fokonola bokoyoka
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 966
- 638
Huyu jamaa ana akili sana basi watu hawataki kumwelewa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kessy ameongea Ukweli hata wakimhujumu asirejeshwe bungeni Kauli yake itadumu na kutumika kama kielelezo kizuri juu ya mapungufu ya muungano huu wa ajabu uliosalia barani Afrika.Kashachoka, ila 2020 chama kitahakikisha harudi bungeni.
Mh! kwa ajili ya huyo Kessy? haya kila la heri na msitu wenu.CCM ni msitu wa Vipaji. Hoja Mujjarab kwa wakati Muafaka.
Anajua kuwa nyamazisha wale jamaa zetu kule japo muonekano wake ni kama wao.Huyu jamaa ana akili sana basi watu hawataki kumwelewa.
Hapana, ni mbunge ana mawazo yake.Mkuu ktk bunge la jamhuri kuna wabunge wa znz aina mbili wapo wa ccm na cuf.
Kauli ya mzee kesy nikauli kinzani na katiba ya chama chake na ni kauli inayopishana na itikadi na falsafa ya ccm dhidi ya muungano.
Na hata muundo wa muungano unapishana na kauli ya mzee kesi.
Mzee kesy anataka wabunge wa znz wasishiriki mijadala ya wizara zisizo za muungano.
Je ni wabunge gani wa znz wanaoathirika au wanao faidika na kauli za mzee kesy ni wa ccm au cuf?
Je ninani wanaotakiwa kutoka nje ya bunge la jamhuri wakati wa kujadili mambo ambayo siyo ya jamhuri(YA TANGANYIKA ISIYO KUWEPO) ni hao wanata kujadili au ni wabunge wa bunge la jamhuri wanao tokea ktk majibo ya znz?
Ili mzee kesy afanikiwe matakwa ya kauli zake kwanza angehakikisha kama bunnge la tanganyika lipo na wabunge wa tanganyika wapo na wamekula kiapo cha ubunge wa tanganyika na wamechaguwa viongozo wa bunge hilo kuanzia spika nk.
Vinginevyo mzee kesy ana wananga wana ccm wenzake wa visiwani na bara na zaidi hastahiki kuwa ccm maana anakiuka katiba ya ccm ambayo ndio aliyo itumia kuingilia bungeni.
Kessy ana hoja nzito sana, nashangaa watu hawazioniNikimtafakari Kessy kiundani naona ana hoja tena nzito kuhusu serikali tatu ila ukimuuliza atakuruka 100m
Huwa mnapata 4%ni lini Zanzibar walisema wanataka Muungano na Watanganyika ?
nashangaa Nyerere alivyokimbilia Zanzibar kufunga mkataba wa Muungano..
Mmesahau mlivyokua mkiingia Zanzibar kununua bidhaa ?
sasahivi hela za bandari ya Zanzibar mkusanye nyinyi, utalii mkusanye nyinyi, foreign exchange kutoka Zanzibar mkusanye nyinyi , misaada ya UN, FIFA iishie kwenu..
makusanyo hayo kutoka Zanzibar mnaingiza kwenye mfuko wa Muungano kuendesha miradi ya bara na Zanzibar kuambulia mazombie ya askari kutoka bara ili kuwadhibiti...
mmeizuia Zanzibar hata kujiunga na OIC ili isinufaike..
MBONA HAMUITISHI REFERENDUM ili Wazanzibar waamue kama wana hata shauku ya kuungana na machogo.
Hoja si tatizo bali kaitoa wapi na kwa naniKessy ana hoja nzito sana, nashangaa watu hawazioni
Nimezifafanua bandiko 210
Hapana, ni mbunge ana mawazo yake. Sioni tatizo akizungumza kile anachokiona ni sawa, wakienda kwenye caucus hilo ni suala jingine. Mbona Bashe amesema maneno machungu kwa CCM haionekani kama amekosea.
