Ama M23 wataiteka Goma au majeshi ya SADC yataingia Ikulu Kigali

Ama M23 wataiteka Goma au majeshi ya SADC yataingia Ikulu Kigali

Kwamba Rwanda wanaweza kuwashinda Afrika Kusini, taifa ambalo linatengeneza kila aina ya silaha ya kivita hapa duniani, kuanzia Infantry Fighting Vehicles, Tanks, APCs, Attack Helicopters, Ballistic Missiles, Fighter Jets, UAVs and Heavy Artillery. Wanawauzia silaha nzito mataifa kama Ujerumani, India, UAE, Philippines na Kuwait. Mashabiki wanaposema kwamba M23 wanaweza kuvishinda vikosi vya Afrika Kusini, Malawi, Tanzania na Congo huwa nashangaa na napata ukakasi sana.

Kiuhalisia M23 wanaweza kusumbua kwa muda kwasababu wanayafahamu mazingira (Terrain) vizuri kuliko wageni na wanaungwa mkono kisiasa na raia wao (Political Support). Wanajeshi wanaweza kudhurika kwa muda mfupi, kwasababu mpaka sasa wanapambana vita ndogo, Asymmetric Warfare and Sporadic Engagement, lakini endapo vita itakuwa kubwa na kurefushwa sidhani kama M23 wanaweza kupambana hata mwezi.

Jambo ambalo watu wengi hawalifahamu ni hili, silaha za M23 na waasi wengine zinatoka kwenye BLACK-MARKET nchini Ukraine, Libya, na Sudan, kupitia Central African Republic, South Sudan, Uganda na Rwanda hadi Congo. Hivyo mbali na huu mgogoro kuwa kuonesha kwamba ni wa kisiasa, kiuhalisia ni mgogoro wa kiuchumi. Watu wanatajirika kwa kuuza silaha, kutoa mafunzo na kueneza ushawishi. Endapo itatokea vita kubwa, basi moja ya wanufaika watakuwa ni Afrika Kusini.

Tofauti na mwaka 1998, The Great Congo War, ambapo Mzee Nelson Mandela alikuwa upande wa General Paul Kagame, endapo itatokea vita kubwa kipindi hiki na kupelekea nchi kama Rwanda na Uganda kuhusika, basi Afrika Kusini itahusika moja kwa moja. Watapewa kandarasi za kijeshi na serikali ya Congo, kuanzia kuuza silaha na kutoa mafunzo ya kijeshi, jambo ambalo nadhani hakuna taifa la Afrika linawashinda Afrika Kusini. Itakuwa ni biashara kubwa yenye faida nyingi mno kwa makampuni ya silaha ya Afrika Kusini.

Zaidi ya hayo, Congo inaweza kufanya kama ilivyofanya kwa Zimbabwe baada ya majeshi yake kuiokoa serikali ya Raisi Laurent Kabila. Zimbabwe walipewa Mineral Concessions (Mikataba ya madini) yenye thamani ya trilioni nyingi. Ukisoma The UN Mapping Report iliyoandaliwa na Marehemu Dr Koffi Anan, serikali ya Zimbabwe ililipwa na Congo madini yenye thamani ya USD 5 Billion, ambazo ni sawa na TSZ 11 Trillion. Sasa kipindi hiki cha Ramaphosa, Afrika Kusini watapewa madili makubwa mno.

JAMBO LA KUJIULIZA:
General Kagame anataka nini haswa nchini Congo ilhali watusi hawako Congo peke yake. Tanzania, Uganda na Burundi zote zina watutsi, lakini kwanini hataki kujishughulisha nao ? Kama ni kupigania haki za watutsi, hivi akimaliza Congo, nini kitamzuia kupigania haki za watutsi nchini Burundi, Uganda au Tanzania? Hii ni michezo ya hatari mno ambayo endapo watutsi hawatakubali kubadilika inaweza ikaja kuwaumiza vibaya hata wao huko mbeleni.

