Am shook: for Tanzanians who dont understand simple lingua


Nashindwa jinsi ya kukujibu maana unatoka nje ya hoja, hamna sehemu nimesema nawapokea wageni Tanzania kisa hamna Watanzania wenye uwezo huo. Tatizo lako huwa unachanganya siasa kwenye hoja ilmradi ushinde lakini sio kwa nia ya kuwekana sawa kimantiki.

Pili, hamna sehemu nimesema kwamba kazi wanazofanya Wakenya haziwezi kufanywa na Watanzania, wapo lakini lazima ujiulize kwanini kampuni ya Mtanzania imfuate Mkenya, iingie gharama ya usafiri wa ndege KQ, iingie gharama zote za hoteli na matumizi atakayotumia huyo Mkenya au Mhindi au hata Mmarekani wakati shughuli yenyewe inaweza kufanywa na Mtanzania hapo Dar tena kwa ada nafuu. Sidhani kama uhusiano wa mataifa tu ndio kigezo cha makampuni yenu kuingia gharama zote hizo.

Japo hayo yafungulie mada tutayajadili, hapa sio pake, tunajadili masuala ya lugha zinazopewa kipaumbele na kutoleana mifano.
 
Haha nakuelewa sasa. Serikali yetu ndio iliweka kiswahili kama lugha ya taifa. Sasa serikali yenyewe ndio inaweza badilisha hilo ila sio wananchi wa kawaida kama mimi. Jambo jingine ni kuwa sidhani kama Wakenya wanaeza kubali serikali itupilie mbali kiswahili. Nahisi kama umeishi Kenya na unajua vizuri kuwa sisi wananchi wa kawaida tunaitumia kiswahili sana kushinda Kiingereza. Kiingereza kinatumika tu shuleni, bungeni au ofisi za serikali. Nikienda dukani nitaongea na mwenye duka kwa lugha ya kiswahili. Jirani zangu nawaongelesha kutumia hio hio kiswahili. Mkenya wa kawaida anatumia kiswahili sana kwa maongezi yasiyo rasmi (informal communication).Japo kiswahili chenyewe ni kibaya kushinda ya Watanzania. Hata mimi mwenyewe kiswahili changu si kizuri sana.Ila kuna Wakenya walioishi T.Z kama Mk254 ambaye kiswahili chake kimetukuka kweli kweli. Wakenya wanatumia kiswahili sana ila wanachanganya na Kiingereza au lugha ya mama. Hapo kwa Wakenya kuchukia kiswahili, sijui kama hio ni sahihi. Ninachojua ni kuwa lugha unayotumia kila siku japo kwa kuchanganya na lugha nyingine ni lugha unayoipenda. Kwa hivyo Wakenya waipenda kiswahili ila matumizi ndio mabaya. Hata American English ni mbaya sana ukilinganisha na British English ambayo ndio lugha rasmi ya Kiingereza. Samuel999 alisema "am shook" ambayo ni American English. Watanzania wengi wakamkosoa kuwa angesema "am shaken" ambayo ni British English. Kuna Kenyan Swahili na kuna Tanzanian Swahili
 

Kaka naona tunazunguka mbuyu na hadi milele sioni kama tutaelewana, maana unakokwenda sio nilikokutuma.
Watanzania mnajifunza lugha ya Kingereza, tena ipo kwenye mtaala wenu, lakini kujifunza ni jambo moja, ila kuitumia ni jambo lingine tofauti. Wengi mnajifunza, hata kuingia darasa za ziada za jioni, lakini kama nilivyosema hapo awali, ujuzi wa lugha ni sayansi ambayo lazima uitumie ili ikufaidi, la sivyo utaishia kuijua kinadharia tu.

Wengi mkitahiniwa Kingereza mnapata alama nzuri, lakini mkiambiwa mjieleze mnaishia kuyumba kwenye matamshi maana hamjazoea kuitumia.

Nimekuambia Wachina na hao Wajerumani hatuwezi kutunishiana misuli au kuwaiga leo kwa mpigo maana tamaduni zao walizianza miaka zaidi ya 500 ambayo hata sidhani hicho Kiswahili kilikua kimebuniwa. Na hata kama kilikuwemo, Watanganyika wengi hawakua wanakitumia, wengi wenu kutokea Usukumani na kwengine mumechangamkia Kiswahili miaka ya hivi majuzi tu.