Pili, wale wabunge wa znz linapokuja suala la muungano huwa upande wao
Vuai kama wengine alisimama na kudai mafao. Hana tofauti na wa CUF, mbona hamsemi kakiuka 'uCCM'
Mwacheni Kessy azungumze kwa niaba ya wananchi wake, kasema ukweli mtupu
Hata kama ni uCCM, kuna hoja hapa.
Wizara ya afya si ya muungano, vipi mznz aliyetibiwa nje kwa kupelekwa na SMZ bili atupiwe Mtanganyika? Kessy kakosea wapi kusema hilo?
Wizara ya Tamisemi si ya muungano, mznz anajadili nini kuhusu wizara hiyo?
Wizara ya Kilimo si muungano, mznz anachangia nini na iweje katika wizara hiyo
Nadhani hoja ya Kessy ni kuwa, midhali hawana wizara nyingi za kuchangia, waje kwa wizara za muungano tu zikipangwa kwa utaratibu wa kufuatana.
Baada ya hapo warudi kwao.
Hili lina maana kubwa sana, kwamba kwavile wanakuja kwa kodi za Watanganyika, basi watusaidie kubana matumizi.
Hawana sababu za kukaa Dodoma miezi 2 wakijadili wizara 4. Wanaweza kukaa wiki moja
Kama wanataka kukaa Dodoma muda mwingi na kusikiliza habari za Tanganyika, wahudumiwe na SMZ katika gharama zao. Kessy kakosea wapi?
Hatuwezi kutafuta wafanyakazi hewa, tukiwa na Wabunge hewa.
Tubane matumizi au wachukue jukumu la wabunge wao.
SMZ ikiwalipia gharama hata kama wanataka kukaa miezi 6 haina tabu.
Sawa kabisa, sasa tuonyeshe malalamiko ya znz ya mabalozi yapo kwa mujibu wa sheria gani?Hii kauli ni ya ubaguzi wa hali ya juu kwa sababu wao hwakubisha hodi bungeni hapo bali walikuja kwa muibu wa sheria.
huwezi kuwa attack kivile bali muhimu ni kuusakama mfumo uliopo.
Halafu nilishangaa bunge kukaa kimya nikajiuliza inhgekuwaje Kessy angekuwa mbunge wa upinzani
Ndugu zangu tunakoelekea si kwema kabisa mbegu hizi zilizooteshwa mh!
Najua yote hayo, lakini tujiulize, kama mabalozi wanateuliwa na Rais wa JMT , hoja ya wznz kutaka mabalozi 10 wakiwa ni wabunge wa JMT inatoka wapi?Mkuu lile ni bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania, jamhuri ya muungano ni muungano wa nchi mbili tanganyika na znz.
Wale wabunge wamekula kiapo cha jamhuri ya muungano wa tanzinia.
Vitu vyote vinavyo tumika mule ni vya jamhuri ya muungano wa tanzania mpaka dua inyo ombwa asubuhi kabla kuanza kwa kikao.
Wabunge wote waliomo mule walio kula kiapo cha utii wa bunge la jamhuri ya muungano wanahaki ya kujadili na kuhoji lolote lile linalo husu jamhuri ya muunano bila kujali atokapo mbunge..
Kama kuna mbunge kama mzee kesy anataka mambo ya tanganyika yasijadiliwe na wabunge wa znz kwanza aitafute hiyo tanganyika kabla hajatafuta bunge la tanganyika.
Unapo sema wabunge watokao znz wajadili wizara 4 za muungano halafu watoke waache wabunge watanganyika wajadili mambo yao ya tanganyika utakuwa ww sio mtanzania na hujui hata katiba ya nchi unayo sema ni yako.
Ktk dunia hii hakuna nchi inaitwa tanganyika lakini kipo kijiji nija ya segera tanga kinaitwa tanganyika na lipo ziwa tanganyika linalo pakana na zambia congo na burundi kwa upande wa rukwa katavi na kigoma tz.
