Ambao hatujawahi kuchanjwa chale wala kwenda kwa waganga licha ya kuishi kwenye mazingira yenye uchawi sana tukutane hapa

Ambao hatujawahi kuchanjwa chale wala kwenda kwa waganga licha ya kuishi kwenye mazingira yenye uchawi sana tukutane hapa

Asante mkuu maana kuna watu wanaamini hii kitu kuwa kila mmoja ameenda kwa mganga

Sisi home mambo haya wazee na kina bibi na kina mama wamekataa kabisa
Hakuna kuamini ujinga huu bali tunaamini kinga ya Mungu tu

Tunamuoamini Mungu na kila jambo likitokea liwe zuri au baya tunamshukuru

Haya wenye kinga ya uchawi hawaibiwi? Hawafiwi? Hawapati ajali?

Kwa hiyo mna maisha mazuri kwa kwa ajili ya chale?

Tulikuwa tunamjaribu mzee kwa kumuambia huyu ni mchawi yaani atakula fimbo mpaka basi
Rafiki yangu Mhindi anavaa madini ya kila namna eti nayo ni kinga
 
Wahindi kwa shirk wanaongoza mkuu
Na wanaamini haswa

Nakumbuka mabasi ya yakiingia wanachukua ule udongo wa kwenye matairi ( utotoni tumelamba sana) na kuingia nao ndani huku wakivunja mayai
Wewe pia ulikua unawanga nao

Ukitaka kumjua mmoja wao Juana na mmoja wao, wewe pia ni mmoja wao
 
Swalama Wananzengo.
Kila mtu anazaliwa na kinga yake ya kimwili na ya kiroho.

Kinga nyingine tunaziongezea baada ya kuzaliwa kama kinga ya magonjwa ya surua, polio, kifua kikuu, dondakoo nk

Wengine sasa huenda mbali zaidi kwa kuongeza kinga za kiroho kwa kuchanjwa chale na waganga, kumezeshwa mafuta ya Mwamposa ili mtoto asidhurike (huu nao ni uganga new model).

Pia kuna sisi ambao tumekaa sehemu ngumu, kwenye urozi wa kila aina na wa kila rangi lakini hatukuyumbishwa.

Nimekaa sehemu zenye Wanyamanyafu, nimekaa kwa kina Ibambanghulu, mtu anatuna ndani ya nyumba anajaa nyumba nzima.

Sikufanya chochote juu ya mwili wangu na roho yangu.

Sisi ndio watu wabishi ambao hatusomeki kwenye rada za kina Mshana Jr
Yaani uchanjwe damu zichoruzike harafu dawa iingie si Bora kama kumeza!Sasa damu inamwagika hiyo dawa inaingiaje?
 
Yaani uchanjwe damu zichoruzike harafu dawa iingie si Bora kama kumeza!Sasa damu inamwagika hiyo dawa inaingiaje?
Umepigwa NDUI wewe wakati unapigwa NDUI damu ilitoka au haikutoka dawa ilikuiingia au haikuingia?

Angalia mkono wako wa kushoto begani una chale ya NDUI ulipozaliwa tu wakakuwahi fasta ukapigwa chale
 
Chale na dawa ya ndui vitu 2tofauti!
Kwa sababu ni vya MZUNGU au sio?

Wazungu walishafanya Plagiarism ya Mambo mengi kutoka kwetu sisi wa Afrika Ila sisi wengi ni mazuzu tunaacha vya kwetu tunafuata vya wenzetu bila kujua nini ni nini na kipi ni kipi na kuvidharau vya kwetu mwisho wao wanachukua na kuhamishia kwao nyinyi mnabaki mikono mitupu

Ntakupa mfano mdogo wazungu walipokosa creativity wali-copy nyimbo ya asili ya Manu Dibango kutoka Cameroon wimbo unaitwa 'Soul Makossa' huu wimbo aliimba MJ unaitwa 'Mamase Mamasi Mamakussa'

Makossa maana yake 'dance' mpaka leo kampuni zote zilizoshiriki ku-copy hio creativity ya Mwafrika inalipa milabaha kwa Manu Dibango

Usidharau vya kwenu wazungu wasikupotoshe ukaona cha mzungu ni cha maana Ila cha Mwafrika ni chaa kupuuzwa wenyewe wanacopy kutoka kwetu hata hio NDUI wamecopy kutoka chale wakaipeleka kwenye ustaarabu wa SINDANO
 
Back
Top Bottom