Kenya imetangaza Kiswahili kama lugha ya taifa, ila kila mmoja wetu ana uhuru wa kutumia lugha yoyote kufanikisha shughuli zake bila kushinikizwa. Lugha ni desturi na tamaduni, hauwezi kuwalazimisha watu, kumbuka pia Wakenya hawajazoea kufungiwa ndani kama Watanzania, sisi kwetu tuna hulka ya kuhoji, ni vigumu sana leo hii rais wa nchi aibuke na kauli za kusema sote tutumie lugha moja na ifanikishwe, atabishiwa hadi aikimbie nchi. Ndio Kenya ya Wakenya ilivyo....watu matata sana, waliofunzwa kuhoji na kutokubali chochote kisa dola imeamrisha, lazima kiwe na mantiki na kueleweka umuhimu wake ndani ya jamii.
 
Tony 254 amenielewa vizuri, soma jibu lake hapo juu kabla ya jibu lako, taarifa zilizotolewa katika report ya mwaka huu 2017 rsf.org unaweza ukagoogle imeiweka Tanzania katika nafasi ya 83 na Kenya 95, katika uhuru wa habari, freedom of expression, hiyo ni baada ya Magufuli kuwa madarakani kwa zaidi ya mwaka akaanza fujo zake za kukandamiza uhuru wa kujieoeza, kabla ya hapo Tanzania ilikua juu sana, kwa hiyo kujipiga kifua kwamba Kenya wapo huru na wanahoji sana kuliko watanzania sio kweli, kwa upande wa demokrasia Kenya haijawahi kuizidi Tanzania hata mwaka mmoja tangu tumepata uhuru, kama unaushaidi ulete hapa hadharani tuone, ila kwa tabia hii ya Magufuli tusipoangalia hiyo gape ya 12 points inaweza kushuka.

Kuhusu lugha ya taifa, bendera na mwimbo wa taifa, hivi ni vitambulisho vya taifa, ni tunu za taifa, hakuna taifa linalolazimishwa kuwa navyo, lakini mkiamua kuwa navyo, lazima vitajwe kwenye katiba ambayo ni sheria mama ya nchi husika na lazima viheshimiwe, lazima vilindwe na lazima watu wavitii, sio hiari kuitii bendera ya Kenya kwa mkenya yoyote, ni lazima, wimbo wa taifa sio hiari ni lazima kuutii na kuuheshimu. Tukija kwenye lugha ya taifa, lazima taifa liitumie lugha yake ya taifa katika kazi zake za serikali, lugha ya taifa na pesa ya taifa vina thamani sawa ndani ya nchi, huwezi ukasema wakenya wana hiari ya kutumia pesa ya nchi yoyote ile akiwa katika ardhi ya kenya, ukiona nchi inaruhusu matumizi ya pesa za kigeni ovyo ovyo tu, ujue hiyo nchi inapoteza udhibiti wa uchumi wake. Vivyo hivyo ukiona nchi inaruhusu lugha nyingine zitumike hovyo hovyo katika ofisi za serikali, yaani serikali haitumii lugha yake ya taifa katika shughuli za serikali na za kitaifa, hiyo nchi inapoteza utengamano wa taifa lake.

Ninarudia,nsijawahi mimi kujua nchi yoyote duniani ukiondoa Kenya, ambayo kwenye katiba wanaitaja lugha ya taifa, lakini shughuli zote zankiserikali na za kitaifa zinafanyika kwa kutumia lugha ya pilinaunya tatu, kama unaijua ninakuomba unijulishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania vilevile kiswahili na English ni lugha rasmi, ni juzi tu bills na ansad za bunge zimeingizwa kwenye kiswahili zamani walikua wanaruhusiwa kuchangia kwa English au kiswahili lakini ansad lazima iandikwe in English so hata sheria zote zilikua kwa English
 
