Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
Naishije haya maisha kwani nahisi kuchanganyikiwa. Mimi ni mama wa watoto 5, niliolewa lakini nimedai talaka na imetoka sina hata shilingi mia kaka. Iko hivi, mume wangu ni mfanyakazi wa serikali, ana kipato kikubwa na mara nyingi yuko bize sana kazini, alinifungulia biashara na katika hii biashara ndiyo nikaja kukutana na huyu mwanaume. NIlikua natumia pesa ya biashara kumhonga huyu mwanaume mtaji ukiisha namumbia mume wangu ananipa mwingine. Kila kitu kilikua vizuri na ndugu zangu walikua upande wangu kwani nao nilikua nawapa pesa tu na kwa kuwa mume wangu si mtu wa kuhangaika na ndugu walimchukia bila kujua pesa zinatoka kwake.
Kilichotokea ni kuwa mimi na mume wangu tumechuma mali nyingi sana, tuna nyumba 12, hivyo katika kuongea na ndugu zangu na huyu mwanaume walinishawishi niombe talaka ili tugawane mali, na kwa kuwa mimi ni mke wake nilijua nitachukua nyumba 6 na yeye kubaki na nyumba sita. Nilianza kuhangaikia talaka tangu mwaka 2021, mume wangu alijua nachepuka, hata wanangu walikua wanajua na sikuwa naficha kwani nilikua nikifanya makusudi ili mume wangu aniache tupeane talaka.
Kila tukifika baraza la mtaa mume wangu alikuwa analia kama mtoto, anaomba kuhusu kurudiana kuwa bado ananipenda, ananipa pesa mimi narudi. Tunarudishwa namfanyia vituko mpaka basi. Mwaka huu tulipofika alikubali kuhusu kunipa talaka, mpaka mahakamani mimi ndiyo nilienda na mume wangu alikubali kunipa talaka. Nilipoorodhesha nyumba tulizonazo, mume wangu alisema nyumba hizo si zetu ni za watoto.
Mimi sikufuatilia na sikujua sababu ya mume wangu kuendelea kulazimishia kubaki na mimi. Kumbe nyumba zote na kila kitu chake alishabaidlisha na kuandika majina ya Watoto na ubaya nikuwa hata mimi nilisaini bila kujua. Alikua hataki kunipa talaka kwakua alikuwa anasubiri watoto wangu wakubwa wawili wafikishe miaka 18 ili wao ndiyo wawe wasimamizi wa mali za wadogo zao. Kanipa talaka kwani sasa hivi wanangu 3 wana zaidi ya miaka 18 na ndiyo kawaandika kama wamiliki na wanaisimamia za wadogo zao wawili. Yeye hamiliki chochote kwenye hizo mali hivyo talaka imetoka sina hata shilingi mia. Kaniachia duka lakini halina kitu kwani mtaji wote nilikua nikimtegemea yeye, mume wangu yeye ana kazi ana kipato kikubwa, na watoto wangu wakubwa hawanitaki kabisa kwani wanasema nilimdhalilisha baba yao.
Mwanaume niliyemtegemea naye kaniacha, hataki hata kuniona, yaani ana ndugu hawakutaka hata kunipokea, nimetoka kuishi nyumba ya ghorofa sasa naishi chumba kimoja. Nisaidie nimejifunza nimejua nilipokosea sitaki tena talaka, ni ndoa ya kanisani najua mbinguni bado ipo lakini namshawishije mume wangu kunirudia, naona kama ananikomoa. Tumeishi miaka 22 mimi na yeye, hanionei huruma hata nikimuomba matumizi ananiambia sina nisaidie najitoaje hapa!