Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Marafiki wa shuleni?Kazini sina marafiki 😂😂 nikifika nafanya kazi zangu zikiisha hata kama ni saa nne naleft, nipo kwenye kikundi cha vicoba kazini lakini sipo interested na hao watu wana umbea uliopitiliza, nipo tu kwasababu nna faida nacho sana
Wewe hauogopi ?hivi kwa nini watu wanaogopa kuzikwa na manispaa?
Itabidi tuanzishe kakikundi chetu😃Evelyn, naa, demi, na mwingine.....umoja wa wasio na marafiki, thread ifungwe ☺️
Wala siogopi. Cha muhimu ni kuenjoy life ukiwa hai. Nitazikwaje hilo kwangu mie halina umuhimuWewe hauogopi ?
Hahahahah saingine hata urembo unawasaidia 😂😂😂Vikundi mfano Vicoba, Upatu
Social networks
Ila pia hao marafiki huwa wanaangalia una nini.. ukiwa na cha kuoffer utawapata vizuri tuu. Hicho cha kuoffer sio lazima iwe pesa/kipato...
Mtaji unao? Nilichogundua its easy to get companyKuna mdada huwa napenda ile life style, weekends hupost status wapo kwenye coaster wanaenda kutembelea yatima yani wanavibe hao, usiku wapo pengine wanamwagilia moyo....napenda kwakweli ila mi sina
Ndio marafiki tulionaoMi nilipata rafiki kumbe ananichunguza jinsi ninavyofanya kazi muda si mrefu aligeuka kuwa mshindani wangu kumbe lilikuwa nafiki tu
Ni coriousty ambayo wengi wanayo kutokana na uwezo wao wa kufikiri (wakati wakiwa hai), ila forsure maiti haihitaji chochote izikwe na watu muhimu au manisipaa huwa haina maana yoyote kwa yenyewe.hivi kwa nini watu wanaogopa kuzikwa na manispaa?
Ni nzuri sana hii ila sikuhizi ulimwengu ulivyo waKuna kitu tunaita "network building" mara nyingi uandaliwa na balozi za nchi za kigeni kama USA, Denmark, Sweden,Japan,Canada, Japan, France & Germany etc japo baadhi unalipia around $30, 40,50 japo nyingine ni bure mara nyingi zinafanyikia Serena, Southern Sun Hotel,Four Season, Kempinsky na Cape Town fish market muda wa jioni baada ya kazi hasa ijumaa/alhamisi zinachukua lisaa 1 mpaka 2 hii utoa fursa ya wageni kupata marafiki na wenyeji kubadilisha mawazo.
Uwa zinaambatana na bites na vinywaji laini ni network building ambazo hamjuani unaenda kwa ajili ya kujuana na watu wapya, ni nzuri na zinakupa exposure kwakuwa hutaki marafiki wasioleweka zinakufaa, ikiwa utafeli/kuogopa kwenda kuna hizi nyingine ila nzuri kwa vijana zaidi hizi balozi za Nordic Countries,UK,France,Swiss,Germany etc huwa zinaandaa cinema kila alhamisi na huzialika balozi nyingine ni free entrance kwa wale wapenda wazungu zinawafaa kwasababu whites wanakuwa wengi mno na wanapenda watu weusi hapo ujanja wako tu wa kupata rafiki au hata mpenzi pia.
Nimehudhuria sana nimejifunza mengi.
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Usiogope kuchangamana na watu. Huwa kuna mambo mawili 1-Aibu na 2-Ego...Kwakweli najiona mi mwenyewe ni tatizo sio mwepesi wa kuchangama sasa nshaanza kuwa mzee ndio nashtuka....
Aje Kona bar hapa tupo kibao, tutamkuwadia ata mibaba ubaya imtafuneJichanganye anzia hapo ktk vikundi vya kina mama wenzio
Mama malizia muda wako tu hapa duniani umeshachelewa.Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa😔
Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.
Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.
Wenye marafiki mnawapataje???