Ambao hatujawahi kuchanjwa chale wala kwenda kwa waganga licha ya kuishi kwenye mazingira yenye uchawi sana tukutane hapa

Ambao hatujawahi kuchanjwa chale wala kwenda kwa waganga licha ya kuishi kwenye mazingira yenye uchawi sana tukutane hapa

Swalama Wananzengo.
Kila mtu anazaliwa na kinga yake ya kimwili na ya kiroho.

Kinga nyingine tunaziongezea baada ya kuzaliwa kama kinga ya magonjwa ya surua, polio, kifua kikuu, dondakoo nk

Wengine sasa huenda mbali zaidi kwa kuongeza kinga za kiroho kwa kuchanjwa chale na waganga, kumezeshwa mafuta ya Mwamposa ili mtoto asidhurike (huu nao ni uganga new model).

Pia kuna sisi ambao tumekaa sehemu ngumu, kwenye urozi wa kila aina na wa kila rangi lakini hatukuyumbishwa.

Nimekaa sehemu zenye Wanyamanyafu, nimekaa kwa kina Ibambanghulu, mtu anatuna ndani ya nyumba anajaa nyumba nzima.

Sikufanya chochote juu ya mwili wangu na roho yangu.

Sisi ndio watu wabishi ambao hatusomeki kwenye rada za kina Mshana Jr
Sisi ndio watu wabishi ambao hatusomeki kwenye rada za kina Mshana Jr[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swalama Wananzengo.
Kila mtu anazaliwa na kinga yake ya kimwili na ya kiroho.

Kinga nyingine tunaziongezea baada ya kuzaliwa kama kinga ya magonjwa ya surua, polio, kifua kikuu, dondakoo nk

Wengine sasa huenda mbali zaidi kwa kuongeza kinga za kiroho kwa kuchanjwa chale na waganga, kumezeshwa mafuta ya Mwamposa ili mtoto asidhurike (huu nao ni uganga new model).

Pia kuna sisi ambao tumekaa sehemu ngumu, kwenye urozi wa kila aina na wa kila rangi lakini hatukuyumbishwa.

Nimekaa sehemu zenye Wanyamanyafu, nimekaa kwa kina Ibambanghulu, mtu anatuna ndani ya nyumba anajaa nyumba nzima.

Sikufanya chochote juu ya mwili wangu na roho yangu.

Sisi ndio watu wabishi ambao hatusomeki kwenye rada za kina Mshana Jr

Moja ya mambo ambayo ninawashukuru wazazi na walezi wangu ni pamoja na hili la kuulinda mwili wangu na kunikabidhi ukiwa hauna Alama za chale. Naendeleza walipoishia.
 
Kwa sababu ni vya MZUNGU au sio?

Wazungu walishafanya Plagiarism ya Mambo mengi kutoka kwetu sisi wa Afrika Ila sisi wengi ni mazuzu tunaacha vya kwetu tunafuata vya wenzetu bila kujua nini ni nini na kipi ni kipi na kuvidharau vya kwetu mwisho wao wanachukua na kuhamishia kwao nyinyi mnabaki mikono mitupu

Ntakupa mfano mdogo wazungu walipokosa creativity wali-copy nyimbo ya asili ya Manu Dibango kutoka Cameroon wimbo unaitwa 'Soul Makossa' huu wimbo aliimba MJ unaitwa 'Mamase Mamasi Mamakussa'

Makossa maana yake 'dance' mpaka leo kampuni zote zilizoshiriki ku-copy hio creativity ya Mwafrika inalipa milabaha kwa Manu Dibango

Usidharau vya kwenu wazungu wasikupotoshe ukaona cha mzungu ni cha maana Ila cha Mwafrika ni chaa kupuuzwa wenyewe wanacopy kutoka kwetu hata hio NDUI wamecopy kutoka chale wakaipeleka kwenye ustaarabu wa SINDANO
Ndui dawa inaingia kwenye mishipa,chanjo ni nje ya mwili na damu inatoka ,we hiyo Bado ni ya wazungu?!!
 
Swalama Wananzengo.
Kila mtu anazaliwa na kinga yake ya kimwili na ya kiroho.

Kinga nyingine tunaziongezea baada ya kuzaliwa kama kinga ya magonjwa ya surua, polio, kifua kikuu, dondakoo nk

Wengine sasa huenda mbali zaidi kwa kuongeza kinga za kiroho kwa kuchanjwa chale na waganga, kumezeshwa mafuta ya Mwamposa ili mtoto asidhurike (huu nao ni uganga new model).

Pia kuna sisi ambao tumekaa sehemu ngumu, kwenye urozi wa kila aina na wa kila rangi lakini hatukuyumbishwa.

Nimekaa sehemu zenye Wanyamanyafu, nimekaa kwa kina Ibambanghulu, mtu anatuna ndani ya nyumba anajaa nyumba nzima.

Sikufanya chochote juu ya mwili wangu na roho yangu.