Jambo la mwisho, hata kama General Kagame na Raisi Museveni wanaungwa mkono na mataifa kama Marekani, Uingereza na Israel katika kuivuruga Congo, hiki kipindi ni kibaya mno kwao kutaka kuanzisha vita kubwa kama ile ya 1998. Nyakati zimebadilika mno kwa Afrika, zile nguvu alizokuwa nazo Marekani na Uingereza za kupindua serikali za Afrika kirahisi tu bila madhara ya vita za muda mrefu hazipo tena. Hebu angalia kule Niger, Mali, Burkina-Faso, Libya na Sudan, ambako mpaka sasa kuna vita kubwa zinapiganwa.

Makundi hatari ya Kijeshi, Private Military Contractors (PMCs), kutoka Urusi, Israel na Marekani yanafanya kazi mbaya mno hapa Afrika yakitanua ushawishi. Watu kama Raisi Kagame na Museveni hawatanufaika kwa chochote kwa kuanzisha vita kubwa kipindi hiki. Hebu zingatia hizi sababu:

Mosi, kwasababu vita vitayahusisha mataifa makukwa duniani na vitakuwa virefu kiasi cha kuvuruga uchumi wa Rwanda, hata kupelekea machafuko ya kisiasa. Angalia kule Sudan, walianza na Al Bashir ila mpaka sasa Urusi, UAE, Saudi Arabia na Iran wanapambana vibaya mno na kuigeuza nchi shamba la bibi. Sidhani kama Rwanda au Uganda, hata kama wanaungwa mkono na Marekani wanaweza kupambana na magenge ya wahuni kama WEGNER GROUP bila kupata madhara.

Pili, kipindi hiki cha utandawazi huwezi kuficha chochote kinachoendelea. Isreal na nguvu yake kubwa ya PROPAGANDA, paka kufika February 2024, ameshashindwa kabisa vita ya PROPAGANDA dhidi ya Hamas. Kule TikTok, #FreePalestine ilikuwa na Views 5 billion, huku #IstandwithIsrael ikiwa na Views 125 million. Jambo lolote litakaloendelea Congo haliwezi kufichwa kama ilivyokuwa mwaka 1998-2003.

Tatu, Afrika Kusini, baada ya International Court of Justice (ICJ) Stunt ya kufungua kesi dhidi ya Israel kuwatetea wapalestina, jambo ambalo mataifa mengi yalikuwa yanaogopa na hadi kudhani haliwezekani, wamejijenga mno kidiplomasia hasahasa kwa wafuasi wa siasa za mlengo wa kushoto, ambao wengi ni mataifa ya barani ASIA na AMERIKA KUSINI. Hivyo endapo itatokea vita, sidhani kama Rwanda, Uganda na M23 wataweza kabisa kuishinda nguvu ya KIDIPLOMASIA ya Afrika Kusini, taifa ambalo liko BRICS na G20.

Bahati mbaya sana, Tanzania siku hizi inatawaliwa na wahuni. Tofauti na mwaka 1998 ambapo tulikuwa wasuluhishi wa ugomvi wa Congo, kipindi hiki watawala wanatamani kuchuma yaliyomo Congo kama ambavyo wengine wanachuma. Hivyo ikitokea vita kwamba Rwanda na Uganda wanavamia Congo, basi ni dhahiri kabisa KIDIPLOMASIA itakuwa mbaya kwake kwasababu mataifa mengi ya SADC watavurugana naye sana. Zile Military Escapades za Mozambique hazitawasaidia.

Sidhani kama litakuwa jambo la afya kwa nchi kama Rwanda, kutengwa KIDIPLOMASIA na mataifa ya SADC, huku taifa kubwa na lenye ushawishi kama Afrika Kusini likiwa linapiga Propaganda dhidi yako. Rwanda atafurukuta weeh, lakini sidhani kama atafika mbali na vita sizizo na msingi.

