Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885



"Kuna watu ni wanafiki Katiba siyo Msaafu, muda wowote inabadilishwa na siyo Rais wa kwanza kuongezewa muda, atake asitake alazimishwe haiwezekani kumuachia nafasi, naulizwa kila siku baada ya Magufuli nani anafuata mimi nasema anaongezewa muda"- Ally Kessy (CCM).

Spika Ndugai ajibu hivi

“Mheshimiwa Keissy ngoja twende uchaguzi mkuu, turudi, na mimi naamini sote tunarudi. Hilo ulishikie uwe nalo moyoni, tutarudi hapa [bungeni] salama, azimio hilo utakuja kulileta wewe Mzee Kessy na litapita kwa kishindo, atake asitake [Rais Magufuli] tutaongeza muda,” Job Ndugai

Kessy.jpg
PIA SOMA
- Hashim Rungwe: Kama tatizo ni muda, Rais Samia aongezewe muda ili tupate Katiba Mpya ndio tufanye Uchaguzi

- Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

- Mzee Mwinyi: Rais Magufuli aongezewe muda wa miaka 5 zaidi kama shukrani

- Zile kelele za Rais Magufuli aongezewe muda mbona hazipingwi kwa Rais Samia?

- Uchaguzi 2020 - Dkt. Magufuli aongezewe muda wa kutawala

- Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala
 
"Kuna watu ni wanafiki Katiba siyo Msaafu, muda wowote inabadilishwa na siyo Rais wa kwanza kuongezewa muda, atake asitake alazimishwe haiwezekani kumuachia nafasi, naulizwa kila siku baada ya Magufuli nani anafuata mimi nasema anaongezewa muda"- Ally Kessy (CCM). #Bungeni https://t.co/Efxma9Dzyf
Aombe Mungu awepo maana hana udugu nae, hata Nkuruzinza alitamani kuwepo lakini Mungu ana kazi nae zaidi. Na watu wema namna hii ndo wala hawacheleweshwaji na muumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Return Of Undertaker,

Huyu ana hali ngumu mno Nkasi Kaskazini, na anajua 2015 alikuwa mtu wa Membe maana ni rafiki mkubwa wa JK. Huku kujipendekeza ni kutafuta huruma ya Mwenyekiti. Mwaka 2014 wakati ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Mpanda unasuasua, alimtolea povu Magufuli bungeni na kumwita mbaguzi anayechelewesha ujenzi wa barabara hiyo sababu ya ugomvi binafsi na Pinda uluosababishwa na Pinda kutamka kusitisha amri ya Magufuli (Waziri) kuhusu sakata la malori akiwa jimboni Chato.
 
Demokrasia yetu ina matobo kweli Mh Kessy anaongea kwa kujiamini "sisi wabunge ndio tuna mamlaka ya kubadili katiba kuwezesha Rais kuongezewa muda" wananchi si lolote si chochote but wao.
Mpumbavu na mshenzi sana, ni shetani kinyamkera. Angeenda bungeni bila sisi, wamevibiwa sasa wanatuona sisi si lolote si chochote!
 
Back
Top Bottom