Alshabaab wavamia "bus" na kuuwa watu wengi huko Wajir, Kenya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Taarifa za hivi punde zinasema kwamba, watu wengi wameuliwa baada ya Alshabaab kuvamia basi la abiria jioni hii huko katika mkoa wa Wajir.

Wakati tunaendelea kuomboleza mamia ya wakenya waliokufa kutokana na mafuriko, huku tukisubiri kujua idadi ya waliofunikwa na jengo lililoporomoka huko Nairobi, Alshabaab wanatia pili pili katika kidonda kibichi kabisa. R.I.P.
 
Hawa jamaa wakiwalea kuna siku wataingia kabisa chumbani Nairobi.... Poleni wakenya
 
Alshabab si Marekani wanasema si kikundi cha ugaidi bali ni chama cha siasa?
Mbona Haya tena yanatokea?
 
Waislamu wenye msimamo mkali ambao wanataka dini Allah isimame kwa kuua watu. Astakhafilalh.
Hakika ni deen ya haki
Ficha ujinga kwa kukaa kimya kuliko kuropoka vitu usivyovijua kelbu we!
 
Hawa jamaa wakiwalea kuna siku wataingia kabisa chumbani Nairobi.... Poleni wakenya
Umesahau kutoka 2013 hadi 2015 walikesha na sisi Nairobi na kulipua matatu na mabasi na malls lakini tulipasua vichwa vyao taratibu hadi wakatulia. Wakabadilisha strategy. Sasa ni kushambulia maeneo karibu na border ya Somalia yaani Lamu, Mandera au Wajir na kutorokea Somalia kabla hatujawakamata kwani wanajua kitakachowafika tukiwashika. Sasa wanafanya kitu kinachoitwa hit and run maana wameshindwa kujitokeza waziwazi maana vichwa vyao vitapata shimo.
 
Ndo tatizo lenu linaanzia hapa.....mnapenda kujisifu mno...and when things turn upside down mnawaita bongolala wanaowakejeli...but anyway nimekuelewa... Na admire uwezo wenu sidhani kama hao wezi watakaribia hata Nairobi.....
 
Poleni sana jiranib, ndugu na watani wetu Kenya, hawa wapuuzi wekeni strategy ya kuwamaliza ibidi kuwafuata huko. Ikishindikana tushirikiane maana wataleta ghasia EA yetu
 
Hilo ndio tatizo lenu, kujipiga kifua wakati uwezo wenu ni mdogo sana. Hivi kwanini msisindikize hayo magari yanayokwenda katika maeneo hayo kama Tanzania tunavyosindikiza magari yanayokwenda mikoa inayopakana na Burundi?
 
Hilo ndio tatizo lenu, kujipiga kifua wakati uwezo wenu ni mdogo sana. Hivi kwanini msisindikize hayo magari yanayokwenda katika maeneo hayo kama Tanzania tunavyosindikiza magari yanayokwenda mikoa inayopakana na Burundi?
Wewe NI mpumbav,hivi polisi akisindikiza Basi Halitarushiwa risasi!Shukuru Mungu haya hayajatokea hapa kwetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…