Chakochangu
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 2,668
- 2,164
Chakochangu,
Mbona nishajibu?
Labda unifahamishe ni kipi sijajibu kwa kuniorodheshea upya hayo maswali.
Samahani Mzee, nilipitiwa kidogo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chakochangu,
Mbona nishajibu?
Labda unifahamishe ni kipi sijajibu kwa kuniorodheshea upya hayo maswali.
Chako...Samahani Mzee, nilipitiwa kidogo.
Habari tena Mzee wangu!!!Peramiho...
Waliompokea Mwalimu Nyerere ni wengi katika watu wa Dar es Salaam.
Walioishinae kwa karibu sana kuliko wengine wote ni watu sita - Abdul Sykes na mkewe Bi, Mwamvua, Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab, Dossa Aziz na John Rupia.
Hapa kwanza nakupa tahadhari ili uijue hali za watu hawa.
Abdul Sykes alikuwa Market Master, Soko la Kariakoo na alikuwa na kituo cha mafuta Ilala Boma inaaminika ndiyo Mwafrika pekee katika miaka ile kuwa na biashara kama hiyo Dar es Salaam.
Abdul na mdogo wake Ally walikuwa na nyumba Mitaa ya Stanley, New Street (2), Kipata, Kirk, Ilala, Uhuru na Tandika nje kidogo ya Kariakoo.
Chache katika hizi walijenga katika miaka ya mwanzo ya uhuru na baada ya hapo walijenga au kununua nyumba kadhaa,
Ally Sykes alikuwa na biashara ya ''sales promotion'' kuanzia mwaka wa 1958 na akaingia katika mikondo mingi ya biashara ndani na nje ya nchi.
Dossa Aziz alikuwa na biashara akimiliki magari ya mchanga na kokoto saba na alikuwa yeye na ndugu zake wakimiliki nyumba kadhaa pamoja na nyumba maarufu ya vigae na vioo Mtoni kwa Aziz Ali.
John Rupia alikuwa na biashara kadhaa na alikuwa na gorofa kubwa maarufu mjini Dar es Salaam.
Uwezo huu ndiyo uliowawezesha kufadhili harakati za siasa kuanzia wakati wa TAA hadi wakaunda TANU wazalendo hawa wakiwa ndiyo wafadhili wakuu.
TANU wameianzisha wao na wakaihudumia hadi uhuru ukapatikana mwaka wa 1961.
Wazalendo hawa Nyerere mwenyewe akijua kuwa hakuwa na kazi yoyote ya kuwapa TANU imewakuta wao wakiwa na fedha zao.
Kwa sasa Ibn Hazm wana vitabu vyangu viwili tu watakuonyesha.
Tajiri...Habari tena Mzee wangu!!!
Kwa history zako naona kama Mzee Ally alikuwa na akili sana za Biashara na alifanikiwa sana kipindi chake.
Je kwasasa Biashara zake zinazojulikana alizo anzisha mwenyewe bado zipo?na je kuna walau watoto au wajukuu zake wanaoendeleza utajiri wake?
Rommy,I nasikitika sn kuona historia imezimwa kama mshumaa kumbe waislam walichangia pakubwa mnooooo kwenye uhuru lakini leo waislam hao hao wanateswa na kufungwa majera dah inauma sn wallah lakini ipo siku in sha Allah historia itaandikwa upya yaa ikwahn fyllah
Laki...rommy shabby, waislamu hawakudai uhuru kutoka kwa wazungu, bali wao walikuwa wanasapoti wapigania uhuru akina Nyerere, Kambona , Hawa viongozi wa TANU ndio waliokuwa wanapanga mikakati na mipango ya kudai uhuru, na waislam wakawa wanawasapoti kwa kuwapa chakula na vinywaji ili kuwatia moyo, mfano Abdul Sykes alikuwa anawapa chakula akina Nyerere lakini hakuwa mpanga mikakati mala kiongozi wa TANU
Laki...Mohamed Said, nashukuru kwa historia nzuri, ni kweli, vyama vya AA na TAA viliongozwa na waislamu wengi, swali langu ni hili, kilitokea nini mpaka viongozi wote wa kiislamu kutoka vyama vya AA, na TAA ,wakatupwa nje ya uongozi wa TANU? ukiangalia viongozi wengi wa TANU hawakuwa waislamu kama ilivyokuwa kwa vyama vya AA na TAA, ni nani aliwaweka pembeni kwenye chama cha TANU? na kwanini walikubali kuwekwa nje ya uongozi,
unamuuliza maswali ili akuelimishe au unamuuliza ili akikujibu ulete ubishi?Mohamed Said, nashukuru kwa historia nzuri, ni kweli, vyama vya AA na TAA viliongozwa na waislamu wengi, swali langu ni hili, kilitokea nini mpaka viongozi wote wa kiislamu kutoka vyama vya AA, na TAA ,wakatupwa nje ya uongozi wa TANU? ukiangalia viongozi wengi wa TANU hawakuwa waislamu kama ilivyokuwa kwa vyama vya AA na TAA, ni nani aliwaweka pembeni kwenye chama cha TANU? na kwanini walikubali kuwekwa nje ya uongozi,
ALLY SYKES, PETER COLMORE, ALBERT ROTHSCHILD NA OSCAR KAMBONA
Fred Nyaluchi ni kijana ambae ameonyesha hamu kubwa sana ya kutaka kujifunza historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kwa kauli yake anasema amevutiwa sana na makala ninazoandika na wakati mwingine huzirudia makala hizi akaziwakilisha kwa namna yake ambayo hupendeza kwa msomaji.
