Am I wrong if I process divorce?


Baada ya kupewa tips huku ndani na kutishwa kuwa kifuatacho ni kifo, kaamua kujiokoa nafsi yake. Ni uamuzi mzuri
 

Sure, atengeneze utaratibu ambao hautamuathiri yeye endapo huyo jamaa anahitaji kumuona mtoto. Na awe na msimamo, sio jamaa anakuja kukubembembeleza anaomba misamaha ya uongo na ukweli unalainika. Be strong [emoji123] kama umeamua kuondoka ondoka mazima.
 
Sure, atengeneze utaratibu ambao hautamuathiri yeye endapo huyo jamaa anahitaji kumuona mtoto. Na awe na msimamo, sio jamaa anakuja kukubembembeleza anaomba misamaha ya uongo na ukweli unalainika. Be strong kama umeamua kuondoka ondoka mazima.
Ni kweli sie wadada tunahuruma au sijui tuna hisia za namna gani, tunawezana kuumizwa lkn tukifanya maamuzi ya kuondoka unajikuta umerudi Tena😀😀. Huwa tunaamini mtu atabadilika lkn ukirudi unakaa wiki mambo ni yale unaanza kujuta na kujiona mjinga. Mungu
atusaidie.
 
Mmh umenikumbusha mdada fulani alinishindaga coz ana misimamo na mtazamo kama wako.

Kuna jinsi mume anataka mke wake aonekane/ abehave, ila mke hataki.

Wewe kinachokusumbua ni elimu na appearance yako.

Jaribu kutii anachokwambia mumeo, utaona manadiliko kwenye ndoa yako.

Hayo anayokufanyia ni impact ya tabia yako na vile unavyojiona.
 
Sasa hapo atii kitu gani jamani, kuvaa madera hadi ofisini? Na huko kutokutii kwake ndiyo chanzo cha mume kuandikisha nyumba jina la ndugu, kumpiga, kutoshiriki naye tendo la ndoa n.k? Hivi utii ni nini haswa? (Unipe somo dada ako kabla sijaachika[emoji188][emoji188][emoji188]).
 
Kutii kunakuja baada ya kupendwa, haya mambo yanaenda sambamba. Mkishaona mke ana elimu mnatumia hicho kigezo kuona hana utii. Muwe mnaoa wanawake ambao hawana elimu Ili msije pata shida baadae.
 
Unaongea as if wewe ndo mume unae zungumziwa hapa
 
Haki me wa hivo alinishindaga ndo nikaoa huyu mrs mito. Yaan alikuwa typical kama huyu dada, alikuwa mzuri wa sura na umbo matata, ana elimu, na kipato. Nikawa najisemea huyu kabarikiwa kila kitu, so nitafanya naye maisha safi kabisa. Weee mbona niliinua mikono nikasepa zangu.

Mimi napenda kuheshimiwa na mke wangu, mimi napenda mke mtiifu. Sasa wa hivi ukimwambia hiki sitaki, utashangaa ndo anakifanya zaidi, so tafsiri yake ni dharau na kiburi. Anakutia stress na kukufanya insecure.

Halafu unategemea kwenu kutokee tatizo then nitoe ushirikiano kama kawa, nyooooo!!!

Kifupi yeye ndo kamfanya mume amtreat hivo. Mume anajiona hana mke, bali mzazi mwenzie tu, ndo maana kaamua kufanya yake kimya kimya tu.

Dada yangu ukitaka kuishi vizuri na mumeo akikisha unajua nini anapenda na nini hapendi. Anavyovipenda viendeleze. Asivyovipenda anachana navyo. Kama mume hapendi uvae nguo za aina fulani, achana nazo. Au ukiacha utakufa?

Umejaliwa guu, umejaliwa tako, na ndo moja ya vitu vilivomvutia kwako. Aliviona wakati unatupia vimini, wakati ule unatupia viwalo vya kuchora tako.

Sasa kakuoa hataki u-expose mali zake, hataki uvae hizo nguo tena. Anahisi wanaume wengine watakutamani kama yeye alivyokutamani hadi akakuoa. Anahisi anaonekana kama kahaba, anaonekana kama bado yuko sokoni, anaonekana kama mavazi yasiyo na staha kwa mke wake. Sasa amekukataza mavazi ya hivo lakini wewe husikii tu, what so you expect? Unataka kufurahisha mumeo au wapita njia na wafanyakazi wenzio wakusifie?

Huyo dada ndo kamfanya mumewe awe hivo. Tena ukichunguza kwa makini hao wadada wenye wako tayari kugombana na mume wako kisa anamzuia 'kupendeza' utakuta hata siyo waaminifu kwa waume zao, ni chaeaters wa hatari.

Mwache tu aachike awe chakula cha mabahari huku mtaani.
 
Unaongea as if wewe ndo mume unae zungumziwa hapa
Yaan ni kama mimi kabisa my dada.

Nilishawahi kuwa na mdada wa dizain hiyo nikamshindwa kabisa.

Hapa hata sijasoma comments za wadau humu. Nimesoma alichoandika tu akanikumbusha kisa changu enzi hizoooooo

Ukikuta dada mzuri wa sura na umbo halafu ana elimu na kazi ya kipato cha maana tu, halafu bado anamtii mume wake na wala hamshiti, ujihesabu wewe ni mwanaume mojawapo wenye bahati
 
Kutii kunakuja baada ya kupendwa, haya mambo yanaenda sambamba. Mkishaona mke ana elimu mnatumia hicho kigezo kuona hana utii. Muwe mnaoa wanawake ambao hawana elimu Ili msije pata shida baadae.
Kupendwa ndo kulianza ndo maana nikakuoa wewe. Sasa wewe nimekuweka ndani sioni huo utii wako, unategemea nini?
 
Kaka mito acha kyzingua bana mtu akupangie had mavazi kisa kujiamini then asiwe responsible kwa familia kisa uzuri na appearance ya mkewe huyo jamaa tu ni mgonjwa usimtetee.
 
Pole, basi watu hawafanani huwezi kuconclude kuwa hana utii wakati hujaishi nae. Una majeraha moyoni
 
Dada hakuwa na shida uoga wako tu. Nimewahi kuwa na mkaka hajiamini hata akiheshimiwa yeye hugeuza gubu. Nawashauri wanawake wenzangu wawe na wanaume waliowazidi kila kitu Hadi dhambi aisee.
 
Unamzungumzia mkeo au mke wa nani? Huyu ni mke wa mtu mwingine
Wanaume wote ndo tulivyo dada. Tuunawapenda kwanza ndo tunawaoa. Hata jamaa naye ni hivo hivo alimpenda huyo bidada na ndo maana alimuoa.

Sasa bidada kaingia ndani, hataki kumtii jamaa, ndo tatizo lilipo japo.
 
Dada hakuwa na shida uoga wako tu. Nimewahi kuwa na mkaka hajiamini hata akiheshimiwa yeye hugeuza gubu. Nawashauri wanawake wenzangu wawe na wanaume waliowazidi kila kitu Hadi dhambi aisee.
Hamna, dada hakuwa na utii, alikuwa analeta ligi kama wa huyu jamaa

We mumeo au boy wangu akikwambia hataki uvae nguo za aina fulani, why hutaki kutii?
 
Wanaume wote ndo tulivyo dada. Tuunawapenda kwanza ndo tunawaoa. Hata jamaa naye ni hivo hivo alimpenda huyo bidada na ndo maana alimuoa.

Sasa bidada kaingia ndani, hataki kumtii jamaa, ndo tatizo lilipo japo.
Sio lazima iwe hivyo. Wewe jizungumzie mwenyewe inatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…