Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Laki si pesa,Mohamed Said unaweza kutueleza chimbuko la ukoo wa Sykes hapa Tanzania? Kuna mtu kaniambia Sykes chimbuko lao ni Africa Kusini, Walihama kutoka Africa Kusini the late 1800, na kuingia Tanganyika kipindi cha utawala wa Sultani, ili wakubalike na sultani na wazawa wa Mzizima ilibidi wabadili dini na kuwa waislam. je ni kweli?
Sykes Mbuwane alikuwa askari katika jeshi la Wazulu kutoka kijiji cha Kwa Likunyi, Imhambane, Mozambique.
Jeshi hili liliingizwa Tanganyika na Kamanda wa Kijerumani Herman von Wissman kuja kusaidia vita vya Wajerumani dhidi ya Bushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa.
Wameingia nchini wakiwa Waislam kwani ndani ya jeshi lile alikuwapo ndugu yake Sykes Mbuwane jina lake Ally Katini.
Ally Katini alikuwa kipofu na hakukaa sana Tanganyika alirudi Mozambique na aliishi hadi mwaka wa 1952 ndipo alipofariki.
Ally Sykes alipozaliwa mwaka wa 1926 baba yake Kleist Sykes Mbuwane alimpa jina la ''Ally,'' ambae ndiye huyu Ally Katini.