Asante sana kwa kunielewa, jaribu kumfafanulia MK254 aweze kuelewa nini ninataka kukieleza. Ni kweli unalosema, serikali ndiyo yenye jukumu la kusimamia na kulinda uhuru, tamaduni, sheria na tunu za taifa ili kulifanya taifa liwe imara, kiuchumi, kiutamaduni, kiulinzi na usalama na kuhakikisha umoja wa kitaifa unakuwepo na kudumishwa, lugha ya taifa ni kitu muhimu sana katika kdumisha umoja wa taifa, ndiyo sababu lugha ya taifa inatajwa katika katiba ya nchi, kinachonishangaza kwa serikali ya Kenya ni kwamba serikali yenyewe ndiyo inayoongoza kwa kuacha kuitumia lugha yake yenyewe iliyoichagua bila kilazimishwa na mtu yeyote, kama serikali iliona bado mazingira hayajawa tayari kwa taasisi mbalimbali za serikali kuanza kutumia kiswahili, wangeendelea na kuifanya kingereza kuwa ndiyo lugha ya taifa, wala hapakuwa na ulazima wowote wa kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha ya taifa wakati serikali yenyewe haitumii lugha yake, sasa itawezaje kuwaambia wananchi wajifunze kiswahili wakati wakienda kupata huduma serikalini wanakutana na kiingereza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuunga mkono ukweli wakenya wanajua kiswahili sana na misamiati mingi sana ya TZ inatokea Kenya.Sema wenzetu walichotuzidi ni lugha ya English maana wao wanaanza nao from primary school ila kwa kweli i like Kenya Swahili ACCENT Unasikia ninakwenda kwa duka
 

Nimesoma bandiko la Tony254, na sioni wapi amekinzana na kauli zangu, ila kumbuka kila mtu ana uhuru wa kuwasilisha mawazo yake. Ni uhuru ambao sisi Wakenya tunajua utamu wake.

Halafu hilo la Tanzania kuizidi Kenya kwenye hayo ya uhuru wa kujieleza na mengineyo inawezekana kuwa kweli kwa sababu Watanzania hawana utamaduni wa kuhoji, wengi wenu waoga wa kutupwa. Hivyo dola ya Tanzania haijajipata kwenye changamoto za kupambana na watu wasiotulia, ni juzi tu mumeanza kuona dalili za mwamko wa watu, ila Kenya viongozi sampuli ya Tundu Lissu ni lukuki, yaani wengi mno, hivyo serikali yetu imekua siku zote kwenye hali ya mapambano na ndio maana inaonekana kama ipo nyuma kwenye hayo ya demokrasia.

Sasa nyie siku chache Tundu Lissu anawapigia makelele mnaanza kumpima mkojo na mengine, mngekutana na mtiti wa Kikenya sijui mngetokea wapi. Kwa mfano nawaza hapa, itokee Raila Odinga apigwe marisasi halafu alazwe hospitalini, aisei inabidi kuihama nchi maana panachimbika mpaka basi.

Hayo ya lugha, kama nilivyokuambia hauwezi ukawalazimisha watu waliokua wamezoea kutumia mchanganyiko wa lugha kadhaa kwamba uwafungie kwenye moja ghafla. Katiba tumeandika juzi na kuweka Kiswahili kama lugha ya taifa, lakini hata hivyo tuna uhuru wa kutumia lugha tunazotaka ili kufanikisha malengo yetu. Unaweza ukamlazimisha mtu atii bendera, rangi, nyimbo n.k. Lakini kumuingilia hata kwenye lugha, huko ni kufanya watu watumwa na unawalemaza kiakili. Maana kila mmoja wetu amezoea kutumia lugha fulani kuwaza na kupanga matakwa na malengo yake.

Kwamba hujasikia nchi yoyote inatumia lugha ambayo haipo kwenye katiba, hiyo sio issue kubwa, sisi ndio wa kwanza, hivyo weka kwenye kumbukumbu zako kwamba sisi tumevunja rekodi kwa hilo dunia yote.
Halafu nyie hapo mna mikataba na stakabadhi nyeti zimeandikwa kwa lugha isiyo ya kwenu, hivyo sio jambo kubwa japo unajifanya kushangaa kiunafiki.
 