Nne, Rwanda ina udhaifu mmoja mkubwa, IT HAS NO POWERFUL AIRFORCE, kitu ambacho kiliwafanywa wapigwe vibaya mno na Zimbabwe mwaka 1998. Hata mwaka 2013, vikosi vya MUNISCO Intervention Brigade viliwashinda M23 waliokuwa wanasaidiwa na Rwanda kwasababu ya Attack Helicopters za Afrika Kusini. Huu udhaifu sidhani kama Rwanda ameurekebisha, ila endapo watasema hii vita iwe kubwa sidhani kama hawatakutwa na madhara.

NAMALIZIA:
Vinchi vya ukanda wetu ni masikini kwelikweli, badala ya kufikiri ni jinsi gani tunaweza kuishi kwa kuvumuliana vimeamua kutunisha msuli. Sidhani kama huu mwisho utakuwa mzuri. Hapa, Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi, tunachezeshwa ngoma nzito na Afrika Kusini akiwa na washirika wake bila kujua. Amini nakwambia, taifa kama Afrika Kusini ambalo liko BRICS na G20 haliwezi kuja mpaka Congo kwasababu za kibanadamu bali kimaslahi na kidiplomasia.

Hivyo mpaka akawepo hapa, lazima amezungumza na washirika wake wakubwa wa kiuchumi na kuwahakikishia kwamba uwepo wake hapa hauwezi kuleta madhara, zaidi zaidi faida kwao. Sisi watanzania, wanyarwanda na wakongo, we're just pawns in a very long game.​
Salute, Mkuu Malcom Lumumba long time
 
Kuna sababu......na sababu ni ukabila......kati ya jamii za wakongo na jamii za kinyarwanda......Ukabila na ujinga ndio sababu
Siyo kweli nakukatalia hii inatengenezwa na utawala wa Congo ili kuwatafutia sababu ya kuwakataa wacongomani wanaozungumza kinyarwanda.
 
Sasa nani juha????
Wewe ambae umeadithiwa na kusoma vijarida na makala....au mimi ambae mwaka 1998 nilikua Kisangani natafuta maisha kwa kununua dhahabu za magendo......na ninasaidia kutoa maiti barabarani za wanajeshi wa pande zote mbili na za raia.......baada ya kutelekezwa na kila upande......wakati huo 1998. wewe upo primary au secondary?????
Wewe ni bure kabisa, story zako zoote ni za uzushi mtupu, umeng'ang'ania eti ulikuwa mnunuzi wa dhahabu duuu! Mfanyabiashara ya dhahabu ndani ya JF, hio ndio umeona mbinu ya kudanganya watu kwamba unaifahamu Congo, bure kabisa. Hayo majarida na magazeti unayo yatajataja ndio yapi hayo? mimi siyajui, isijekuwa ndio source zako maana story imekuwa moja tuu, eti natafuta maisha kwa kununua dhahabu. Kwenye battle field na biashara ya dhahabu wapi na wapi. Kijana sina muda wa kubishana na wewe tena ila kwa taarifa yako hapa unaongea na veterani wa operetion Kitona alietua na ndege ya pili. Japo nimekwisha staafu lakini nafahamu mengi kuhusu huu mgogoro, nafuatilia kwa karibu sana na nina vyanzo vya habari kutoka kwa wahusika wenyewe waliopo front line. Right now kuna mambo mengi sana mnafichwa kwani ni siri za kijeshi, especially habari zinazo husiana na hivi vikosi vyote vinavyopigana huko iwe ni M23, Wagner, Burundi, Wazalendo, Fardc,Fdlr,Sa,Tz,Ml I have more information and accurate ones about what is going on in congo, kwa bahati mbaya sana humu jf watu wengi ni mashabiki tuu, na watu wa ma sentiment, Hatufanyi hata simple analysis.
 
