Alphonce Simbu: Hatukwenda kuiangalia njia(Olimpiki 2024), tuliiona tu kwenye Mtandao

Alphonce Simbu: Hatukwenda kuiangalia njia(Olimpiki 2024), tuliiona tu kwenye Mtandao

Mwanariadha Alphonce Simbu alipotua Nchini akitokea Ufaransa alihojiwa na hii ni sehemu ya maelezo yake kuhusu sababu za yeye kutofanya vizuri na kushinda Medali kwenye Michezo ya Olimpiki 2024 Jijini Paris:

"Kwanza kabisa tulitakiwa tujijue njia ambazo tutatumia kukimbia hata miezi miwili kabla ili tuweze kuifanyia mazoezi, kuanzia hapo lakini tuliijua siku za karibuni kabla ya kuelekea Paris, hiyo ilikuwa changamoto kwetu.

“Mfano mimi nilikimbia sana katika mteleko, nilipofika kwenye kilima kukawa na ugumu kidogo.

“Tuliona njia hiyo katika mtandao tu, tulivyofika tuliangalia tu ilivyochorwa lakini hatukuwa na nafasi ya kwenda kuifanyia mazoezi.

“Unajua njia sio tu kuiangalia lakini lazima uifanyie mazoezi, usipofanya hivyo kuitumia inakuwa ngumu.”

Alipoulizwa maoni yake kuhusu Olipimiki kwa jumla na Tanzania inafeli wapi mesema “Tuwe na tabia ya kukuza Vijana tusiwe na tabia ya kusubiri watu wajitokeze wenyewe inatengeneza ‘gape’, mfano tukiwa na program ya kutafuta wachezaji hasa vijijini, unajua kuna wachezaji wengi wa riadha wapo vijijini.

"Tukiwa na tabia hiyo ya kutafuta watu na kuwatengeneza kutakuwa hakuna tena ile tabia ya Mtu akistaafu panapoa haitakuwepo.”
Mbona wafaransa hawakushika nafasi za juu? Inamaana nao hawakuijua njia?
 
Alichokiongea Simbu kuna uzi mmoja kuna member nae alikiongelea na nikamwambia kuwa wazo lake ni zuri sana, Tanzania vipaji vipo lakini huko ngazi za juu huwa wanasubiri mpaka wajulikane nje ya nchi nao ndio wanajifanya kuwasapoti ambapo walikuwa na uwezo wa kuwasapoti kabla ya kutoka/kujulikana kwao nje ya nchi.
Kwa sababu hawako serious na kukuza vipaji ila wanavizia wapige hela kupitia wewe ndio kitu ambacho Mwakinyo huwa anakikataa kutumika na hela wale wengine wakati njia zote za kufika alipo alijitengenezea mwenyewe na Mungu akamuinua.
 
Mwanariadha Alphonce Simbu alipotua Nchini akitokea Ufaransa alihojiwa na hii ni sehemu ya maelezo yake kuhusu sababu za yeye kutofanya vizuri na kushinda Medali kwenye Michezo ya Olimpiki 2024 Jijini Paris:

"Kwanza kabisa tulitakiwa tujijue njia ambazo tutatumia kukimbia hata miezi miwili kabla ili tuweze kuifanyia mazoezi, kuanzia hapo lakini tuliijua siku za karibuni kabla ya kuelekea Paris, hiyo ilikuwa changamoto kwetu.

“Mfano mimi nilikimbia sana katika mteleko, nilipofika kwenye kilima kukawa na ugumu kidogo.

“Tuliona njia hiyo katika mtandao tu, tulivyofika tuliangalia tu ilivyochorwa lakini hatukuwa na nafasi ya kwenda kuifanyia mazoezi.

“Unajua njia sio tu kuiangalia lakini lazima uifanyie mazoezi, usipofanya hivyo kuitumia inakuwa ngumu.”

Alipoulizwa maoni yake kuhusu Olipimiki kwa jumla na Tanzania inafeli wapi mesema “Tuwe na tabia ya kukuza Vijana tusiwe na tabia ya kusubiri watu wajitokeze wenyewe inatengeneza ‘gape’, mfano tukiwa na program ya kutafuta wachezaji hasa vijijini, unajua kuna wachezaji wengi wa riadha wapo vijijini.

"Tukiwa na tabia hiyo ya kutafuta watu na kuwatengeneza kutakuwa hakuna tena ile tabia ya Mtu akistaafu panapoa haitakuwepo.”
Huwa tunatoa sababu za kijinga sana, kwahiyo walioshinda walifanya mazoezi kwenye njia hizo! Hivi Tanzania hakuna njia zenye vilima tena zaidi ya hiyo anayoisema! Aseme tu wazi hana uwezo kama aliokuwanao zamani, mbona wakenya tunawaona mitandaoni wakifanya mazoezi binafsi vijijini.
 
