Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

The way unavyoongea iyo "napenda kwakweli Ila mi Sina"😂

Nimemkumbuka My Young Sister na kile kisauti chake kipindi kile anakuwa Daah!! Aliwaona wenzie wamependeza akapenda gauni la mmoja wao ndo akaniambia Ivo Ile gauni naipenda Kaka Ila me Sina😍😍

Ila suala la kuwa na marafiki ni the way unavyojiweka, inaonekana ww ni mgumu kuchangamana na watu. Sio mwepesi kujenga mazoea na watu.

Mwenzio kila weekend nakaribishwa kwa watu. Hakuna kitu kizuri Kama kuishi vizuri na jamii inayokuzunguka.

Mie nilitengeneza marafiki kutokana na kuwahudumia wateja vizuri kazini, achana na staff wa kazini maana wale wakikuzoea Sana heshima inashuka.

Nilikuwa najitahidi kutoa huduma vizuri, wengi hushukuru ndo mwanzo wa kufahamiana na kualikana.
Kwakweli najiona mi mwenyewe ni tatizo sio mwepesi wa kuchangama sasa nshaanza kuwa mzee ndio nashtuka....
 
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa😔

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
Umemuuliza kenzy?
Try to ask him anajibu lako.
 
Tatizo yaani watu wanapenda kufaidika wao tu...
Mimi ndo linalonishinda kwa kweli
Yaani ile mutual friendship sijawahi kukutana nayo..
Kuhusu shobo...mimi hainisumbui sanaa.
Napenda rafiki anaechangamka kunizidi..
Au tubalance shobo...yaani iwe equivalent flani hivi.
Tatizo linakuja mnashobokeana afu baadae unaanza kuona kabisa unakua una shobo zaidi..
Mutual Friendship ni chache sana na ndio anachotaka hata mleta mada... na ndio wengi hatujawapata hao watu
Mkishazoeana sasa unaanza unafiki na kukosa heshima
 
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa😔

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
Changamkia watu,usiwe unaniona Nina tu
 
Ndo kilichobaki hicho. Mimi Nashukuru ni mtu ambaye najitoa sana, Yani dizaini shosti akiumwa nitaenda nimpikie uji mwenyewe sio kumuagiza mdada wake wa Kazi, nimfulie...najitoa sana, Nashukuru pia watu wa karibu wananipenda....shida ni Mimi, I can't keep them....Yani naona mapungufu Yao sana, nikijua umenisema nalegeza urafiki, afu hairudi hiyo....siwezi unafki kabisaaa.
Ndo naishia kuwa nipo nipo tu!
Uko kama mimi. Sipendi urafiki wa kinafiki kabisa. Nina rafiki zangu wa 2 ndio tunasaidiana kwa shida na raha. Vikundi vingi vya akina mama vina majungu na unafiki hatari. Kikundi kinaanzishwa mara watu wanaanza kusemana inbox, mara kikundi ndani ya kikundi yaani ni shida sana
 
Kuna kitu tunaita "network building" mara nyingi uandaliwa na balozi za nchi za kigeni kama USA, Denmark, Sweden,Japan,Canada, Japan, France & Germany etc japo baadhi unalipia around $30, 40,50 japo nyingine ni bure mara nyingi zinafanyikia Serena, Southern Sun Hotel,Four Season, Kempinsky na Cape Town fish market muda wa jioni baada ya kazi hasa ijumaa/alhamisi zinachukua lisaa 1 mpaka 2 hii utoa fursa ya wageni kupata marafiki na wenyeji kubadilisha mawazo, huwa zinaambatana na bites na vinywaji laini ni network building ambazo hamjuani unaenda kwa ajili ya kujuana na watu wapya, ni nzuri na zinakupa exposure kwakuwa hutaki marafiki wasioleweka zinakufaa, ikiwa utafeli/kuogopa kwenda kuna hizi nyingine ila nzuri kwa vijana zaidi hizi balozi za Nordic Countries,UK,France,Swiss,Germany etc huwa zinaandaa cinema kila alhamisi na huzialika balozi nyingine ni free entrance kwa wale wapenda wazungu zinawafaa kwasababu whites wanakuwa wengi mno na wanapenda watu weusi hapo ujanja wako tu wa kupata rafiki au hata mpenzi pia.
Nimehudhuria sana nimejifunza mengi.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ongeza nyama
 
Bado sijaona comment ya jinsi ya kupata rafiki wa kweli kufa na kuzikana naona wengi ni kujiunga na vikoba ambayo sio mbya lakini naona inakuwa kama wanachama zaidi maana mambo ya vikoba ya kiisha hamna mawasiliano.
 
Kosa lako linaanzia hapo unaposema unataka "marafiki wa faida"

Au labda mimi sikuelewi unachomaanisha, nilivokuelewa ni kuwa unataka kuwa na marafiki, ili upate faida hasa hasa ya kipesa, kama ni hivyo, iyo ni moja ya sababu ndo maana hupati marafiki. Sijui baadhi ya watu mkoje.

Ondoa hiyo mentality ovu ya kishetani, ya kujenga urafiki na mtu ili ufaidike na kitu fulani toka kwake, jenga urafiki na mtu kwa sababu mko compatible na mna enjoy each other's time.

Ndo maana baadhi ya matajiri hawataki urafiki na maskini, sababu wanawakwepa nyie Mnaotafuta marafiki wa faida, maana anajua umejenga naye mazoea sababu ya pesa zake, Na si kwasababu umependa uwepo wake Evelyn Salt
Motivational speakers mmeshaanza tayari.
 
Back
Top Bottom