MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Hao watu wa ulaya unawapokea kwa sababu wanakuja kufanya na wewe kazi kwenye mradi ambao unakuwa umeomba kuufanya hapa nchini! Ni lazima uwapokee maana wewe ndo mwenyeji wao! Hii haimaanishi kuwa hakuna mtanzania asiyeweza kuwapokea hao wageni wako! Na kingine ukumbuke kuwa kibali chako cha kufanya kazi hapa nchini sio cha kupokea wageni au kuwa mkarimani, bali ni cha kufanya kazi nyingine ndo maana unaishia kuwapokea tu hao washirika wako na kwenda kufanya mradi wenu.
Hivi nikuulize, watu wote kutoka nchi za ulaya na marekani wanaokuja hapa huwa wanapokewa na wakenya? Au je kama watanzania hawajui hicho kiingereza, hao watu wa mataifa mengine huwa wanafanyaje kazi zao?
Na kitu kingine ambacho unatakiwa ukifahamu, japo najua unakifahamu ni kuwa wewe pamoja na wakenya wengine mnaofanya kazi hapa Tanzania mnazifanya si kwa sababu kuwa watanzania hawawezi kuzifanya, bali kwa sababu ya ushirikiano na makubaliano kati ya taifa na taifa.
Nashindwa jinsi ya kukujibu maana unatoka nje ya hoja, hamna sehemu nimesema nawapokea wageni Tanzania kisa hamna Watanzania wenye uwezo huo. Tatizo lako huwa unachanganya siasa kwenye hoja ilmradi ushinde lakini sio kwa nia ya kuwekana sawa kimantiki.
Pili, hamna sehemu nimesema kwamba kazi wanazofanya Wakenya haziwezi kufanywa na Watanzania, wapo lakini lazima ujiulize kwanini kampuni ya Mtanzania imfuate Mkenya, iingie gharama ya usafiri wa ndege KQ, iingie gharama zote za hoteli na matumizi atakayotumia huyo Mkenya au Mhindi au hata Mmarekani wakati shughuli yenyewe inaweza kufanywa na Mtanzania hapo Dar tena kwa ada nafuu. Sidhani kama uhusiano wa mataifa tu ndio kigezo cha makampuni yenu kuingia gharama zote hizo.
Japo hayo yafungulie mada tutayajadili, hapa sio pake, tunajadili masuala ya lugha zinazopewa kipaumbele na kutoleana mifano.