Maelezo.....meengi.......umeyatoa kwenye majarida na makala.......yawezekana 1997 mpaka 1999 ulikua primary school!!!!
Sasa sisi tuliokuwepo tunanunua kimagendo dhahabu kwa wanajeshi wa UPDF na RDF na Banyamulenge mjini Kisangani 1998 tusemeje????
Sisi tuliokua nyuma ya wanyarwanda na waganda na waasi wa kikongomani wakati wanajaribu kuisogelea kwa mara ya pili kinshasa 1998 baada ya kugombana na kabila tusemeje????
TATIZO LENU MADOGO WA JF MNAONGELEA ZAIRE ILA HAMJAWAHI KUISHI HUKO ZAIDI YA KUADITHIWA.......NA KUSOMA MAGAZETINI!!!
SISI TUMESHUHUDIA VITA KWA MACHO KUANZIA GOMA,UVIRA,BUKAVU,KISANGANI MPAKA MITAA YA KINSHASA.
Eti "Madogo wa JF" nani dogo hapa? humu JF umeingia hujakaa hata miezi 13 lakini una post karibu 9k hivi hauna kazi nyingine? Halafu unajiita mfanyabiashara wa dhahabu duuuu, sasa dogo ni nani kati ya mtu alie ingia humu mwaka jana na mtu yuko humu kwa zaidi ya miaka 10, Au una multiple ID's kijana. Bahati mbaya siwezi kupata muda wa kutosha kutokana na kazi zangu za kilasiku hapa Bukavu ningekupatia news zenyewe for free na kukuonyesha jinsi ulivyo short informed bwana Kagame.
 
Wewe ni bure kabisa, story zako zoote ni za uzushi mtupu, umeng'ang'ania eti ulikuwa mnunuzi wa dhahabu duuu! Mfanyabiashara ya dhahabu ndani ya JF, hio ndio umeona mbinu ya kudanganya watu kwamba unaifahamu Congo, bure kabisa. Hayo majarida na magazeti unayo yatajataja ndio yapi hayo? mimi siyajui, isijekuwa ndio source zako maana story imekuwa moja tuu, eti natafuta maisha kwa kununua dhahabu. Kwenye battle field na biashara ya dhahabu wapi na wapi. Kijana sina muda wa kubishana na wewe tena ila kwa taarifa yako hapa unaongea na veterani wa operetion Kitona alietua na ndege ya pili. Japo nimekwisha staafu lakini nafahamu mengi kuhusu huu mgogoro, nafuatilia kwa karibu sana na nina vyanzo vya habari kutoka kwa wahusika wenyewe waliopo front line. Right now kuna mambo mengi sana mnafichwa kwani ni siri za kijeshi, especially habari zinazo husiana na hivi vikosi vyote vinavyopigana huko iwe ni M23, Wagner, Burundi, Wazalendo, Fardc,Fdlr,Sa,Tz,Ml I have more information and accurate ones about what is going on in congo, kwa bahati mbaya sana humu jf watu wengi ni mashabiki tuu, na watu wa ma sentiment, Hatufanyi hata simple analysis.
Dogo......hata zaire hupajui.....kelele nyingi........mwaks 1998 mpaka 2003 ww si ulikua unadeka deka kwa wazee wako huko Tanzania 🤣🤣🤣
 
Eti "Madogo wa JF" nani dogo hapa? humu JF umeingia hujakaa hata miezi 13 lakini una post karibu 9k hivi hauna kazi nyingine? Halafu unajiita mfanyabiashara wa dhahabu duuuu, sasa dogo ni nani kati ya mtu alie ingia humu mwaka jana na mtu yuko humu kwa zaidi ya miaka 10, Au una multiple ID's kijana. Bahati mbaya siwezi kupata muda wa kutosha kutokana na kazi zangu za kilasiku hapa Bukavu ningekupatia news zenyewe for free na kukuonyesha jinsi ulivyo short informed bwana Kagame.
Sasa dogo ww kukaa JF jukwaa la kuhabarishana miaka kumi ndio kuijua dunia........Kaka zako tumeanza kuijua dunia hata simu za mkononi hatuna......!!!Sisi tupo North Kivu na South Kivu since 1992.....utatuambia nn wandewa kuhusu Zaire"
Kama huijui Zaire yetu kaa kimya.....,..
 
