Ally Sykes, Peter Colmore, Albert Rothschild na Oscar Kambona

Habari tena Mzee wangu!!!
Kwa history zako naona kama Mzee Ally alikuwa na akili sana za Biashara na alifanikiwa sana kipindi chake.
Je kwasasa Biashara zake zinazojulikana alizo anzisha mwenyewe bado zipo?na je kuna walau watoto au wajukuu zake wanaoendeleza utajiri wake?
 
Tajiri...
Sina taarifa zaidi nini kinaendelea lakini nadhani wanae wali-wind up business.
 
I nasikitika sn kuona historia imezimwa kama mshumaa kumbe waislam walichangia pakubwa mnooooo kwenye uhuru lakini leo waislam hao hao wanateswa na kufungwa majera dah inauma sn wallah lakini ipo siku in sha Allah historia itaandikwa upya yaa ikwahn fyllah
 
Rommy,
JELA...
 
rommy shabby, waislamu hawakudai uhuru kutoka kwa wazungu, bali wao walikuwa wanasapoti wapigania uhuru akina Nyerere, Kambona , Hawa viongozi wa TANU ndio waliokuwa wanapanga mikakati na mipango ya kudai uhuru, na waislam wakawa wanawasapoti kwa kuwapa chakula na vinywaji ili kuwatia moyo, mfano Abdul Sykes alikuwa anawapa chakula akina Nyerere lakini hakuwa mpanga mikakati mala kiongozi wa TANU
 
Laki...
Swali la kwanza ambalo ningependa kukuuliza ni hili.
TANU imetokana na chama gani?

Swali nitakujibia.
TANU imetokana na African Association iliyoundwa mwaka wa 1929.

Unawajua waliounda AA?
Waliounda AA ni hawa wafuatao: Kleist Sykes, Cecil Matola, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Rawson Watts, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima na Raikes Kusi.

Unajua katika kundi hilo Wakristo ni wawili unayajua majina yao?
Rawson Watts na Raikes Kusi.

Unajua sababu yake?
Kanisa lilikuwa linawatahadharisha waumini wake kujiweka mbali na siasa.

Nani kasema maneno haya?
Maneno haya kayasema Kleist katika mswada wa kitabu cha maisha yake alioandika kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Unajua wapi unaweza kuyasoma maneno haya?
Maneno haya unaweza kuyasoma katika kitabu hiki: ''Modern Tanzanians,'' kitabu kilichohaririwa na John Iliffe (Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95 -114).

Unawajua wapangaji wa mikakati ya uhuru na wapi unaweza kusoma historia hiyo?
Utapata historia hiyo kutoka kwa ndimi za watoto wa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes hebu msikilize Juma Mwapachu:

1953
''I still recall the visit vividly. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.

Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.

Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University.''

Sasa msikileze Aisha ''Daisy'' Sykes binti yake Abdul Sykes:

1955
Top most in my mind as a child was Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, and through him we got to know for the first time of the existence of a tribe called Zanaki. His home coming was always an event and there would be silent murmurs of “Mwalimu is coming or has arrived”.

For me that signaled my main task as I was always asked to make breakfast of tea and eggs whenever he arrived from St Francis Secondary School in Pugu where he taught. I in fact have a more or less vivid childish memory of him actually taking up temporary residence at our Stanley St. home after he resigned from St. Francis, while his committed friends, that is Baba and Uncle Dossa, were looking for a place for him to stay.

Our house at Stanley being a corner house had a unique design for those times.

The main house with several rooms was on the Stanley side and the Sikukuu side was a kind of studio cum apartment with just the sitting room and an open plan bedroom.

So although it was sizeable, it was difficult for two male adults to share. I believe, my Uncle Abbas who was the regular occupant of this premises would have had to move to Kipata, our other home, or squeeze in on the main house, so that Mwalimu could be comfortable and have privacy.

Of all the regular visitors, Mwalimu Nyerere and Uncle Hamza Mwapachu were highly impressionable to me because of the way they pronounced my nick name Daisy with an Anglicized twist, making it a permanent name for me, even lagging behind my official name Aisha.

As a child I also remember how diligently Baba was preoccupied about the welfare of Mama Maria and her kids, making sure that enough cooked food was delivered to her daily at her little shop in Livingstone/ Mchikichi, a mark of extreme kindness and generosity.

It was also during this formative period in my life that I met the budding women nationalist leaders such as Bi Lucy Lameck from Moshi, Mary Ibrahim and the Moslem women such as Bibi Titi Mohamed, Bi. Tatu biti Mzee, Bi. Hawa biti Maftaha from Dar es Salaam, who all passed as my grannies. Interestingly, these Moslem women were drawn in by Bibi Chiku biti Kisusa, populary known to us as Mama Sakina.

It was Mama Sakina who introduced these famous Moslem women mentioned above. Baba was very central to this strategy because without his encouragement and influence, it is unlikely that these women could have been drawn into the mass mobilization of Moslem women to become prominent at political rallies, singing and shouting out nationalist slogans.

