
 

Kauli ya Mh January Makamba -kudai kuwa Wabunge wa Zanzibar watoke nje wakati yanapojadiliwa mambo ya Muunga-siyo uungwana ndiyo haswaaa kinachokera waTz Bara. Mkataba wote umebainisha yaliyomo na yasiyomo katika muungano.

Kuwataka Bara wawe WASTAARABU wafumbie macho waZenj kuingilia Bara ni sawa? AHMwinyi wakati wake aliteua Katibu Mkuu A Vuai Wizara ya Elimu Bara ili aidhinishe pesa za Bara kusomesha WaZenj tena basi nje ya nchi. Makamba ana kamradi gani huko Znz mpaka atake Bara tuzidi kufumbia macho kwa kuwa WAUNGWANA?


Kessy ana hoja nzito sana, nashangaa watu hawazioni
Nimezifafanua bandiko 210
 
KimsingI kessy amevunja sheria na alipaswa kuchukuliwa hatua hilo ni bunge la muungano sio tanganyika
 
KimsingI kessy amevunja sheria na alipaswa kuchukuliwa hatua hilo ni bunge la muungano sio tanganyika

Wakati A H Mwinyi alipokuwa Rais aliwahi kwenda BBC na kutoa kauli iliyoanzia hivi: "Nilipopewa kutawala Bara ....". Ilifika mahali watu wazima akina Njelu Kasaka (G8) wakapindukia uvumilivu wakataka Serikali ya Tanganyika.

Nakumbuka jeuri ya Wabunge wa Zanzibar ilifikia kuwaudhi waBara mpaka kupigana ndani ya Bunge. Kikubwa ni Mzanzibari pia ni Mtanzania lakini Mbara siyo Mzanzibari. Vuai kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu (Bara) siyo kesi, ni Mtanzania kutoka Zanzibar.

Swali, Wazenji ni wahuni wanaokwenda wakiwalalia waBara kwa hoja za kijinga tu. Mke ndani ya nyumba hudai vikombe hata akitambua kuwa hakuvinunua. Tueleweke vipi? Zanzibar hawaoni HAYA wakakubaliana na huyu Mbunge Ally Kessy?

Mimi nilidhani Mchaga lakini inaelekea ana mizizi tofauti. Napenda sana kuheshimu watu lakini siku zote JK nilimtilia mashaka. Alisema eti " Tuwasaidie wenzetu kwa sababu uchumi wao ni mdogo." Kauli hii natamani kuisahau lakini nashindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…