Kisa hiki kimenikumbusha kitu, siku moja nilipanda dala dala kutoka kituo cha mabibo hostel kuelekea Tabata, kituo kilichofuata (kinaitwa extenal) alishuka mtu nikapata siti nikaketi maana gari lilikuwa level siti tulienda mbele kidogo na kituo kilochofuata (kinaitwa garage) aliingia mama mmoja mtu mzima kidogo nilisita kumpisha siti maana nlikuwa nimechoka na najihisi kuumwa pia gari likiwa bado level siti zaidi yule mama tu ndo alisimama niliona isiwe tabu ngoja nimpishe Nilimuita akaja kuketi akashukuru pia. Vituo vilivyofuata gari ilijaza abailia hakuna mfano hadi mtu inakubidi usimame na mguu moja ndio upate balance, nakumbuka kama kituo cha tano aliinuka mwingne karibu yangu nikakaa na hivyo nikawa sija loose chochote, mfukoni nilikuwa na 35,500 tu. Nikampa konda 500/= ikarudi 100.
Kisa kipo hivi Wakati nashuka ile pesa 35,000 niliiacha kwenye siti nikashuka nikiwa sina hili wala lile' niliitwa na yule mama akaniambia naona umeacha pesa yako hapa. Nikajicheki kweli sina pesa yoyote mfukoni. Nilijiuliza mara mbili mbili imekuwaje huyu pekee ndiye aliyeona hizi pesa nikakumbuka ule wema niliomfanyia haya ndiyo malipo yake.
Nilimshukuru maana nilikuwa sina kitu sio cash wala mpesa nipo mweupe nimebakia mapumbu matupu.
Kila wema hulipwa! Hujui ni lini au nani atalipa.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu ni kweli kabisa, wema huwa unalipa sana ingawa ni mara chache na ni bahati sana kwa tukio kama ambalo limemtokea huyo dogo hapo. Mimi ni shuhuda wa tukio kama hilo, linafanana kwa asilimia nyingi sana na hilo, mpaka leo naona kama ilikuwa ndoto.
Ilikuwa hivi;
Nakumbuka ilikuwa ni miaka kadhaa nyuma nikiwa mwaka wa pili Chuoni, 'tuliibana' mimi na aliyekuwa rafiki yangu wa kike kipindi kile (kwa sasa ni mke wangu) kwenda Morogoro mwishoni mwa wiki. Tulifikia kwenye hotel moja (jina kapuni - Iringa road nje kidogo ya mji) ambayo mara kwa mara tulikuwa tunafikia tukienda Morogoro.
Tulifika siku ya Ijumaa mchana na lengo ilikuwa ni kupumzika na kuondoka Jumatatu asubuhi. Tulilala usiku wa Ijumaa fresh, Jumamosi hatukushinda pale ila tulirudi usiku tukalala, siku ya Jumapili tuliamka mapema tukaenda Kanisani, sasa tuliporudi tukaishia restaurant (hii restaurant imo ndani ya hiyo hotel), kwa lengo la kupata chakula cha mchana.
Wakati tupo pale tunasubiria huduma wakaja jamaa wawili na mhudumu wa ile hotel (huyu alikuwa ni hotel manager, nakumbuka). Kwakuwa tulishakuwa wenyeji pale, yule mhudumu akatutambulisha kuwa;
" hawa jamaa ni wateja wenzenu wamefika leo, kwahiyo watakuwepo hapa mpaka kesho." Tukasalimiana nao, wakaomba kampani, kukaa na sisi meza moja kwasababu (sehemu zingine zilikuwa zimejaa).
Tukapata nao chakula na stori 2,3 na utani wa hapa na pale, jamaa walikuwa wachangamfu sana, wacheshi mno sio rahisi kuwawekea mashaka kama walikuwa
majambazi. Tulipomaliza kula, tulipokuwa tunalipa msosi jamaa walitukatalia, wakasema wao watalipa, na sisi tukakataa, basi baada ya mvutano wao wakalipa vyakula (vyao na vyetu) na sisi tukalipia vinywaji (vyao na vyetu).
Mmmoja wa wale jamaa alikuwa akilalamika kuwa tumbo linamuuma kabla hata ya chakula, na muda ulivyokuwa unaenda bado alikuwa akilalamika. Mimi na huyu binti (mke wangu sasa) tulitoka tukaenda town, tuliporudi tukamletea jamaa dawa za tumbo, jamaa akatushukuru sana, sisi hao tukaingia zetu chumbani tukapumzika, hiyo ilikuwa mida kama ya saa 9 jioni.
Ilipofika saa moja kama na nusu usiku tukamuagizia mhudumu msosi akatuletea chumbani, tukala tukalala. Watati nipo katikati ya usingizi nikasikia mlio kama wa mtutu wa bunduki, sijakaa sawa nikausikia mwengine, nikaamka nikamuasha mtu wangu nikamuambia kuwa mambo sio mazuri pale tulipo. Hatujakaa tena sawa, tukasikia vishindo kwa nje ya dirisha letu kama watu wanaokimbizwa, kumbe jamaa walikuwa wanawakamata wahudumu wote wa hoteli, waliwafunga kamba mikononi na miguuni na kwenda kufafungia Jikoni.
(Inasemakana mpaka tukio linatokea jamaa walifikia kuwa 6 kwa idadi).
Wakabakia na yule meneja wa hotel na kumuamuru awapeleke chumba fulani na wanamhitaji mtu fulani, walimtaja kwa jina
(Inasemekana kuna mteja alikuwa chumba fulani ndiyo ilikuwa target yao). Walimpata, ila walikosa wachokihitaji kwake (dau walilomkuta nalo silo walilodhamiria) wakampora na kumpiga risasi miguuni na mgongoni.
Hasira zao zikahamia kwa wateja wengine baada ya kukosa kwa jamaa, walipita chumba kimoja baada ya kingine. Mteja ambaye alikaidi kufungua Mlango jamaa walivunja wenyewe. Kila chumba walichopita walidhuru watu kwa mapanga ama risasi, Tulisikia vilio na milio ya bunduki, walipita vyumba vyote.
Sasa walipofika chumbani kwetu wakavunja Mlango, sisi tulikuwa tumepiga magoti tukisali, kufumbua macho nakutana uso kwa uso na mmoja wa wa wale jamaa tuliokuwa tunakula nao mchana ameshika bastola &Kisu mkononi, alipotugundua tu akapiga risasi juu na kutoka. Nilihisi kama nilipoteza fahamu. Sikusikia kitu chochote baada ya pale, kumbe jamaa walikuwa wameshakimbia. Polisi walifika baadaye sana, (nimefupisha habari).
Kwahiyo haya mambo huwa yanatokea, tena kama sisi ingekuwa ni rahisi sana kuhusishwa na hao viumbe kumbe tulikuwa hatuwafahamu kabisa wala mipango yao kabla ya pale. Kwahiyo hata huyu dogo wa Kenya inawezekana hahusiki kwa njia yoyote. Ninaamini kabisa ni vile tulivyowathamini mchana pale kwenye msosi ndio ilikuwa pona yetu.
Jumapili njema.