Hivi karibuni ameweka katika mtandao historia ya koo 13 anazodai kuwa zinazotawala dunia na moja katika koo hizo ni ukoo wa Rothschild.
Pamoja na haya amegusia Freemasons.
Suala la Freemasons limekuwa katika midomo ya watu wengi katika miaka hii ya karibuni.
Nimemwandikia Nyaluchi na kumueleza kuwa mengi yameandikwa kuhusu hayo yake ya ukoo wa Rothschild, Freemasons nk. nk. aliyotuandikia lakini tatizo kama ninavyoliona mimi na kwa muda wa miaka mingi ni kule kupata ukweli wa hayo ambayo yanayosemwa kuhusu Rothschild na Freemasons.
Nimeishi na watu waliokuwa karibu sana na mimi ambao ikisemwa ni Freemasons lakini tofauti na nyakati hizi siku zilizopita Freemasons watu wakiiogopa na kuhisi ni taasisi moja yenye usiri mkubwa wa kutisha.
Miaka hii karibuni hofu hii haipo tena na mkubwa wa Freemasons hapa Tanzania, marehemu Andy Chande amekuwa akiandikwa kwenye magazeti na sura yake ikionyeshwa katika televisheni akieleza shughuli za taasisi hiyo tofauti na miaka iliyopita.
Hapo chini nataka nimweleze Albert Rothschild kwa faida ya rafiki yangu Nyaluchi na kwa faida ya wasomaji kama nilivyokutananae katika kumbukumbu za Sykes.
Ally Sykes anamweleza Rothschild na hii ilikuwa mara tu baada ya Azimio la Arusha na yeye kwa kushindwa kufuata masharti ya kiongozi kutofanya biashara na kuwa na nyumba za kupangisha, Ally Sykes ilibidi aachishwe kazi serikalini kwa barua aliyoandikiwa na Bhoke Munanka:
‘’Nilikuwa tayari nimeshaingia katika aina nyingine za biashara.
Nilikuwa nawakilisha makampuni kadhaa ya kuuza madawa na vipuli kutoka Ulaya na Marekani.
Biashara hii mpya ikanifanya niwe nasafiri sana kwenda Ulaya na Marekani.
Katika hali kama hii nilipata marafiki wengi wenye nguvu na maadui pia wenye uwezo kama huo.
Katika marafiki zangu wenye nguvu alikuwa Albert Rothschild, mtu maarufu katika dunia ya mabenki.
Ngoja nieleze kisa kifupi ambacho Rothschild na mimi tulikutananacho kinachowahusu maoffsa wa serikali ya Tanzania.
Rothschild alikuwa Myahudi na akiishi Paris.
Nilimfahamu Rothschild Nairobi kupitia Peter Colmore.
Tukawa marafiki na mwenzangu katika biashara.
Nilimtia Rothschild hima aje Tanzania kuangalia uwezekano wa kufungua biashara.
Ilikuwa siku moja wakati yuko Madagascar ndipo akanipigia simu kunifahamisha kuwa anakuja Dar es Salaam na nimpokee.
Mimi sikuwa nafahamu, kumbe Oscar Kambona, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje pia alikuwapo uwanja wa ndege kaja kumpokea Rothschild kama mgeni wa serikali.