Kaka nguvuni kwani ww hujawahi kumsikia mzee ali akidai barabara za nkansi akifoka kuwa nkansi hana lami lakini kilimanjaro kuna lami kila maha?Najua yote hayo, lakini tujiulize, kama mabalozi wanateuliwa na Rais wa JMT , hoja ya wznz kutaka mabalozi 10 wakiwa ni wabunge wa JMT inatoka wapi?
Kama wanajadili mambo ya JMT, hoja ya wznz kulalamika mgonjwa wao hajalipiwa na JMT wakati amepelekwa na SMZ inataoka wapi?
Kama ni wajumbe wa bunge la JMT, hoja ya wzn kuwa wanaonewa inatoka wapi?
Wanaonewa na nani? Na Watanganyika watatewa na nani?
Wazanzibar wakisema ni haki, wakijibiwa ni makosa.
Wao wanajadili hoja kwa mtazamo wa uzanzibar, nasi tunasema midhali wanaona uzanzibar kwanza na si utanzani, basi yale yasiyowahusu wakae pembeni
Chimbuko la haya yote ni kauli za wznz zisizozingatia ukweli wala tafiti ndogo tu.
Nasi tumechoka kukashfiwa tunasema, hebu tuanze taratibu.
Kwanza wanapata haki zao kama January alivyoonyesha
Lakini pia tunatakiwa tulinde haki zetu ili isItokee watu wakadhani Uzanzibar ni sifa maalumu na kwamba katika JMT uzanzibar una hadhi fulani na mamlaka fulani ya kusema, kutukana, kukashifu, kutaka, kupewa n.k.
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazowahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.
Ally Kessy Mbunge wa Nkasi(CCM), amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. Ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje. Zanzibar haina uwezo wa kumlipia hata balozi mmoja kule nje.
Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.
Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.
Sawa kabisa, sasa tuonyeshe malalamiko ya znz ya mabalozi yapo kwa mujibu wa sheria gani?
Tuonyeshe malalamiko ya mgonjwa kupelekwa nje na SMZ na bili kuletwa Tanganyika yapo kwa mujibu upi?
Alichokifanya Kessy ni kujibu kauli za wznz ambazo kila siku madai ya kuonewa ndiyo hoja
Ukisikiliza, Kessy alishangiliwa na wabunge w ikimaanisha hoja yake iliwagusa wengi
Utamaduni wa mzanzibar akitoa tuhuma au kutukana ni sawa akijibiwa ni kashfa haufai
Ndio maana tumefika hapa pa kuhoji, wenzetu katika huu muungano mnaonewa wapi?
Nasi tunajibu kwanini hamuonewi bali ni wanafuika kuliko sehemu yoyote ya JMT.
Fikiria kuwa mbunge wa znz anadai kudhulumiwa nafasi za mabalozi.
Anataka katika mablozi 21 wapewe 10. Mbunge huyu anasahau watoto 1000 wa znz wananufaika na pesa za bure za HESLB. Nani anaonewa hapa!
Mbunge wa znz anataka nafasi 10 za mabalozi, amesahau wznz maelefu wamejazana katika mambo yasiyo ya muungano. Nania anaonewa hapa!
Mbunge wa znz anataka nafasi za ubalozi, hatuwasikii wakisema, jamani tupeni balozi japo 3 tuzihudumie. Nani anaonewa hapa!
Mumedai kila kitu na kusikilizwa, sasa nasi tunasema hapana, ikifika mahali haumuwezi kulipia hata wagonjwa wenu inatisha.
Pengine imezoeleka kupeleka bili Dar kama ilivyo kwa umeme , taasisi na mambo mengine. Hili lazima tuliangalie , Watanganyika wana ukomo wa uvumilivu pia.
Kessy ana hoja nzito sana, nashangaa watu hawazioni
Nimezifafanua bandiko 210
KimsingI kessy amevunja sheria na alipaswa kuchukuliwa hatua hilo ni bunge la muungano sio tanganyika