Siyo kweli nakukatalia hii inatengenezwa na utawala wa Congo ili kuwatafutia sababu ya kuwakataa wacongomani wanaozungumza kinyarwanda.
HATA KABLA YA WAKOLONI KUJA MAKABILA YOTE YA KONGO NA UKANDA WA MAZIWA MAKUU YALIKUA YANABAGUANA NA MPAKA KESHO WANABAGUANA............KWANI WANYARWANDA WAMEANZA KUKAA MAENEO YA KIVU JANA AU LEO????
WAMEKAA PALE MIAKA ZAIDI YA 1500.
WANABAGULIWA SABABU HATA WAO WANAWABAGUA MAKABILA MENGINE
HUO UTAWALA UNAOUSEMA ULIANZA 1959.....1960...!!
KABLA YA HAPO WALIKUEPO WABELGIJI......NA KABLA YA WABELGIJI WALIKUEPO WAARABU WA TABORA NA UJIJI AKINA RUMALISA NA AKINA SEIF NA AKINA TIP TIP NA WENGINE WENGIII......NA WOOTE HAO WALICHOCHEA ZAIDI TABIA YA MAKABILA YA MASHARIKI MWA CONGO KUBAGUANA.
 
Hakuna sababu. Nikuulize swali hivi wamasai wa kwenya na wamasai wa Tanzania inawezekanaje nchi moja ikatae na kusema siyo raia? Kwa sababu ya mipaka ya nchi? Nani alichagua kuwa mmasai wa Kenya na nani alichagua kuwa masai wa Tanzania?
UBAGUZI HAUNA SABABU...BALI UBAGUZI NI UGONJWA WA AKILI.....NA SABABU KUBWA WATAKUAMBIA KUA....TUNAONGEA LUGHA TOFAUTI BADI WACHA TUBAGUANE............KULE MASHARIKI MWA KONGO KARIBIA MAKABILA YOOTE YANABAGUANA.
 
Dah Rwanda inachukiwa sana.... Nadhani sababu ni raisi wake!!!
Ifike point uongozi uache kuwaponza raia wake,
USHUHUDA:
niliwahi msikia mama wa rafiki yangu akimpa ushauri mwanae wa kiume kwamba "kwenye maisha yako usijeoa mtusi"
nilivunga sijasikia lakini ile kitu huwa inanisumbua Sana mpk leo........ Viongozi wasituchonganishe jaman, ifike point mambo yao wasihusishwe raia wasio na hatia
Unajua wanyarwanda hasa watusi ni watu wanaojali sana uasili wao hivyo Kwa jamii nyingine inawaona kama Wana ubaguzi but sio wote ubaguzi uko kila Mahali nimekaa na watu wengi Toka Rwanda nimewafundisha na wengine ni marafiki zangu hadi sasa hivyo nawaelewa Hawa ndugu zetu.
 
Bro tofauti nyingine hii hapa........sisi wabantu mtu akikuchukia utajua siku hyohyo au siku chache za usoni(kwahy ukishajua utaona n namna vipi mmalize tofauti zenu au umuepuke maisha yaendelee)...... Ila Hawa wenzetu unaweza kaa nae 2 yrs anakuchekea kumbe unataftiwa timing uuwawe!!!
Ndo maana watu wanawaogopa, mtu ambaye akichukia haoneshi n bora ukaish na Simba ndani!!!
Maana akiamua kukuua n asubuhi tu majirani tunakunywa uji

