Mahakama ya Kisutu imemuhukumu Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Rutty' na Mpenzi wake Said Bakary pamoja na James Charles (James Delicious) kulipa faini ya milioni 11 ama kwenda jela miaka mitano, ni baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matatu ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya "nimezingatia hoja za pande zote mbili na athari za makosa haya, ni kweli Washitakiwa wote Vijana na wanategemewa, nimeona mshitakiwa wa kwanza anajutia, Mshitakiwa wa pili na tatu ni wakosaji wa kwanza, kutokana na mazingira ya kesi hii adhabu yake ni miaka 30 kila kosa ambapo nikiwafunga mtapotea kabisa"
"Hivyo kwa mazingira mliyoyasema na lengo la adhabu ni kujirudi, mshitakiwa wa kwanza utalipa Mil.3 ama jela miaka 5, wa pili utalipa faini ya Mil.3 ama jela miaka 5 na mshitakiwa wa tatu faini Mil.5 ama jela miaka 5"
Amberutty na wenzake wameshindwa kulipa faini hiyo kwa leo hivyo wamepelekwa Gerezani na endapo watafanikiwa kulipa wataachiwa huru. #MillardAyoUPDATES