Rothschild alikuwa ametua na ndege yake binafsi akiwa na wasaidizi wake.
Alipitishwa haraka sehemu ya VIP lakini Kambona alipigwa na butwaa pale Rothschild alipomwambia kuwa asingependa gari la serikali lililokuja kumchukua bali ataingia katika gari yangu na kufuatana na mimi mjini.
Hii ilikuwa kinyume cha itifaki lakini hakukubali akashikilia kupanda gari yangu.
Rothschild akapanda gari yangu akawa na mimi na mke wangu.
Nikafanya mazungumzo ya biashara na yeye kabla hajakutana na maofisa wa serikali ya Tanzania.
Haya yaliwaudhi sana watu fulani ndani ya serikali.
Mimi sikuona kosa lolote kwani sote tulikuwa tunahangaika katika kujenga nchi yetu na kumfanya mwekezaji ajihisi yuko katika mikono ya watu wema wa kuweza kutegemewa.
Kitu ambacho mimi sikuwa nakifahamu kwa wakati ule ni kuwa nilikuwa nachunguzwa na vyombo vya usalama.
Wivu na choyo vilikuwa vimeingia katika mioyo ya watu fulani wakubwa ndani ya serikali.
Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kuwa chini ya uchunguzi wa serikali.
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika wakoloni nao pia walikuwa waneniweka chini ya uchunguzi.
Itakuwa jambo zuri kwa watafiti kutafiti jinsi wakoloni walivyotumia vyombo hivi vya mabavu dhidi ya wazalendo wapigania uhuru.
Kwa hakika kabisa nilikuwa nafahamu kuwa marehemu Amiri Kweyamba, siku zile yuko Special Branch, alikuwa akipeleka taarifa zangu na za Julius Nyerere serikalini.’’
Kutoka mswada wa maisha ya Ally Sykes: ''Broken Dreams the Life of Ally Kleist Sykes (1926 - 2013).''
Unajua sheikh tatizo LA uandishi wenu kuu ni moja.Hampo objective na history inawezekana historia kweli imepindishwa kwa namna Fulani na mnayo haki ya kudai historia isahihishwe ila napata shida kujua kwanini serikali ikataze ujenzi wa chuo kikuu cha kiislamu bila sababu yoyote ya msingi.Tukisoma makala zenu nyingi sababu inayotelewa ni kana kwamba mwalimu alikuwa anafanya hila dhidi ya uislamu. Ili suala siamini kuna kitu hata nyie mnaficha kwenye history kama sababu ya uzuiaji wa ujenzi wa hicho chuo ulichotaja hapo juu.Laki...
Swali la kwanza ambalo ningependa kukuuliza ni hili.
TANU imetokana na chama gani?
Swali nitakujibia.
TANU imetokana na African Association iliyoundwa mwaka wa 1929.
Unawajua waliounda AA?
Waliounda AA ni hawa wafuatao: Kleist Sykes, Cecil Matola, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Rawson Watts, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima na Raikes Kusi.
Unajua katika kundi hilo Wakristo ni wawili unayajua majina yao?
Rawson Watts na Raikes Kusi.
Unajua sababu yake?
Kanisa lilikuwa linawatahadharisha waumini wake kujiweka mbali na siasa.
Nani kasema maneno haya?
Maneno haya kayasema Kleist katika mswada wa kitabu cha maisha yake alioandika kabla hajafariki mwaka wa 1949.
Unajua wapi unaweza kuyasoma maneno haya?
Maneno haya unaweza kuyasoma katika kitabu hiki: ''Modern Tanzanians,'' kitabu kilichohaririwa na John Iliffe (Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95 -114).
Unawajua wapangaji wa mikakati ya uhuru na wapi unaweza kusoma historia hiyo?
Utapata historia hiyo kutoka kwa ndimi za watoto wa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes hebu msikilize Juma Mwapachu:
1953
''I still recall the visit vividly. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.
Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.
Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University.''
Sasa msikileze Aisha ''Daisy'' Sykes binti yake Abdul Sykes:
1955
Top most in my mind as a child was Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, and through him we got to know for the first time of the existence of a tribe called Zanaki. His home coming was always an event and there would be silent murmurs of “Mwalimu is coming or has arrived”.
For me that signaled my main task as I was always asked to make breakfast of tea and eggs whenever he arrived from St Francis Secondary School in Pugu where he taught. I in fact have a more or less vivid childish memory of him actually taking up temporary residence at our Stanley St. home after he resigned from St. Francis, while his committed friends, that is Baba and Uncle Dossa, were looking for a place for him to stay.