Huku kwaya kwa saut ya chini zinaendelea kuimba polepole🚶🚶
 
Hawa madogo wa vyuo wanajifanya wajuaji...,......mm 1998 umri wangu ni kijana mdogo ila nipo kisangani natafuta ugali.......ipo siku nitaadithia kwenye nyuzi zangu mkuu.
mkuu wasamehe bure wadogo zako nadhani wamejuta kujidai wajuaji kumbe wanasoma vijarida [emoji16][emoji16][emoji28][emoji23]
 
Mambo mengi.......nipo Kivu kusini right now.....huku kumewaka sio kitoto
Ahaaa kama upo South Kivu, hebu fika pale Kavumu, Utakuta vifaa vya kijeshi vya SADC Vimerundikana, unajua vimetoka wapi? hivi ndio vilikuwa pale Goma. Sasa sijui ndio re-Org, au ndio tactical withdraw kama wanavyo sema wenyewe😀😀😜. Daa mambo sio mchezo kimewaka moto na hata vikosi vya SADC havionekani tena ndani ya Goma, ule mkwala walioingia nao sijui umekwenda wapi maana tangia wafike hawajaweza kuwarudisha hawa M23 hata km chache tu, sana sana ni kuchanja mbuga kila wanapo kutana na hawa vijana wa Gen. Sultan MAKENGA.
 
Ahaaa kama upo South Kivu, hebu fika pale Kavumu, Utakuta vifaa vya kijeshi vya SADC Vimerundikana, unajua vimetoka wapi? hivi ndio vilikuwa pale Goma. Sasa sijui ndio re-Org, au ndio tactical withdraw kama wanavyo sema wenyewe😀😀[emoji12]. Daa mambo sio mchezo kimewaka moto na hata vikosi vya SADC havionekani tena ndani ya Goma, ule mkwala walioingia nao sijui umekwenda wapi maana tangia wafike hawajaweza kuwarudisha hawa M23 hata km chache tu, sana sana ni kuchanja mbuga kila wanapo kutana na hawa vijana wa Gen. Sultan MAKENGA.
Hii ndi ndoto. Tangu 2000 hadi leo RDF RPA, RDC CNDP na matawi yake yote hawajawahi kuwa na upper hand mbele ya SADC.

Kuna msema kuwa kamanda wenye akili hushinda vita bila kupogana. Hadi sasa M23 na shina lake RDF wamepoteza vita ya diplomasia hii ni hatua ya kwanza katika kushindwa vita ya ardhini.

Sasa wamebaki kuteka vijiji na mapori. Naona SADC na FARDC haziwafuati huko nadhani ni strategy ya kurefusha supply line ya RDF angalau ifike KM 200 na ukiikata unapata kuteka ama kuuwa RDF-M23 kama 2000 mbili hivi. Hapo wataelewa nani kaka.

Sent from my A002SH using JamiiForums mobile app
 
Utamaliza utamu japo umeandika kwa hisia ila hisia zako zitaharibu utamu.
 
Hii ndi ndoto. Tangu 2000 hadi leo RDF RPA, RDC CNDP na matawi yake yote hawajawahi kuwa na upper hand mbele ya SADC.

Kuna msema kuwa kamanda wenye akili hushinda vita bila kupogana. Hadi sasa M23 na shina lake RDF wamepoteza vita ya diplomasia hii ni hatua ya kwanza katika kushindwa vita ya ardhini.

Sasa wamebaki kuteka vijiji na mapori. Naona SADC na FARDC haziwafuati huko nadhani ni strategy ya kurefusha supply line ya RDF angalau ifike KM 200 na ukiikata unapata kuteka ama kuuwa RDF-M23 kama 2000 mbili hivi. Hapo wataelewa nani kaka.

Sent from my A002SH using JamiiForums mobile app
Lakini hebu jiulize, SADC wako wapi? Mbona kimyaaa? Fuatilia kwa makini mambo sio mazuri. Sasa hivi ni Diplomasia inafanya kazi kwani mbu katua kwenye korodani.
 
Back
Top Bottom