Ambao hatujawahi kuchanjwa chale wala kwenda kwa waganga licha ya kuishi kwenye mazingira yenye uchawi sana tukutane hapa

Rafiki yangu Mhindi anavaa madini ya kila namna eti nayo ni kinga
 
Wahindi kwa shirk wanaongoza mkuu
Na wanaamini haswa

Nakumbuka mabasi ya yakiingia wanachukua ule udongo wa kwenye matairi ( utotoni tumelamba sana) na kuingia nao ndani huku wakivunja mayai
Wewe pia ulikua unawanga nao

Ukitaka kumjua mmoja wao Juana na mmoja wao, wewe pia ni mmoja wao
 
Yaani uchanjwe damu zichoruzike harafu dawa iingie si Bora kama kumeza!Sasa damu inamwagika hiyo dawa inaingiaje?
 
Yaani uchanjwe damu zichoruzike harafu dawa iingie si Bora kama kumeza!Sasa damu inamwagika hiyo dawa inaingiaje?
Umepigwa NDUI wewe wakati unapigwa NDUI damu ilitoka au haikutoka dawa ilikuiingia au haikuingia?

Angalia mkono wako wa kushoto begani una chale ya NDUI ulipozaliwa tu wakakuwahi fasta ukapigwa chale
 
Chale na dawa ya ndui vitu 2tofauti!
Kwa sababu ni vya MZUNGU au sio?

Wazungu walishafanya Plagiarism ya Mambo mengi kutoka kwetu sisi wa Afrika Ila sisi wengi ni mazuzu tunaacha vya kwetu tunafuata vya wenzetu bila kujua nini ni nini na kipi ni kipi na kuvidharau vya kwetu mwisho wao wanachukua na kuhamishia kwao nyinyi mnabaki mikono mitupu

Ntakupa mfano mdogo wazungu walipokosa creativity wali-copy nyimbo ya asili ya Manu Dibango kutoka Cameroon wimbo unaitwa 'Soul Makossa' huu wimbo aliimba MJ unaitwa 'Mamase Mamasi Mamakussa'

Makossa maana yake 'dance' mpaka leo kampuni zote zilizoshiriki ku-copy hio creativity ya Mwafrika inalipa milabaha kwa Manu Dibango

Usidharau vya kwenu wazungu wasikupotoshe ukaona cha mzungu ni cha maana Ila cha Mwafrika ni chaa kupuuzwa wenyewe wanacopy kutoka kwetu hata hio NDUI wamecopy kutoka chale wakaipeleka kwenye ustaarabu wa SINDANO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…