Our house at Stanley being a corner house had a unique design for those times.
The main house with several rooms was on the Stanley side and the Sikukuu side was a kind of studio cum apartment with just the sitting room and an open plan bedroom.
So although it was sizeable, it was difficult for two male adults to share. I believe, my Uncle Abbas who was the regular occupant of this premises would have had to move to Kipata, our other home, or squeeze in on the main house, so that Mwalimu could be comfortable and have privacy.
Of all the regular visitors, Mwalimu Nyerere and Uncle Hamza Mwapachu were highly impressionable to me because of the way they pronounced my nick name Daisy with an Anglicized twist, making it a permanent name for me, even lagging behind my official name Aisha.
As a child I also remember how diligently Baba was preoccupied about the welfare of Mama Maria and her kids, making sure that enough cooked food was delivered to her daily at her little shop in Livingstone/ Mchikichi, a mark of extreme kindness and generosity.
It was also during this formative period in my life that I met the budding women nationalist leaders such as Bi Lucy Lameck from Moshi, Mary Ibrahim and the Moslem women such as Bibi Titi Mohamed, Bi. Tatu biti Mzee, Bi. Hawa biti Maftaha from Dar es Salaam, who all passed as my grannies. Interestingly, these Moslem women were drawn in by Bibi Chiku biti Kisusa, populary known to us as Mama Sakina.
It was Mama Sakina who introduced these famous Moslem women mentioned above. Baba was very central to this strategy because without his encouragement and influence, it is unlikely that these women could have been drawn into the mass mobilization of Moslem women to become prominent at political rallies, singing and shouting out nationalist slogans.
This was knew in the culture, a trend that was at the time totally unexpected and untypical for Moslem women. I overheard numerous discussions when my Dad and his colleagues discussed the names and occasions for which these women were to be brought in to build the political momentum.''
Laki...
Haya ni machache sana katika mengi ambayo nayafahamu.
Kambona kaja baadae sana katika TANU akitokea Dodoma ambako Dodoma waasisi wa TANU walikuwa Omari Suleiman na Haruna Taratibu na hawa ninazo historia zao ambazo walinijadithia kwa vinywa vyao wenyewe wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.
![]()
KIPINDI MAALUM MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA: HISTORIA ILIYOSAHAULIKA YA SHUJAA HARUNA TARATIBU
Haruna Taratibu Mubarak Ghulum Mtangazaji Radio Kheri Akiwa Katika Matayarisho ya Kipindi Maalum cha Miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyik...mohamedsaidsalum.blogspot.com
![]()
Mzee Omar Suleiman (1910 - 2012) Mwasisi wa TANU Dodoma
Mzee Omar Suleiman (1910 - 2012) Mwasisi wa TANU Dodoma 1955 Mohamed Said Mzee Omar Suleiman Katika moja ya misiba mi...mohamedsaidsalum.blogspot.com
Unajua kuwa Southern Province Kanisa lilikuwa na nguvu sana kiasi cha kuchelewesha TANU kukubalika kwa Wakristo? Unawajua waliovunja ngome ya Kanisa huko Southern Province?
Ni Yusuf Chembera na Salum Mpunga:
![]()
SALUM MPUNGA NA YUSUF CHEMBERA MARAFIKI WAASISI WA TANU LINDI
Salum Mpunga Yusuf Chembera Akiwa Mayor wa Lindi Town Council SHUKRANI Ninatoa shukrani kwa waasisi wa walioleta mabad...mohamedsaidsalum.blogspot.com
![]()
MUASISI WA TANU LINDI MDOGO KUPITA WOTE AFARIKI: AHMED SEIF KHAMISI SULEIMAN MANYANYA (1936 - 2015)
Ahmed Seif Naanza kwa kusema kuwa inawezekana kabisa kuwa Ahmed Seif ndiye muasisi wa TANU mdogo kupita wote katika historia ya k...mohamedsaidsalum.blogspot.com
Nahitimisha maswali yangu kwa kukuuliza kweli inawezekana kwa Nyerere atoke nyumbani kwake aje nyumbani kwa Abdul Sykes kupanga mipango ya uhuru wakati Abdul Sykes keshazungumza kuhusu uhuru wa Tanganyika na Chief Kidawa Makwaia hata sura ya Nyerere haijui?