Kukimbia mbio ndefu sio kuwa 3 Hadi km 39, ni mikakati ya km 42 , na jinsi ya kutumia hizo nguvu katika nyakati tofauti tofauti
Nakubaliana na wewe.
Kukimbia ni mahesabu ukitumia nguvu nyingi kuanzia mwanzoni mbeleni utachoka kisha wenzako wanakupita polepole tu unabaki kuwaangalia huku unahema.
Lakini hata hivyo kama hadi km 39 alitembea nazo vizuri huyo mtu kipaji kipo km 3 zilizobaki ni sehemu ndogo sana,akienda kushindana tena kwenye mashindano ya kimataifa anaweza kufanya kitu huenda ni ugeni wa mashindano ya kimataifa pia imemchanganya.
 
Duh mimi sio mzoefu ila loosers always have a lot of excuses

Ila huwenda excuse zaks zina make sense
bro mimi nimeona hizo mbio mwanzo mwisho,kwenye miteremko simbu alikuwa grupu la watano wa mwanzo,na kuna wakati ilipobakia km 10 alikuwa wa tatu,aisee ilipoanza miinuko alipitwa kama kasimama,hivyo alichosema simbu ni kweli
 
Hivi hakunaga mashindano ya fitina na majungu?
Tanzania tungechukua medali zote mshindi wa kwanza hadi 10
 
Hii ina maana hamkuandaliwa vizuri, kwa Olympic ijayo turekebishe makosa haya yasijirudie.
 
Hii ina maana hamkuandaliwa vizuri, kwa Olympic ijayo turekebishe makosa haya yasijirudie.
kwa safari hii kila alitimiza viwango vya olimpiki alipewa dola 1500 kwa mwaka mzima na kamati ya olimpiki ya kimataifa ikiwa ni sehemu ya matayarisho.
 
Kinachonisikitisha ni tambo walizizitoa viongozi wa msafara kwamba wanakwenda Paris na wataishangaza Dunia kwa matokeo yao. Badala ya kushangaza Dunia wametushangaza sisi wananchi kwa matokeo hayo waliyoyapata. Ukiwa na maandalizi duni usitegemee matokeo ya kushangaza Dunia. Tegemea aibu na fedheha.
 
Huyo Simbu mwenyewe hata kupata hiyo nafasi ya kwenda kushirik ni kwa sababu ya corrupted system iliyopo kwenye mchakato mzima wa kumpata mshiriki... tangu ameanza kushiriki 2016 hakuna cha maana aliachowahi kufanya, lakini bado anachaguliwa yeye sio kwamba eti hakuna wakimbiaji wengine... analeta sababu ambazo hazina kichwa wala miguu utafikiri hao aliokuwa anshindana nao walikuwa familiar na mazingira ya kimashindano.... yeye aseme tu hakufanya maandalizi ya kutosha sababu alijua nafasi yake kutuwakilisha ipo basi.

Kwa nchi zilizo serious na michezo huyu angekuwa ameshapigwa chini siku nyingi sana.
 
Mk
Stupid excuse.

Hadi kilomita 39 alikua namba 3, ghafla kilomita 3 mbele anakua wa 17, hizo 39 ambazo alikua wa 3 alikua pia ameziona kwenye tv ama online, aliwezaje kuwa wa
Kujua njia wakati kuna gari na pikipike zinawaongoza?😂😂
Umeelewa hoja yake, kujua njia ni milima au mteremko na sio kujua njia kwamba hawajui wanapokwenda . Msibeze jitihada za watu kirahisi tuuu
 
Huyo Simbu mwenyewe hata kupata hiyo nafasi ya kwenda kushirik ni kwa sababu ya corrupted system iliyopo kwenye mchakato mzima wa kumpata mshiriki... tangu ameanza kushiriki 2016 hakuna cha maana aliachowahi kufanya, lakini bado anachaguliwa yeye sio kwamba eti hakuna wakimbiaji wengine... analeta sababu ambazo hazina kichwa wala miguu utafikiri hao aliokuwa anshindana nao walikuwa familiar na mazingira ya kimashindano.... yeye aseme tu hakufanya maandalizi ya kutosha sababu alijua nafasi yake kutuwakilisha ipo basi.

Kwa nchi zilizo serious na michezo huyu angekuwa ameshapigwa chini siku nyingi sana.
Corrupted system ipi mkuu, vigezo vinawekwa ukifikisha time flani umefuzu, sasa vp inakuwa corrupted system
Ni jitihada zake mkuu
 
Kwanza hizo nafasi za Olympic zinapatikanaje?yaani vigezo vikoje?maana tunashitukia tu tunaona mashindano ya Olympic lakini utaratibu wa kufika huko watanzania wengi hawajui
....pia tufahamu hata namna viongozi wao wanavyopatikana...maana huyo Bayi na mwenzie Henry Tandau nimeanza kuwasikia muda kweli..nadhani hawana MAWAZO mapya tena
 
Back
Top Bottom