Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Marekani pamoja na Ukongwe ule ila wamekuwa wakiheshimu sana Constitution ambayo ilikuwa formed na Wale Founding fathers Sita mpaka leo D.Trump ni Rais wa 45 ila miongoni mwao hao ni Franklin Roosevelt Pekee ndio aliyehudumu kwa term nne nae alifia madarakani hio term ya nne ni Rais wa 32 na ndio aliwaokoa wamerakani baada ya Great depression na ni moja ya marais bora kupata kutokea marekani, Rais wa kwanza mwenye George Washington alihudumu kwa Term mbili aliemfata alikuwa john Adam ali serve for one term na second term hakuwa elected, Rais anaweza kuwa bora sana tukasema akae muda mrefu na kuchange katiba je ikitokea Hatunae na Akashika mtu mbaya je hio katiba tutegemee imlinde huyo mbaya pia? Kiongozi bora ni mtu mwenye kuandaa succession plan hata ya zaidi ya choices nne na awape freedom wananchi wa vote hakuna kiongozi aliyengangania Urais akawa na mwisho mzuri never
 
Mimi naona tofauti kubwa huyu wa sasa hawezi kusaidiwa na busara za Nyerere kwasababu Nyerere alishauriwa asing'atuke na wa sasa nyuma ya pazia anawatuma wapambe washinikize huku yeye akijifanya kugoma
 
Mh. Rais keshaona kuna baadhi ya watu wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Akimaliza muhula wake wa pili atakayefuatia pia atakuwa na timu yake [emoji4]
 
Watanzania tuwe macho, naona tumefikia hatua tunachezea mboni ya jicho kwa kusogeza mshale wenye ncha Kali.
 
Tuliwaambia mbunge awe na walau Degree moja from recognised university mkabisha!!
 
Acheni ujinga nyinyi.
Inainekana hatumheshimu hata muasisi wa Taifa hili aliyeweka ukomo
 
Juzi na Jana bungeni mbunge wa Namanyere nkasi Ally Kessy na spika Job Ndugai walisema watu watake wasitake , Magufuri atake asitake lazima aongezewe muda wa kutawala zaidi ya mihura miwili,swali hawa ni wawakikishi wa majimbo wanayotoka ,wanananchi wa majimbo yao ndio Wamewatuma kuwa hawana shida nyingine kwenye majimbo yao zaidi shida yao ni rais Magufuri aongezewe muda? Kuna majimbo mengine hata maji hakuna. Ninavyofahamu mabadiliko yoyote wananchi ndio wanatakiwa wayadai sio mbunge wala spika. Naona wametumwa kupima kina Cha maji ,Kifupi majibu Ni kuwa kina ni kirefu.
 
CC. DR. BASHIRU: KWA TAARIFA NA REJEA ZA KAULI ZAKE KWAMBA CCM ITAHESHIMU KATIBA
 
Huyu mshenzi anatakiwa asirudi bungeni tena, mwinyi mbona alifanya mengi tu lakini hakutaka kuongeza muda. Magufuli hata ajenge magorofa mbinguni akikamilisha muda wake akitoe. Atabaki kukumbukwa kwa aliyo yafanya lakini Tanzania hatutaki ufalme wala uchifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…