McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa, amemtaka Dkt. Mwigulu Nchemba kuacha kupotosha umma kuhusu madai ya msingi ya wananchi juu ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Amesema madai hayo hayakuibuka ndani ya miezi mitatu kuelekea uchaguzi mkuu, bali yalianza muda mrefu uliopita.
Golugwa alisisitiza kuwa Tanzania haiwezi kujengwa juu ya uongo na kufunika ukweli wa maafa yaliyotokea. Alionya kuwa amani inayotokana na vitisho siyo amani ya kweli, na ukimya unaotokana na hofu si utulivu. “Hakuna amani bila haki, hakuna haki bila uwazi, na hakuna uwazi bila kusema ukweli wote,” alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 27, 2025, Golugwa alihimiza taifa kuungana na serikali kuepuka sura ya unafiki, akisisitiza umuhimu wa uwazi na haki katika kujenga amani ya kudumu.