Ebwana lile dude la uncle waffles linaitwa Tanzania..last week nilikuwa pale longstreet capetown mtaa wa mapopo hilo dude lilinikosha kwakweli tena msauz kaisifia nchi yangu,, from beerhouse to bobs bar to souk to coco yaani clubs kibao lilikuwa ni hilo dude tu. Ukweli ni kwamba amapiano OG ya sauz ni muziki unaotengenezwa na sound engineers most of producers and DJs in south africa ni sound engineers. Amapiano bongo ni makelele tu ya s2kz hayawezi kupigwa hata MTV maana mixing ni uchafu na nyie mnaokesha kidimbwi chungeni sana maskio yanu maana mnasikiliza uchafu nyimbo hazina quality ni kelele uzeeni mtakuwa viziwi muanze kusumbua. Ushauri wangu tusiige wenzetu hawafanyi amapiano kutafuta jina wasauz muziki ni part ya maisha yao kila kona ukipita utakuta kwaya zinaperfom mitaani au vijana wanatumbuiza mitaani kila kona utakuta watumbuizaji wenye vipaji mitaani tu sasa bongo watu wanatafuta kiki tu.