Sisi ndio watu wabishi ambao hatusomeki kwenye rada za kina Mshana Jr
Umekagua vizuri mkuu huenda ukichanjwa usiku na wachawi au utotoni

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Chanjo ya mzungu sio Ushiriki ila kinga asili kutoka kwa babu zako ndo ushirikina.

Change your mindset
 
Asante mkuu maana kuna watu wanaamini hii kitu kuwa kila mmoja ameenda kwa mganga

Sisi home mambo haya wazee na kina bibi na kina mama wamekataa kabisa
Hakuna kuamini ujinga huu bali tunaamini kinga ya Mungu tu

Tunamuoamini Mungu na kila jambo likitokea liwe zuri au baya tunamshukuru

Haya wenye kinga ya uchawi hawaibiwi? Hawafiwi? Hawapati ajali?

Kwa hiyo mna maisha mazuri kwa kwa ajili ya chale?

Tulikuwa tunamjaribu mzee kwa kumuambia huyu ni mchawi yaani atakula fimbo mpaka basi
Mnafanana kabisa na familua yetu aiseee.
 
Chanjo ya mzungu sio Ushiriki ila kinga asili kutoka kwa babu zako ndo ushirikina.

Change your mindset
Chanjo ya mzungu ina-mechanisms na formula ambayo inaeleweka na kufahamika duniani kote, ambayo hata wewe mwenyewe unaweza kuifanya na ikakuletea matokeo yaleyale.

Izo chale zenu za mababu ambazo anajua babu tuu na hataki mwingine ajue ndio ushirikina wenyewe
 
Sawa

Sasa kama hizo chanjo zina formula kil mtu anaweza why tushindwe kupata Chanjo ya magonjwa kama hep b, TB nk mpaka tusubir kuletwa na wazungu?.
 
Usipokuwa na kinga mwanga hakuoni, Sasa hapo kama ni mgeni anajua wewe una Kinga kali kumzidi na umeificha... Ndio maana rada inanasa taharifa ya kitu ambacho Ina informations zake Kwa jinsi ilivyokuwa instructed.
Mwanga akikuditect una Kinga atataka Mpimane, ukimshinda anaenda kuwapa taharifa wenzake, nao wakikushindwa inatumwa taharifa ngazi ya Kijiji, kata nk
 
Duh kweli mkuu umeona mengi yani yani mtu anatuna ndani ya nyumban anajaa nyumban nzima[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
wamekufanya nn mkuu
Watu wangu wa karibu wanataka niangamie
wamekufanya nn mkuu
Aise mambo ni mengi. Chuki, kuchonganishana, wivu tena kutoka Kwa watu wa karibu. Kuna mtu wa karibu kabisa anatamani nife ili hali bado nipo kwenye nyumba za kupanga na watoto 4! Nikifikiria nilichofanya sikijui.

Niliwatendea wengi wema wananilipa majungu na masengenyo. Kabla sijaoa niliwekeza maisha yangu Kwa watu wengine. Nilivyooa majukumu yakawa mengi nikikwama kitu kidogo nasemwa mpaka basi. Kuna mwaka nilipata safari ya kwenda nje ya nchi kikazi kuna mtu niliyemtoa mbali aliumia sana. Pia wananisema vibaya ninavyoishi na watoto wangu wanne (wote wasichana). Yaani ili mradi tafrani. mambo yangu mengi yamevuruguka Kwa kukosa utulivu.
 
Acha kutudanganya, hebu angalia hapo kichwani karibu na utosi uone kama hamna chale tatu.

Mengine yalifanywa na wazazi wetu pasi kujua.

Mengine yamefanywa na wachawi tukiwa tumelala.
Kabisa hawaelewi dada mkubwa wazazi walisha maliza yao kitambo. Wao wanapiga kifua mbele na kujipongeza bila kujua yanafanywa alikuwa juu ya mgongo.😎
 
Usipokuwa na kinga mwanga hakuoni, Sasa hapo kama ni mgeni anajua wewe una Kinga kali kumzidi na umeificha... Ndio maana rada inanasa taharifa ya kitu ambacho Ina informations zake Kwa jinsi ilivyokuwa instructed.
Mwanga akikuditect una Kinga atataka Mpimane, ukimshinda anaenda kuwapa taharifa wenzake, nao wakikushindwa inatumwa taharifa ngazi ya Kijiji, kata nk
Hii inaweza ikawa kweli.. kuna maza mmoja wa kizaramo nilikuwa nakula sana matunda kwenye genge lake (anasifika kwa ndumba na yeye hakatai)..katika kupiga stori sijui ikawaje tukaanza kuongelea mambo haya.. akaniambia live hapa mtaani kwetu (kipindi nakaa kigogo) ni nyumbani kwetu na nyumba nyingine moja akaitaja ndio hamjafanyiwa mila yoyote (hatuna busta)... na mtaa wetu ulikuwa una watu wengi sana wanaoenda church.. nilikuwa namuuliza una ushahidi gani.. ananiambia tunajuana ingawa mimi ndio nasemwa sana kwasababu sifichi.
 
Back
Top Bottom