Kwanza ninakupongeza kwa kukubali kwamba Tanzania ipo mbele sana ya Kenya kwa demokrasia, sasa hayo uliyosema kama ni sababu ndizo zilizosababisha Tanzania kuizidi Kenya ni maoni yako tu, unahaki ya kusema upendavyo, ila waliofanya hizo tafiti wametumia vigezo vingi sana, ila mimi ninachoweza kukuambia ni kwamba yule yule aliyeifanya Tanzania kujitolea kuwasaidia waafrika waliokuwa wanaonewa huko kusini mwa afrika pamoja na kwamba tulikuwa fukara wa kutupwa, na yeye mwenyewe japo aliichukua nchi yenye ardhi kubwa yenye rutuba na madini ya kila aina, lakini amekufa akiwa na gari moja, na shamba lisilozidi hekari 50, na hana pesa bank, kwa sababu alikuwa anajali sana UTU kuliko mali, ndiye aliyejenga umoja na demokrasia katika Taifa la Tanzania, katika kipindi chote cha miaka 23 aliyokaa ikulu hakuna hata tukio moja la kuuliwa kwa mwanasiasa yeyote au jaribio kama hili la Tundu Lisu.

Unadai kwamba akiuliwa Raila hapata kalika, kwanza elewa kwamba hadhi ya Raila kwa Kenya huwezi kulinganisha na Tundu Lisu, Raila ni sawa na Luwasa huku Tanzania, Tundu Lisu hana wafuasi kiasi hicho, yeye ni mtu wa publicity zaidi. Lakini ninahisi umesahau kwamba Kenya wameuliwa watu wengi sana maarufu na nchi inasonga mbele, Tom Mboya, Pio Gama Pinto, Robert Aoko ni baadhi tu ya majina makubwa Kenya na Afrika, mliwauwa Kinyama na nchi imesonga mbele.

Kuhusu lugha kwamba mko huru kufanya mnavyotaka, hapo ndiyo ninahisi ama hujanielewa au hutaki kukubali kama alivykubali Tony254, ila ninakubaliana na wewe kwamba Kenya ni nchi pekee duniani ambapo kitaba yake inasema vingine, nchi inatekeleza kinyume na yale waliyojichagulia wenyewe, Ila kumbuka kwamba, pesa ya taifa, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, lugha ya taifa, na mipaka ya taifa, ni tunu za taifa ambavyo dola lolote duniani ni lazima ivihifadhi kwa gharama zote na kuvilinda, kama ilivyo pesa kwa serikali kufanya matumizi yake ya ndani kwa kutumia pesa yake ya taifa, ni lazima pia ifanye shughuli zake za ndani kwa kutumia lugha ya taifa, ndiyo sababu kule juu nikasema Kenya is a confused country as far as language is concern, kwa sababu hii haiko kokote duniani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu kwamba nchi hii haijapata wanasiasa machachari, ndiyo tunaanza na Tundu Lisu, kwanza ujue kwamba Tundu Lisu alikuepo tangu utawala wa Kikwete, na wala hakuna mtu aliyemgusa, hii inaonyesha kwamba tuna wanasiasa machachari kuliko hata huko kwenu, ulishawahi kukutana na moto wa Mtikila?, huyo Tundu Lisu ni cha mtoto kwa mtikila, nani aliangaika na Mtikila, tatizo sio kutokuwa na wanasiasa machachari, tatizo ni Magufuli tabia yake ya kushindwa kuwavumilia wapinzani, ila akimaliza kipindi chake, kila kitu kitarudi kama zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nilishasema kuwa mimi sio mwanasiasa, hivyo sio sawa kuhusisha maoni yangu na mtazamo wa kisiasa!

Kuhusu kuwa hujasema kauli nilizofafanua kwenye andiko langu lililopita ni kuwa, yawezekana kweli hujasema moja kwa moja,lakini kauli yako ikaashiria hivyo maana hii ni SARUFI na kazi zake ndo hizo! Ndo maana nikakufafanulia ili kuweka kumbukumbu sawa!

Mwisho ni kuhusu baadhi ya kampuni kuchukua watu kutoka kenya kuja kufanya kazi ambayo inaweza kufanywa na watanzania, jibu lake ni dogo sana ila la kufikirisha tu! Ntakujibu kwa kulinganisha labda na ukandarasi wa barabara! Hapo Kenya wapo wahandisi wengi na wazuri kabisa, lakini utashangaa kampuni flani kutoka nje inapewa zabuni ya kujenga na kuziacha kampuni za ndani wakati zina uwezo na kila kitu kwa ajili ya kazi kama hiyo! Hiyo ipo kwa nchi na makapuni mengi sana, hasa kwa hizi nchi zetu za kiafrika ambazo bado hazijaendelea/zinazoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…