Almasi Kasongo na wenzako wa TPLB mnatuharibia mpira wetu mnatakiwa mjiuzulu hakuna kanuni inayoruhusu timu kugomea mechi wa kunyimwa kufanya mazoezi

Almasi Kasongo na wenzako wa TPLB mnatuharibia mpira wetu mnatakiwa mjiuzulu hakuna kanuni inayoruhusu timu kugomea mechi wa kunyimwa kufanya mazoezi

Morning Glory1

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2019
Posts
237
Reaction score
381
Tff wanakiri kabisa kwenye barua yao ya kuhairisha mechi kua timu ya simba haikutoa taarifa kwa mamlaka yeyote ili taratibu za kikanuni zifuatwe nanukuu paragraph ya nne(4)

Baada ya kupitia taarifa mbalimbali zikiwemo za maofisa wa mchezo na vyanzo vingine,kamati ilibaini kua klabu ya simba wakati ikielekea kutumia haki yake iliyohainishwa kwenye kanuni ya 17:45 ya ligi kuu haikuwasiliana na ofisa yeyote wa mchezo,timu mwenyeji wala mamlaka ya uwanja kuhusu nia yao ya kufanya mazoezi ili maandalizi ya kikanuni yafanyike

Kwahiyo kama simba hawakutoa taarifa yeyote yanga wanahukumiwa kwa sababu gani?!

Kwa faida ya wasiojua kanuni za ligi kuu ..kanuni ya 17:45 utaratibu wa mchezo inasema ivi nanukuu
Timu ngeni itafanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi katika muda tarajiwa wa mchezo husika.Sababu zozote za kukwamisha timu ngeni kukidhi ipasavyo kupata haki hii zitathibitishwa kwanza na kamisha wa mchezo

Taarifa ya tff inathibitisha kwamba alievunja kanuni ya 17:45 ni timu ya simba kwasababu hawakutoa taariga kwa mamalaka yeyote lakini hata kama yanga ilivunja kanuni 17:45 kwa kuizuia simba kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi je kanuni inatoa uhalali wa simba kugomea mechi?!

Hakuna kanuni yeyote inayoipa uhalali simba kugomea mechi ila hata kama yanga ilivunja kanuni tff ilitakiwa kuipa yanga adhabu ya either onyo kali au karipio au kutozwa faini au kufungiwa kwa mujibu wa kanuni 17:60 nanukuu

TFF/TPLB itachukua hatua kwa ukiukwaji wowote wa taratibu za mchezo kama zilivyohainishwa kwenye kanuni ya 17 kwa kutoa onyo kali au karipio au kutoza faini kuanzia shilingi laki tano (500,000/-) mpaka shilingi milioni moja (1,000,000/-) na/au kufungia michezo isiyozidi mitatu(3) au kipindi kisichozidi miezi mitatu(3).Faini kwa makosa yanayojirudia itatoshwa kati ya shilingi milioni moja (1,000,000/-) na shilingi milioni tano (5,000,000/-) kwa mchezaji,kiongozi au timu itakayovunja kanuni

Kwa hili bodi ya ligi imepuyanga na inatakiwa iombe radhi kwa wadau wa soka na klabu ya yanga inastahili ipate pointi tatu na magoli matatu vinginevyo bodi ya ligi yote kuanzia kwa mtendaji wake mkuu Almasi Kasongo na wenzie wanatakiwa wajiuzulu haraka hatuwezi kuvumilia uhuni kama huu uliofanywa na klabu ya simba wa kukimbia dabi
IMG_20250308_231443.jpg
 
Mpira wa Tanzania umegubikwa na uhuni mwingi sawa OiC na TPB ambayo imevunjwa juzi waziri asipepese macho avunje bodi leaguekuna uhuni mule Almas kila mwaka yeye tu kwani yeye nani ???? Tumechoka sasaaa
 
Simba walishaziona 5.
Unadhani nani angekuwa tayari kubeba fedheha tena?

Ila Simba wamefaulu kwa kuwatisha zigo lililooza kina Kasongo!
 
Back
Top Bottom