Macos
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 1,979
- 1,416
Ndugu yangu, wakati wa bunge la katiba, gavana wa benki kuu aliwahi kusema Zanzibar haichangii muungano. Hakuna mzanzibar aliyesimama kupinga hilo.
Pili, kutuambia wapemba karikoo wanachangia, kunatupa uvivu kujadiliana nawe
Hata hivyo tuna wajibu wa kutoa elimu ya umma. Makampuni ya simu yanachangia si kwasababu ya znz. Zantel si walikuwa znz nini kiliwahamisha? Lazima utambue ukubwa wa soko. Hayo mengine hayana sababu za kujibu maana ni ya kiwango chako, si chetu
Labda nikuambie usiyo yajua kidogo. Wizara zote za muungano znz haichangii hata senti.
Zanzibar haina bajeti za wizara za ulinzi na usalama ambazo ni kubwa ka taifa lolote
Wizara ya mambo ya ndani ambayo ni kubwa kwa taifa lolote
Wizara za muungano na taasisi za muungano
Zanzibar inapewa bajeti sapoti kutoka hazina Tanganyika. Hazina hiyo haina mchango wa znz
Znz inapewa 4.5 ya pato la Tanganyika, kwamba bila kufanya chochote pato la Tanganyika likiongezeka znz inapata mgao mnene.
Ukisikia mabilioni ya kodi yanakusanywa Tanganyika znz ina 4.5% yake hapo
Hao wabunge wanaokuja Dodoma, wanabeba mifuko tu.
Hawahudumiwi na SMZ. Gharama na huduma zao ni za Tanganyika.
Pamoja na mgao huo, tunasikia watapewa tena 4.5 6 ya benki kuu.
Hiyo nayo inategemea uchumi wa Tanganyika
Wanapewa asilimia za mikopo na misaada. Mikopo hiyo ni mzigo wa Tanganyika
Kwamba wanapewa mgao, hawajui deni wala ukubwa wake
Utashangaa Kodi za Tanganyika kupitia mfuko wa elimu HESLB zinafadhili wanafunzi wengi wa znz kuliko ZHESL. Wakati wanafunzi wa znz wakilazimika kurudisha mikopo ZHESL wanafunzi wa ZNZ waniopewa HESLB hawarudishi.
Kumbuka znz imeshapewa mgao wake, vipi ipewe tena HESLB za Bureee! bila kurudisha?
Na ni kwa hesabu au sababu gani inapaswa kupewa pesa hizo.
Kuhusu utumishi, ajira za muungano zinatengenezwa Tanganyika si znz.
Lakini pia kupitia Tanganyika wapo wznz ndani ya maeneo yasiyo ya muungano.
Kupewa mgao wa PAYE ni zawadi, znz haina ajira wanasaidiwa
Muhumi,wazanzibar wasiwe watu wa kudai tuu, tunataka kuwasikia wakichangiwa mawazo ya kuimarisha uchumi ambao wao ni wanufaika kuliko eneo lolote la JMT.
Tunataka wznz wawajibike kwa watu na taasisi zao.
ZHESL ichukue dhamana ya wanafunzi wake. Ada za taasisi zao zilipwe na SMZ.
SMZ ihudumiwe wabunge wake wakija Dodoma, na wasishiriki mambo yasiyowahusu
Lakini pia wakiongelea muungano hatupendi bla bla bla za vocha za simu.
Tunataka tuwasikie wakitueleza wao wanachangia nini katika muungano kwa namba
Wakitaka usawa wa mabalozi(hoja ya kitoto sana) basi waombe kuhudumia balozi hizo.
Si kutaka nafasi za ubalozi wasizojua gharama zake
Wznz wanataka na kudai kwasababu hawajui gharama za muungano, tunataka wawajibike kwa michango ya wazi si kusikia hoja za mabalozi
Hongera mbunge Kessy kwa kuwaambia ukweli mchana. Tumechoka jamani
Hayo unaandika yanao onekana kwa sababu Tanganyika imo ndani ya muungano..sasa Tanganyika ndio muungano na Tanzania ndio Muungano.
Tukizungumzia mapato ...inabidi tujue yana toka wapi ...bila ya shaka ni kodi..kodi anakusanya nani? Muungano...anakusanya kutoka vyanzo gani ? Vyanzo vya Kodi vyote ni vya Muungano...Ikiwa Ni Visa , Kodi za Simu Hapa Tigo au Voda huwa zinalipa VAT ina inalipwa kwa MuUNGANO. Ya zantel ilizaliwa Znz lakini sio kwamba mapato yalikua yanakwenda Znz ...ni share tu ilikuwapo ya SMZ. ..lakini walikuja bongo bila ya shaka soko kubwa la watu ..lakini wanaofaidi sio Znz , kodi za propmotion zinaenda Bongo...na Vat zote Muungano
Kuna Grants Tanzania Inapewa kutoka njee kwa njia mbali mbali ikiwamo budget support znz ndio inatengewa hio 4% ...lakini bajeti ya kote zaidi ya 35% ni tegemezi...hivyo wanapata suppoirt ..jee hio wanayopata znz inaziba pengo hilo 35% bila ya shaka hapana sio lolote...wao hawaruhusiwi kuomba msaada...
issue nyingine ambayo znz ni ujinga kukubali ...ni issue ya sarafu...
Tanganyika wakati wa kuporomoka uchumi wakafanya mazungumzo na IMF Ili kupata Misaasa na mikopo.....Sharti walopewa ni kushusha Thamani ya Shillingi.... na sarafu ikashushwa kwa asilimia zaidi ya 57% na Tanganyika wakapewa fedha za kusaidia bajeti na fedha za kigeni ambazo walikua hawana pamoja na mikopo ...hii ilikua IKIJUILKANA KAMA SAP..Fedaha hii ikashuka upande wa pili hawakuwamo katika program ya IMF hawakufaidika na mapatano yale isipokua kupata machungu tu ya kushuka kwa fedha ...
Hapa tatizo sio wao ..walikua walipwe fidia ..hawakupata hayo..uchumi wao kuanzaia hapo ukaanguka vibaya mno ...na mpaka leo thtamani ya shiling inaanguka wala hakuna fidia huku wanao sababisha kuanguka thamani ni Tanganyika....huu ujinga unakubalika na wachumia tumbo tu...halafu anakuja mtu anasema kuchangii.....kwani Tanganyika inachangia nini katika mambo ya kwake ndani ya koti la muungano ? hamna.
Unajua ungetenda haki na ally kessy angeshauri chama chake kiachane na znz ...hakuna faida tunawalisha tu.tuvunje muungano...Miaka 5 tu inatosha kuifanya znz ...nchi bora zaidi africa...Muungano una faida ..lakini znz wameingia na wrong partner...bora tungekua Kenya..tungekua mbali