Amesema wadada wanakubali utoaji mimba ndio sababu kubwa ya kuharibika kwa mimba! Wewe unatafsiri vp kauli yake? Amekataa kusema moja kwa moja ni indirect statement, kwahiyo alichokuwa anachokizungumzia muathirika ni uongo kwa maana nyingine! Mnataka atoe sababu ambayo ipo kwenye vichwa vyenu.
Nitoke kwenda wapi Matola, point yangu ni kwamba kwa nini hawakuzungumzia madhara ya utoaji mimba kwenye kizazi mwanzo mpaka mwisho wa kipindi? au kuuliza hivyo ni kusema kwa nini hakusema alitoa mimba huko nyuma? Ni nimeuliza kama ni bahati mbaya au makusudi? au wewe hujui kama hiyo ni moja ya sababu kubwa sana?
so unataka tuache kuhoji ili dada zetu waendelee kutoa mimba huku monitor development za huo ugonjwa?
Tatizo Hilo Lina complications nyingi sana mkuu, hizo sababu zote alizotoa zinasabishwa na Hilo tatizo, Hebu jisomee mwenyewe mkuu, unakataa hukusema alitoa mimba ila indirectly umetoa sababu kwamba utoaji mimba ni moja ya sababu kubwa ya uharibifu wa mimba.
Mkuu, hao wadada hawakuelezea hata kidogo swala la utoaji mimba, ndo swali langu, kwani kama najua alikuwa na historia ya kutoa mimba nini kinanifanya nishindwe kusema? alafu wapi nimesema amedanganya?
Kwann unalazimisha wazungumzie kitu kilichokuwa nje ya topic mkuu? Usiseme Kama unajua alikuwa anatoa mimba ni bora useme unajua alikuwa anatoa mimba! Kitu ambacho umekata hukusema lakini unalazimisha wakizungumzie!! Kuna sababu nyingi za kuharibika kwa mimba lakini hizo zote hazina uhusiano na tatizo lake, sasa unataka wakizungumzie kivipi?!
Ningesema utoaji mimba ndio sababu pekee ya kuharibika kwa kizazi ni sawa kunichukulia nimesema na yeye alitoa mimba, point yangu ni kwamba wadada wengi wenye matatizo ya uzazi kwa kiwango kikubwa matatizo hayo yamesababishwa na utoaji mimba.
Pale hawakuwa wakizungumzia tatizo lake, walikuwa wanazungumzia tatizo hilo kwa wanawake kwa ujumla, point yangu ni kwamba walilizungumzia kwa namna inayoweza kuaminisha watu kwamba ni tatizo kama lake pekee ndio linaweza kusababisha mwanamke asipate mtoto?
Kwa mfano, wakati alisema amekwisha pata mimba mara kadhaa na zikawa zinaharibika hakusema kwamba na hilo ni matokeo ya tatizo hilo.
Na pia, wakati alisema amefanya operations nyingi za kizazi, hakusema kama hizo operations zote zilikuwa ni jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo.
Lakini, wakati alisema ugonjwa huo ulijurikana baada ya hizo operations zote, hakusema huko nyuma walikuwa wanafanya operations kutatua sababu zipi?
Nimegundua tatizo lako lipo wapi mkuu, ulitaka kipindi kizungumzie kwa upana tatizo lake pamoja na matatizo mengine yanayosababisha kuharibika kwa mimba na hiyo inategemea na muendesha kipindi uwezo wake wa kuhoji/kuuliza maswali vinginevyo Mimi sioni tatizo kwa kujikita ktk tatizo Hilo linalomsumbua.
Inawezekana.
Lakini, katikati ya mjadala, baaada ya Mtangazaji kusema vidonge vya kuzuia vina madhara, na kumuuliza Happy kama haoni kwamba kuwaambia mabinti watumie vidonge hivyo wakati wakiwa nje ya ndoa kama ni kwenda kinyume cha mira na desturi zetu?
Happy alipotezea... zaidi akasisitiza kwamba, hakuna kitu ambacho hakina madhara, akaeleza kwamba hata condom zinamadhara, na akasisitiza kwamba vidonge vya kuzuia mimba vinapunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huo.
Sasa sijui mimba ndio zinasababisha pia au la? sababu ni kwanini vidonge vya kuzuia mimba viwe ni kinga?
Siwezi kuthibitisha Kama vidonge vya kuzuia mimba vinaweza kuzuia Hilo tatizo unless nifanye research ya kusoma zaidi ila kumbuka yeye ndiye muhanga wa hayo maradhi na ameshazunguka kwa wataalamu wengi kwahiyo kuna vitu vingi anajua ambavyo Mimi na wewe hatujui pengine na madaktari wengine hawajui wala haishangazi!
Kuna vitu vingine muendeshaji wa kipindi lazima atumie akili sio kila kitu ni cha kuuliza tu! Utaacha kuelimisha watu matumizi ya vidonge vya uzazi na matumizi ya condom wakati unajua watu wanafanya ngono sana tu! Sasa unakuwa unasaidia jamii kivipi?
Madhara ya kutotumia condom na vidonge vya kuzuia mimba ni makubwa sana kwa jamii kila mtu anajua na hakuna ubishi anachosema hakuna kitu kisichokuwa hakina madhara inategemea mtu na mtu, kuhoji au kuendesha kipindi inahitaji busara na hekima sana mkuu.
unamaanisha nini?
Kuhusu busara.
Una maanisha nn kwamba the so called "shangazi Cecilia" alikua akimuuza HM? Just open up! Ama alikua shangingi kurumbembe like Dida wa Mchops? Is it?
Mkuu shangazi yangu ni shost yake H.M anaitwa Cecilia jina la nyumbani lakini ana jina lake la shule, sikutajii ng'o kwani wengi marafiki zake shangazi yangu hawamjui kama anaitwa Cecilia. Sitakutafunia kila kitu mkuu, H.M huwa anawaasa mabinti wanaopenda short cut.
Unataka kusema yeye alikuwa anapenda short cut mkuu? Au ni dhambi kuwaasa mabinti wanaopenda short cut? Maana baadhi Yao ni tabia zao.