Mzee moh'd naomba kujua katika watu ambao walimpokea mwalimu akitoka shule ya St Francis Kama sjakosea n wangap walibahatika kupata madaraka ya juu nikimaanisha uwazir had ukuu wa wilaya na nyadhfa nyingine kubwa kubwa baada ya kupata uhuru Kama hautojari unaweza kuwataja majina na vyeo vyao au ndio aliwatosa kabisaa
Swali la pili baba yao hao akina Sykes aliyekuja na Jeshi la kiingereza alikuwa na elimu gani wakat huo maana naona Kama Mtu aliyekuwa na upeo Mkubwa Au exposure ya kutembea ilimfanya awe hivyo na je alipotoka huko likunya Mozambique hakuacha Mke na Watoto wengine Au alikuja bado hajaoa?
OMBI Kama hautojari unaweza kuorodhesha vitabu vyako vyote ulivyoandika ili nilienda pale ibn hazm kwa mtoro kariakoo nisihangaike kuuliza nitaje orodha ninunie tu
Shukran sana na Hongera kwa Mada zako tamu zenye kufungua kichwa japo sometimes znaleta taharuki kwa wasiopenda ukweli
Mzee moh'd naomba kujua katika watu ambao walimpokea mwalimu akitoka shule ya St Francis Kama sjakosea n wangap walibahatika kupata madaraka ya juu nikimaanisha uwazir had ukuu wa wilaya na nyadhfa nyingine kubwa kubwa baada ya kupata uhuru Kama hautojari unaweza kuwataja majina na vyeo vyao au ndio aliwatosa kabisaa
Swali la pili baba yao hao akina Sykes aliyekuja na Jeshi la kiingereza alikuwa na elimu gani wakat huo maana naona Kama Mtu aliyekuwa na upeo Mkubwa Au exposure ya kutembea ilimfanya awe hivyo na je alipotoka huko likunya Mozambique hakuacha Mke na Watoto wengine Au alikuja bado hajaoa?
OMBI Kama hautojari unaweza kuorodhesha vitabu vyako vyote ulivyoandika ili nilienda pale ibn hazm kwa mtoro kariakoo nisihangaike kuuliza nitaje orodha ninunie tu
Shukran sana na Hongera kwa Mada zako tamu zenye kufungua kichwa japo sometimes znaleta taharuki kwa wasiopenda ukwelitano
Peramiho...
Waliompokea Mwalimu Nyerere ni wengi katika watu wa Dar es Salaam.
Walioishinae kwa karibu sana kuliko wengine wote ni watu sita - Abdul Sykes na mkewe Bi, Mwamvua, Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab, Dossa Aziz na John Rupia.
Hapa kwanza nakupa tahadhari ili uijue hali za watu hawa.
Abdul Sykes alikuwa Market Master, Soko la Kariakoo na alikuwa na kituo cha mafuta Ilala Boma inaaminika ndiyo Mwafrika pekee katika miaka ile kuwa na biashara kama hiyo Dar es Salaam.
Abdul na mdogo wake Ally walikuwa na nyumba Mitaa ya Stanley, New Street (2), Kipata, Kirk, Ilala, Uhuru na Tandika nje kidogo ya Kariakoo.
Chache katika hizi walijenga katika miaka ya mwanzo ya uhuru na baada ya hapo walijenga au kununua nyumba kadhaa,
Ally Sykes alikuwa na biashara ya ''sales promotion'' kuanzia mwaka wa 1958 na akaingia katika mikondo mingi ya biashara ndani na nje ya nchi.
Dossa Aziz alikuwa na biashara akimiliki magari ya mchanga na kokoto saba na alikuwa yeye na ndugu zake wakimiliki nyumba kadhaa pamoja na nyumba maarufu ya vigae na vioo Mtoni kwa Aziz Ali.
John Rupia alikuwa na biashara kadhaa na alikuwa na gorofa kubwa maarufu mjini Dar es Salaam.
Uwezo huu ndiyo uliowawezesha kufadhili harakati za siasa kuanzia wakati wa TAA hadi wakaunda TANU wazalendo hawa wakiwa ndiyo wafadhili wakuu.
TANU wameianzisha wao na wakaihudumia hadi uhuru ukapatikana mwaka wa 1961.
Wazalendo hawa Nyerere mwenyewe akijua kuwa hakuwa na kazi yoyote ya kuwapa TANU imewakuta wao wakiwa na fedha zao.
Kwa sasa Ibn Hazm wana vitabu vyangu viwili tu watakuonyesha.