Ngoja niandike uhalisia na ukweli wa maisha, even though sijui kwanini watu wengi wanaogopa uhalisia.
Sababu naona mnalazimisha kitu kisicho kuwepo wala kisichowezekana.
At the end utabaki peke yako tu na ukilinganisha marafiki wengi ni wanafiki ni kutumiana kwa faida na huo ndio uhalisia, I have got experience.
Kingine marafiki hawatafutwi bali mtajikuta mnakuwa karibu tu then baadae unaitwa urafiki lakini bado kamwe hamuwezi kuwa pamoja every moment.
Marafiki wa kweli ni familia yako tu namaanisha watoto na mke/mume. Lakini zaidi ya hapo watu baki watakuwa ziada tu kwenye maisha yako sababu siku zote watakuja na kuondoka lakini familia yako mtakuwa pamoja milele hata kama wengine wataenda mbali lakini siku zote mtabaki pamoja. trust me.
Familia yako hao ndio mtakao lia, kucheka na kufurahi wote pamoja na ndio mtakaozikana na watakao kuzika wewe.
Utapata mke/mume then mtazaa watoto wenu wanne au nane, mtawalea na kuwakuza kwa maadli mema mkiwa pamoja, mtakula na kunywa pamoja, mtacheka na kufurahi pamoja, mtaenda beach, Cinema, Vacations milimani, misituni na mijini.
Mtakwenda Shoppings, hotelini pamoja. Na wao watoto watakuwa wakubwa na kuwaletea wajukuu huku nyie mkianza kuzeeka lakini it doesn't matter sababu mtakuwa pamoja na hautokuwa alone na cycle itazidi kuongezeka huku wajukuu wakiwachangamsha na kuwakumbusha dhumuni na maana ya maisha. kutoka wawili wapendanao mpaka familia ya watu 16 au 20. kundi kubwa la watu ambalo ni your own creation imagine that? ni proud na furaha kiasi gani utajisikia just kutambua hilo?
Mtakutana na kupika na kula na kunywa pamoja huku mkifurahi kila siku hata kama haitokuwa kila siku it doesn't matter sababu siku zote watakuwepo pale utakapopata shida au utakapowahitaji.
Na siku ukifa hao ndio watakaokuja kukuzika na kukulilia na kukukumbuka milele na jina lako litaishi ndani yao.
Lakini kusema watu baki muwe wa kufa na kuzikana hiyo itabaki kuwa theory tu na ni kitu kisichowezekana kabisa.
Familia yako ndio marafiki zako wa kufa na kuzikana, huo ni Uhalisia. that's all.
Na ndio maana siwaelewi watu wanaosema Usioe au usizae na usiwe na mwanamke mmoja mimi nawaona bado watoto na akili zao hazijakua na kukomaa kiasi cha kuona uhalisia wa maisha. that's why nataka nioe mapema before it's too late, my future wife is a lucky woman I admit sababu dunia imejaa wahuni wasaka vitamu bila future wala kujua wanachokitaka au wanapokwenda bali wanaangalia sasa hivi tu.
Umesema unaanza kuzeeka then I'm really sorry kama ninachokifikiria ni kweli na wala sijamaanisha wala kukusudia kumuumiza yoyote.
Wale wanaoendelea kula tunda kimasihara na kula ujana sijui kuenjoy life na kula bata good luck, siku mtakuja kusoma hii comment na kukumbuka it's too late kumbe Uncle butcher alikuwa sahihi.