Alshabaab waaamuru watu wote ambao si wazawa kuondoka katika eneo lote la Kaskazini mashariki mwa Kenya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Hii amri inafuatia baada ya Wizara ya elimu ya Kenya kuwaondoa waalimu wote ambao sio wazawa kutoka hivyo kusababibasha upungunfu mkubwa wa waalimu ktk eneo hilo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara toka kwa Alshabaab dhidi yao.

Baada ya kuona kwamba wamefanikiwa katika kusambaratisha sekta ya Elimu, wameamua kupanua wigo na malengo yao, sasa hivi wanalenga watu wote ambao sio wazawa /wakristo, hii ikifanikiwa ni wazi kwamba uchumi wa eneo hili utasambaratika kabisa na itakua rahisi sana kwao kupata wafuasi na kuzidi kujiimarisha.
 
Hee...wao wenyewe ni wazawa??
 
Yaani unamaanisha Alshabab wanawapangia Wakenya wapi waishi na wapi wasiishi ndani ya nchi huru ya Kenya??
Hii ni dharau kubwa kwa jeshi letu imara la KDF ambalo lina kiapo cha kulinda mipaka yetu kwa gharama ya jasho na damu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi ninashangaa sana, yaani wizara ya elimu inawaondoa waalimu badala ya serikali kuimarisha ulinzi, Kenya bajeti ya ulinzi ni kubwa sana karibu mara mbili ya Tanzania, lakini vyombo vya ulinzi vimeshindwa kabisa kuzuia mashambulizi ya Alshabaab ndani ya Kenya, Alshabaab wanashambulia na kuingia katika ardhi ya Kenya vile wapendavyo, hapo ndio wakenya wanapaswa kujua kwamba taarifa za kwenye makaratasi ni tofauti na hali halisi.
 
isis-caliphatemap.jpg
Hata ISIS pia kwa ubabe wao walijichorea ramani mpya ya dunia. Wakajitengea sehemu yao ambayo watatawala kisharia. Leo hii wengi wao wapo kwao Jehanam. Wachache waliosalia wanakula maharage ya bure na kuishi kama fuko, hata jua wasikumbuke linafananaje. Mtz mpumbavu tu ndiye anayeweza kushabikia magaidi ambao wamemwaga damu ya watz wenzake mara kadhaa. Tena ambao wamewageuza vijana wengi wa kitanzania kule Somalia wakawa mazombie. Mleta mada, unachofanya ni sawa na kumcheka mama wa kitanzania ambaye kwa muda mrefu hajala, hajanywa, kisa mtoto wake alifunga safari ya kuvuka boda hadi Somalia, akawe zombie. Hongera.
 
Wacha kupindisha mada, kinachozungumzwa hapa ni jeuri ya Alshabaab kwa serikali ya Kenya, vipi Kenya imewaoondoa waalimu wote badala ya kuimarisha ulinzi, ina maana serikali ya Kenya imesalimu amri hivyo kutekekeza matakwa ya Alshabaab?
 
Bajeti ya ulinzi kwa Tanzania ni shilingi ngapi mh waziri?
Hata mimi ninashangaa sana, yaani wizara ya elimu inawaondoa waalimu badala ya serikali kuimarisha ulinzi, Kenya bajeti ya ulinzi ni kubwa sana karibu mara mbili ya Tanzania, lakini vyombo vya ulinzi vimeshindwa kabisa kuzuia mashambulizi ya Alshabaab ndani ya Kenya, Alshabaab wanashambulia na kuingia katika ardhi ya Kenya vile wapendavyo, hapo ndio wakenya wanapaswa kujua kwamba taarifa za kwenye makaratasi ni tofauti na hali halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KDF ilitakiwa kuweka kambi ya kudumu huko kaskazini. Fyokofyoko yoyote itaongelewa kwa kuwarambisha risasi na mabomu kadhaa hawa Al Shabaab.

Badala ya kuacha watu wazalishe mali wanawazidishia umaskini tu!
 
Relevance ya Tanzania katika hili imekuja vipi? Umesoma geography kweli wewe

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hata mimi ninashangaa sana, yaani wizara ya elimu inawaondoa waalimu badala ya serikali kuimarisha ulinzi, Kenya bajeti ya ulinzi ni kubwa sana karibu mara mbili ya Tanzania, lakini vyombo vya ulinzi vimeshindwa kabisa kuzuia mashambulizi ya Alshabaab ndani ya Kenya, Alshabaab wanashambulia na kuingia katika ardhi ya Kenya vile wapendavyo, hapo ndio wakenya wanapaswa kujua kwamba taarifa za kwenye makaratasi ni tofauti na hali halisi.
Nyie hamjawahi pambana na magaidi kwa hivyo hamuwezi zungumza katika meza ya wazee. Mtapewa ruhusa ya kuzungumza punde tu mtakapoanza kupambana na shabab au boko haram au Isis au al qaeeda. Nyie endeleeni kupambana na rebels wa DR Congo.
Marekani mwenyewe ameshindwa kumuangamiza Taliban sasa Kesho atapiga mkataba na Taliban ili kusitisha uhasama.
 
Nyie hamjawahi pambana na magaidi kwa hivyo hamuwezi zungumza katika meza ya wazee. Mtapewa ruhusa ya kuzungumza punde tu mtakapoanza kupambana na shabab au boko haram au Isis au al qaeeda. Nyie endeleeni kupambana na rebels wa DR Congo
Hahahaha, andaeni makaburi" next week" Alshabaab wanachinja wakenya kama kumi na mbili.
 
KDF ilitakiwa kuweka kambi ya kudumu huko kaskazini. Fyokofyoko yoyote itaongelewa kwa kuwarambisha risasi na mabomu kadhaa hawa Al Shabaab.

Badala ya kuacha watu wazalishe mali wanawazidishia umaskini tu!
Watu wenyewe wazawa wa hapo wanawapa hifadhi alshabab kwa sababu wanaongea lugha moja na wanafanana. Wacha wakose waalimu ili washike adabu. Hatutaendelea kupoteza Wakenya ilhali wenyeji wanawaruhusu shabab kuishi miongoni mwao. Every action has an equal and opposite reaction.
 
Unacheka??
Kwasababu mnajifanya wajuaji sana, hamtaki kupokea ushauri, kila jambo mnajiona mnajua zaidi ya wengine, msiba wa kujitakia hauna rambirambi, hata kanisani huwa hatukubali kuendesha misa kwa mtu aliyejiua kwa makusudi
 
Hiyo ni dalili ya kushindwa kwa serikali yenu, nchi lazima ilinde raia wake katika mazingira yote, ukweli ni kwamba Kenya hamna umoja, wakazi wa pwani wanahisi kutengwa na serikali kuu, wapo tayari kuungana na mtu yeyote mwenye lengo la kuidhohofisha serikali ya Kenya. Lawama zote zimuendee mzee Jommo Kenyatta, badala ya kuanza kujenga utaifa kwanza, yeye alianza kujenga uchumi kwanza.
 
Kwasababu mnajifanya wajuaji sana, hamtaki kupokea ushauri, kila jambo mnajiona mnajua zaidi ya wengine, msiba wa kujitakia hauna rambirambi, hata kanisani huwa hatukubali kuendesha misa kwa mtu aliyejiua kwa makusudi
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuluza kati yako na Geza ni nani wazimu zaidi. Geza Ulole ana wivu na Kenya lakini hana roho mbaya kama yako. Huna ubinadamu
 
Back
Top Bottom