Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Marekani pamoja na Ukongwe ule ila wamekuwa wakiheshimu sana Constitution ambayo ilikuwa formed na Wale Founding fathers Sita mpaka leo D.Trump ni Rais wa 45 ila miongoni mwao hao ni Franklin Roosevelt Pekee ndio aliyehudumu kwa term nne nae alifia madarakani hio term ya nne ni Rais wa 32 na ndio aliwaokoa wamerakani baada ya Great depression na ni moja ya marais bora kupata kutokea marekani, Rais wa kwanza mwenye George Washington alihudumu kwa Term mbili aliemfata alikuwa john Adam ali serve for one term na second term hakuwa elected, Rais anaweza kuwa bora sana tukasema akae muda mrefu na kuchange katiba je ikitokea Hatunae na Akashika mtu mbaya je hio katiba tutegemee imlinde huyo mbaya pia? Kiongozi bora ni mtu mwenye kuandaa succession plan hata ya zaidi ya choices nne na awape freedom wananchi wa vote hakuna kiongozi aliyengangania Urais akawa na mwisho mzuri never
 
Mimi naona tofauti kubwa huyu wa sasa hawezi kusaidiwa na busara za Nyerere kwasababu Nyerere alishauriwa asing'atuke na wa sasa nyuma ya pazia anawatuma wapambe washinikize huku yeye akijifanya kugoma
 
Mh. Rais keshaona kuna baadhi ya watu wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Akimaliza muhula wake wa pili atakayefuatia pia atakuwa na timu yake [emoji4]
 
Hii ni aram kubwa imekwisha amriwa. Sasa kilichobakia ni utekelezaji na utekelezaji wake upo so planned kwamba waanze kuingiza KWENYE akili za watu. Jana TBC ikimhoji speaker chini ya mkurugenzi walisema jambo ambalo nahisi ni strategy kubwa. Kinachonishangaza viongozi wapo kimya kabisa
Marais wastaafu
Mawaziri wakuu wastaafu
Na wenye hekima mbalimbali.

Tuweni makini.
Watanzania tuwe macho, naona tumefikia hatua tunachezea mboni ya jicho kwa kusogeza mshale wenye ncha Kali.
 
Tuliwaambia mbunge awe na walau Degree moja from recognised university mkabisha!!
 
Anatoa elimu bure
Amenunua ndege
Amejenga barabara
Umeme kila kijiji
Zahanati kila kijiji
Ujenzi wa reli
Ujenzi wa fly over
Ujenzi wa bwawa la umeme kule rufiji
Mikopo kwa wanachuo
Amewapa wamachinga na mama lushe unafuu wa kufanya biashara

Mambo mengi sana
Acheni ujinga nyinyi.
Inainekana hatumheshimu hata muasisi wa Taifa hili aliyeweka ukomo
 
Juzi na Jana bungeni mbunge wa Namanyere nkasi Ally Kessy na spika Job Ndugai walisema watu watake wasitake , Magufuri atake asitake lazima aongezewe muda wa kutawala zaidi ya mihura miwili,swali hawa ni wawakikishi wa majimbo wanayotoka ,wanananchi wa majimbo yao ndio Wamewatuma kuwa hawana shida nyingine kwenye majimbo yao zaidi shida yao ni rais Magufuri aongezewe muda? Kuna majimbo mengine hata maji hakuna. Ninavyofahamu mabadiliko yoyote wananchi ndio wanatakiwa wayadai sio mbunge wala spika. Naona wametumwa kupima kina Cha maji ,Kifupi majibu Ni kuwa kina ni kirefu.
 



"Kuna watu ni wanafiki Katiba siyo Msaafu, muda wowote inabadilishwa na siyo Rais wa kwanza kuongezewa muda, atake asitake alazimishwe haiwezekani kumuachia nafasi, naulizwa kila siku baada ya Magufuli nani anafuata mimi nasema anaongezewa muda"- Ally Kessy (CCM).

Spika Ndugai ajibu hivi

“Mheshimiwa Keissy ngoja twende uchaguzi mkuu, turudi, na mimi naamini sote tunarudi. Hilo ulishikie uwe nalo moyoni, tutarudi hapa [bungeni] salama, azimio hilo utakuja kulileta wewe Mzee Kessy na litapita kwa kishindo, atake asitake [Rais Magufuli] tutaongeza muda,” Job Ndugai


CC. DR. BASHIRU: KWA TAARIFA NA REJEA ZA KAULI ZAKE KWAMBA CCM ITAHESHIMU KATIBA
 
IMG_20200611_174250.jpg
 
Huyu mshenzi anatakiwa asirudi bungeni tena, mwinyi mbona alifanya mengi tu lakini hakutaka kuongeza muda. Magufuli hata ajenge magorofa mbinguni akikamilisha muda wake akitoe. Atabaki kukumbukwa kwa aliyo yafanya lakini Tanzania hatutaki ufalme wala uchifu.
 
Back
Top Bottom