This was knew in the culture, a trend that was at the time totally unexpected and untypical for Moslem women. I overheard numerous discussions when my Dad and his colleagues discussed the names and occasions for which these women were to be brought in to build the political momentum.''

Laki...
Haya ni machache sana katika mengi ambayo nayafahamu.

Kambona kaja baadae sana katika TANU akitokea Dodoma ambako Dodoma waasisi wa TANU walikuwa Omari Suleiman na Haruna Taratibu na hawa ninazo historia zao ambazo walinijadithia kwa vinywa vyao wenyewe wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.


Unajua kuwa Southern Province Kanisa lilikuwa na nguvu sana kiasi cha kuchelewesha TANU kukubalika kwa Wakristo? Unawajua waliovunja ngome ya Kanisa huko Southern Province?
Ni Yusuf Chembera na Salum Mpunga:


Nahitimisha maswali yangu kwa kukuuliza kweli inawezekana kwa Nyerere atoke nyumbani kwake aje nyumbani kwa Abdul Sykes kupanga mipango ya uhuru wakati Abdul Sykes keshazungumza kuhusu uhuru wa Tanganyika na Chief Kidawa Makwaia hata sura ya Nyerere haijui?
 
Mohamed Said, nashukuru kwa historia nzuri, ni kweli, vyama vya AA na TAA viliongozwa na waislamu wengi, swali langu ni hili, kilitokea nini mpaka viongozi wote wa kiislamu kutoka vyama vya AA, na TAA ,wakatupwa nje ya uongozi wa TANU? ukiangalia viongozi wengi wa TANU hawakuwa waislamu kama ilivyokuwa kwa vyama vya AA na TAA, ni nani aliwaweka pembeni kwenye chama cha TANU? na kwanini walikubali kuwekwa nje ya uongozi,
 
Wallah heshima ya waislam italindwa na waislam wenyewe kwanza najivunia kuona kuna msomi mbobezi kama ww mzee wangu saidi allah akuifadhi, najua waislam tunachangamoto kubwa sn sasa hv tumekosa hizza, ila in sha Allah allah atatupa hizza na kauli ya mtume itatimia tu kua uislamu utatawala dunia japo kanisa na watu wake watachukia haqq lazima isiwe zama zimebadilika sn na muda sio rafiki tena.
 
Laki...
Hili si swali ambako nitaweza kukujibu hapa.

Ikiwa utasoma kitabu cha Abdul Sykes hii ni sehemu ya mwisho ya kitabu utapata majibu yako hapo pamoja na mengi mathalan kwa nini historia ya TANU ikabadilishwa ili kuwafuta wale waliopigania uhuru na badala yake ikaingizwa historia mpya nk. nk.
 
unamuuliza maswali ili akuelimishe au unamuuliza ili akikujibu ulete ubishi?
 

Mkuu

Wewe ni best katika narration,hakuna mwingine aisee!

Na una command best English and Kiswahili fluency more than anyone else!

Sio siku hizi mitoto haijui hata Kiswahili vizuri!
 
Unajua sheikh tatizo LA uandishi wenu kuu ni moja.Hampo objective na history inawezekana historia kweli imepindishwa kwa namna Fulani na mnayo haki ya kudai historia isahihishwe ila napata shida kujua kwanini serikali ikataze ujenzi wa chuo kikuu cha kiislamu bila sababu yoyote ya msingi.Tukisoma makala zenu nyingi sababu inayotelewa ni kana kwamba mwalimu alikuwa anafanya hila dhidi ya uislamu. Ili suala siamini kuna kitu hata nyie mnaficha kwenye history kama sababu ya uzuiaji wa ujenzi wa hicho chuo ulichotaja hapo juu.


Kitu kingine vitabu vyenu baada ya Ku focus kwenye history bila bias ila kila baada ya mistari kadhaa "wanawake wa kiislamu" waislamu hao. Ni kama kuna ajenda ya siri mlikuwa nayo mi sioni ubaya wowote wadai Uhuru wa nchi kuwa waislamu au wahindu au wayahudi(kidini) au waabudu mizimu ila kwanini kwenye kuwazungumzia lazima muhusishe dini zao kabla ya utaifa wao. Makala nyingi naona unaelezea historia ya Tanzania katika kudai Uhuru kama vile "jihad" kuliko political struggle.

Ni hayo tu mzee wangu.Mi nahisi mngeandika hizi historia kwa mlengo wa kihistoria na sio kidini pengine haya madini unayo mwaga hapa jamii forum yangekuwa kwenye curriculum ya historia ya Tanzania katika skuli zetu.

Namna ya uandishi wenu ndounafanya kuondoa credibility ya makala zenu na vitabu vyenu ambavyo pengine zi/vinaukweli mwingi ndani yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…