Unajua ni ngumu sana kwa mwanaume kumhandle mwanamke pisi kali, ana akili na anajiweza kiuchumi; wanaume wachache sana ndiyo wamefanikiwa katika hilo. Mimi nachoamini mwanamke yeyote independent especially kifikra sio rahisi kumpelekesha as majority of you hamtaki wanawake wa kuwatii; bali wanawake wa kuwapelekesha; kila kitu ndiyo mzee. Kwenu nyie utii is more of losing your self worth and your sense. As a result wengi wenu mnakuwa insecure; akikosea kidogo tu basi ushaconclude ni kwa sababu ni mzuri na ana kipato; kwani wabaya na wasio na vipato ndiyo wanyenyekevu wote? Wangapi wameoa wanawake wa kawaida kabisa na still ndoa zao zimevunjika? Utii ni tabia ya ndani kabisa ya mtu, regardless of her status. Mama Samia ni Rais, ila you can tell yule mama ni mnyenyekevu tu wa asili.
Mnatukimbilia sisi wenye sura za wajomba, na shape za kina babu + mangumbaru: kwa sababu mnahisi hatuna options nyingine, zaidi ya kuwatii. Ni wale wanawake ambao mnajua hawatongozwi sana, unamfanya utakavyo na yeye hatoondoka kwa sababu hana huwezo wa kujihudumia; in short hatuna options. Hata wanawake wengi wanaonyanyaswa na mnawaita wavumilivu; wengi si wavumilivu kweli kwamba ndiyo asili yao; ni vile hawana pa kwenda, bora tu abaki hapohapo ambako ana uhakika wa kula ugali, ila siku akipata pa kwenda atatoka ndukiii. Utii au uvimilivu wa design hii, ni wa kinafiki na ni wa muda tu. Hakuna raha kama mwanamke anajiweza afu bado anakutii; raha kichizi.
Mume wa huyu dada hajiamini na hamwamini mkewe, anawaza kuchapiwa tu muda wote. Anachokitaka yeye ni kumfubaza mke wake ili asionekane kwa wengine. Bahati mbaya, mzuri ni mzuri tu hata akivaa gunia; chukulia mfano yule muigizaji Batuli, most of times anavaa nguo za heshima and yet wakware udenda unawatoka. Ndiyo huyo bwana anajikuta mara leo nyoa, kesho suka, ooh vaa dera; hivi unalijua trako la ndani ya dera wewe, si bora tu avae vitenge? Na kwa mwanaume asiyejiamini, hata ufanyaje hatokuona mtii. Kila siku anakuja na jipya ana anataka umfuatishe tu kama bendera; yeye mwenyewe hajui hata anachokitaka kwa mkewe afu bado mke amtii aseeeeeee
Mahusiano yoyote kucompromise lazima kuwepo, ili angalau tukutane mahali fulani pazuri. Lakini pia, unapomuhitaji mwenzako abadilike/kupunguza kitu fulani; jua itachukua muda kutokea au penginepo lisitokee kabisa. Imagine mdada ambaye maisha yake yote anavaaga mawigi, leo all of a sudden unamtaka atupe mawigi chini; do you think ni rahisi hivyo? Na ni bora hata sisi huwa tunawasikiliza; jikute sasa unamwambia mume wangu acha kitu fulani au rafiki fulani si mzuri kwako; afu yeye hivyo vitu awe anaviona kwake havina madhara; utajua haujui. So kuna muda tuwape watu nafasi ya kuona mambo kwa jicho tunaloliona sisi, ikishindikana tunajifunza kuwachukulia madhaifu yao as long as hayatuletei madhara. You will never please an insecure person, neverrrr.