Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Hawa wabunge nadhani wanatafta kuteuliwa tena kugombea ubunge ndio maana wana fanya uivi
 
Mkuu Mimi sio masikini,nitoe kwenye kundi hill,niweke kwenye kundi la middle income people, tangu nazaliwa na kukua nimekulia ccm,na ninaona inatuletea maendeleo sasa shida ya nini?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app

Mkuu katika siku nimekutana na mwanaccm amejibu vizuri ni wewe , me sina chama yeyote atakaeshinda na akafanya mambo yanayotakiwa na majority i am okay, na kwa hili ulilosema kuhusu kuzaliwa na kukulia ccm ni sawa mkuu..I forgive you mkuu. Your doing what is right for you
 
IMG-20200610-WA0007.jpg
 
Ivi kweri ccm wote akuna mwenye uwozo wa kumzidi magufuri kwenye utendaji kwaiyo hoja asitoke kisa miradi itakufa hii fact ni kwa africa tu
 
Hatari! Kwani kwa muda huu uliobaki kabla ya uchaguzi kuna fununu ya teuzi zo zote?
 
Kama ni hivyo kuna haja gani ya kufanya uchaguzi? Serikali inapoteza mamilioni ya fedha kuandaa uchaguzi harafu ubabe unatumika kukibakiza Chama pendwa madarakani?
Lengo ni kuwahadaa mabeberu ili wasikose misaada.Uzuri washaiona janja yao
 
Kuna uwezekano kabisa wabunge wa CCM wamejiandaa kupeleka muswada bungeni wa kumwongezea jiwe muda wa kukaa madarakani hatowezi kukubali huu upuuzi
 
Habari za wakati huu;
Nasikia Tetetsi kuwa CCM wanataka kumuongeze muda JPM awe rais wa maisha.Rais wa Maisha maana yake ni kwamba afie madarakani.Jambo ambalo htujui ni kwamba kifo kinaweza kuja wakati wowote.Unapoomba afie madarakani anaweza kufa kabla ya kuingia hata awamu ya pili.

Lengo la uzi ni kuwaambia CCM kwamba kama OMBI lenu ni rais wenu kufia madarakani basi jiandaeni kisaikolojia maana kwa hakika kila mukiombacho ndio mtakachopata.
 
Yes tunaweza kusema asiongezewe muda. Na hata yeye hana mpango huo. Ila lazima tukubali. Magufuli ndiye rais bora africa kwa sasa. Na ndiye rais maarufu africa kwa sana. Na ndiye rais mwenye akili nyingi sana africa. Hilo halina ubishi. Binafsi namwamini sana. Maana kila anachokisema ni kama huwa anasema na akili yangu, kila uamuzi anaouchukua huwa kama ameingia kichwani kwangu akajua nlitamani afanye vile
Kwa hiyo anafaa sababu anafanya km unavyotaka wewe?
 
Mkuu kwa kweli huyu Raisi ni mwamba tena inapaswa tumlinde kweli kila mwenye uwezo wa kumlinda huyu Rasi kwa namna yeyote ile hamlinde.

Nimepita juzi pale Busisi Mwanza nimekuta material yamemwagwa pale ya kutosha, wa China wanapiga kazi usiku na mchana kujenga daraja la Busisi ambalo ndio litakuwa kubwa kuliko yote Africa mashariki na litagharimu takriban bilion 200. Hili daraja litakuwa mkombozi kwa wakazi wa kanda ya ziwa na nchi za maziwa makuu. Wakati huo huo SGR ya kutoka Dodoma-Tabora-Isaka-Mwanza hadi Rwanda nayo ipo mbioni kuanza, Mungu atupe nini zaidi Watanzania.
Hayo yote Ni matokeo ya Kodi zetu
Wewe ulitaka asijenge ili azile?
Tumia akili.
 
"Kuna watu ni wanafiki Katiba siyo Msaafu, muda wowote inabadilishwa na siyo Rais wa kwanza kuongezewa muda, atake asitake alazimishwe haiwezekani kumuachia nafasi, naulizwa kila siku baada ya Magufuli nani anafuata mimi nasema anaongezewa muda"- Ally Kessy (CCM).

Spika Ndugai ajibu hivi

“Mheshimiwa Keissy ngoja tuende uchaguzi mkuu, turudi, na mimi naamini sote tunarudi. Hilo ulishikie uwe nalo moyoni, tutarudi hapa [bungeni] salama, azimio hilo utakuja kulileta wewe Mzee Keissy na litapita kwa kishindo, atake asitake [Rais Magufuli] tutaongeza muda,” Job Ndugai

R.I.P Pierre Nkurunziza. Alijipangia mengi makubwa yajayo lakini Mungu akapanga yake.
 
Rais Magufuli anafaa aongezewe muda anafanya mambo makubwa
Hicho tu? kwamba hakuna Mtanzania mwingine kati ya watu wazima Milioni 30 ambaye anaweza kufanya makubwa zaidi? Ni udhaifu kufikiria kitu kama hicho
 
Back
Top Bottom