Haki me wa hivo alinishindaga ndo nikaoa huyu mrs mito. Yaan alikuwa typical kama huyu dada, alikuwa mzuri wa sura na umbo matata, ana elimu, na kipato. Nikawa najisemea huyu kabarikiwa kila kitu, so nitafanya naye maisha safi kabisa. Weee mbona niliinua mikono nikasepa zangu.
Mimi napenda kuheshimiwa na mke wangu, mimi napenda mke mtiifu. Sasa wa hivi ukimwambia hiki sitaki, utashangaa ndo anakifanya zaidi, so tafsiri yake ni dharau na kiburi. Anakutia stress na kukufanya insecure.
Halafu unategemea kwenu kutokee tatizo then nitoe ushirikiano kama kawa, nyooooo!!!
Kifupi yeye ndo kamfanya mume amtreat hivo. Mume anajiona hana mke, bali mzazi mwenzie tu, ndo maana kaamua kufanya yake kimya kimya tu.
Dada yangu ukitaka kuishi vizuri na mumeo akikisha unajua nini anapenda na nini hapendi. Anavyovipenda viendeleze. Asivyovipenda anachana navyo. Kama mume hapendi uvae nguo za aina fulani, achana nazo. Au ukiacha utakufa?
Umejaliwa guu, umejaliwa tako, na ndo moja ya vitu vilivomvutia kwako. Aliviona wakati unatupia vimini, wakati ule unatupia viwalo vya kuchora tako.
Sasa kakuoa hataki u-expose mali zake, hataki uvae hizo nguo tena. Anahisi wanaume wengine watakutamani kama yeye alivyokutamani hadi akakuoa. Anahisi anaonekana kama kahaba, anaonekana kama bado yuko sokoni, anaonekana kama mavazi yasiyo na staha kwa mke wake. Sasa amekukataza mavazi ya hivo lakini wewe husikii tu, what so you expect? Unataka kufurahisha mumeo au wapita njia na wafanyakazi wenzio wakusifie?
Huyo dada ndo kamfanya mumewe awe hivo. Tena ukichunguza kwa makini hao wadada wenye wako tayari kugombana na mume wako kisa anamzuia 'kupendeza' utakuta hata siyo waaminifu kwa waume zao, ni chaeaters wa hatari.
Mwache tu aachike awe chakula cha mabahari huku mtaani.