Am shook: for Tanzanians who dont understand simple lingua

Katika jambo linalonishangaza na bado sipati jibu ni wakenya kuwa very comfortable na kutoijua lugha yao ya taifa, lakini kuwa very uncomfortable kwa kutojua kiingereza, naomba mnieleweshe kinachoendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Typical Tanzanian misconception of Kenya.
Aliyekwambia waKenya hawajui Kiswahili alikudanganya. Kiswahili ndio lugha inayotumika kwa kawaida. Nairobi, hasaa mitaa ya Eastlando, imetupatia Sheng' mchanganyiko wa Kiswahili, Kiingereza na lugha zinginezo za mama. Kiswahili cha bongo hakijaongezea kwa lugha hii labda kuyatamka maneno kwa kuyalegeza legeza na kuyatafuna; mfano, Salama ikawa kati ya Sarama na Sayama, Barabara ikawa baabaa. Lexicographicide I'd say!
Ningependa kuona mKenya anayehitaji msaada wa kutafsiriwa huku bongo. La kumkanganya mKenya ni kasi na rafizi ya mBongo anpofungua mdomo, maneno mengi na ya mzunguko; mfano, Kenya salamu ni 'Habari yako - Mzuri' bas, Bongo 'Habari za Mda, Kwema, Mzima, Pole kw kazi, Upo' yote hayo na nikupita mnapitana barabarani.
So ndugu zangu waTZ, beef ni ya nini mnayo hivi na Kenya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo salamu za mzunguko ni za wazazi wetu enzi za ujima.

Wewe ndiyo umeleta mzunguko.

Hiyo sentensi "Beef ni ya nini mnayo hivi na kenya" ni mzunguko mno na hauna maana kisemantiki, ungeandika tu "Mna ugomvi gani na Kenya?"
 
Twende taratibu kijana, utanielewa tu lengo langu, ni ukweli kwamba wakenya wengi hasa serikalini hawako comfortable kabisa kujieleza kwa ufasaha kwa kiswahili, hata Uhuru Kenyata mwenyewe, hawezi kujieleza kwa ufasaha kwa kiswahili kama afanyavyo kwa kiingereza.

Jambo linalonishangaza zaidi ni kuona shughuli zote za kitaifa, kama vile vikao vya bunge, mahakamani na hata hutuba karibu zote za kitaifa zinafanywa kwa kiingereza wakati lugha rasmi ya Kenya ni kiswahili, mbona mnajichanganya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani msikubaliane kwamba lugha rasmi ya taifa lenu ni kiingereza na kiswahili kiwe ni lugha ya pili ieleweke wazi, inaonekana kama mnajilazimisha kukifanya kiswahili iwe lugha ya taifa lakini moyoni hamkikubali, hamkipendi matokeo yake kinawasumbua sana, naomba mnifafanulia bila ushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Oii
Official languages of Kenya are English and Kiswahili...according to Wikipedia...
 

Kiswahili ni lugha yetu rasmi, lugha ya taifa tena ambayo imetajwa kwenye katiba kabisa, lakini hata hivyo ni lugha yenye mapungufu, ni vigumu kujieleza kwa kutumia Kiswahili mwanzo hadi mwisho bila kuchakachua. Hata hiyo Tanzania bado mna vitu vingi sana vimeandikwa kwa lugha ya Kingereza, japo mnajitahidi kuegemea upande wa Kiswahili.

Nimekua hapo Dar es Salaam, nilikuja kuwasilisha ombi (proposal) kwa ajili ya mradi fulani. Sasa juzi nilipoitwa tukaja na wezangu kujieleza, aisei nilishangaa mahojiano yalikua kwenye lugha ya kingereza, dodoso zote ilibidi tujaze kwenye hiyo lugha kwa kwenda mbele.

Mwanzo nilikua nimejiandaa kujieleza kwa kiswahili japo shughuli yenyewe (monitoring & evaluation) ina misamiati ambayo tafsiri yake kwa kiswahili ni balaa. Hapa tu baadhi ya misamiati ambayo ilinipa shida kuweka kwa Kiswahili, Baseline assessment, Bias, Conceptual Framework, Cost-Benefit Analysis, Cost-Effectiveness Analysis, Triangulation, DOPA Indicators, Efficacy, Exogenous Indicator, Formative Research, Hawthorne Effect

Nilifurahi pale jamaa waling'ang'ania kwamba tufanye yote kwa Kingereza, na ndivyo ilikua hata kwa washindani wetu.
 
Official languages of Kenya are English and Kiswahili...according to Wikipedia...
lugha ya taifa la Kenya rasmi ni Kiswahili, hii huitaji kuangalia kwenye wiki pedia, kama ambavyo ukiulizwa rangi ya ngozi ya wakenya ni ipi, utasema ni nyeusi...according to wikipedia?...watakucheka watu, japo watu wenye rangi tofauti kama wahindi, wazungu na wengine wengi, i



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daima MTUMWA HAACHI KUMWONA BWANA WAKE NI BORA KULIKO YEYE. WANABABAIKIA UZUNGU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Boss...whatever...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…