Amefika benki na kukuta deni ambalo halifahamu

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,960
Reaction score
2,945
Muda si mrefu napokea simu kutoka kwa relative yangu mmoja,

Kisa chake alivyonisimulia kiko hivi. Ameenda benk, anataka aombe mkopo (basically kufanya top up).
Ila ana mkopo mwingin benk ya NMB.

Sasa huko akaambiwa kwenye mfumo kuna deni la milioni 3 NMB.

Alipoenda NMB napo wanaangalia wanamweleza kuwa na wao hawajui ila inasomeka CRB. Katika kuuliza ndo kitu gani na inatokana na nini nao hawana maelezo yaliyonyooka, ameishia kuahidiwa asubiri hadi kesho watafuatilia.

Nikamshauri labda una deni kwenye miamala ya simu, akasema hapana, isipokuwa alikuwa nadeni la 50k kwenye m pesa na aliclear kabla hajaenda huko. Kimsingi nimeshindwa cha kumjibu, hivi kuna wadau waliowahi kukutana na kadhia hii?
 
Credit bearau (CRB) ambayo inachukua taarifa zote za mikopo uliyonayo kutoka kwa taasisi yoyote na makampuni ya simu! lazima una mkopo sehemu na wametoa taarifa zako kuwa wewe ni mkopaji mbaya haulipi madeni kwahiyo hapo huwezi kukopa!
 
Hakuna taasisi zingine zaidi ya hizo benki mbili. na ana line 1 tuu ya simu, ni mtu namfahamu in details, japo siwezi kumsemea just because tuna undugu.
 
Sawa ila ndio tayari inasoma hivyo, na maana ya crb nimekupa! Hapo jamaa achekeche mwenyewe..huenda mtu kakopea salary slip yake huko na hamjui lolote!
 
Arudi kesho kama walovyomiahidi atapata muafaka. Maisha ya sasa ni mifumo hakuna wa kitakachokosa evidence source
 
Nitacomment kesho baada ya hayo majibu Ila jamaa anadaiwa na bank nyingine
 
Muda si mrefu napokea simu kutoka kwa relative yangu mmoja,

Kisa chake alivyonisimulia kiko hivi. Ameenda benk, anataka aombe mkopo (basically kufanya top up).
Ila ana mkopo mwingin benk ya NMB.

Sasa huko akaambiwa kwenye mfumo kuna deni la milioni 3 NMB.

Alipoenda NMB napo wanaangalia wanamweleza kuwa na wao hawajui ila inasomeka CRB. Katika kuuliza ndo kitu gani na inatokana na nini nao hawana maelezo yaliyonyooka, ameishia kuahidiwa asubiri hadi kesho watafuatilia.

Nikamshauri labda una deni kwenye miamala ya simu, akasema hapana, isipokuwa alikuwa nadeni la 50k kwenye m pesa na aliclear kabla hajaenda huko. Kimsingi nimeshindwa cha kumjibu, hivi kuna wadau waliowahi kukutana na kadhia hii?
CRB ni TAASISI ambayo kama kuna SEHEMU ukikopa halafu ukakwepa kulipa DENI, unawekwa jina lako huko ili usikopesheke kwingine kote.

Jambo la msingi akam hajui kabisa kuwa alikopa MPESA, TIGO PESA, au kwingine, aende CRB ataambiwa hilo deni ni la wapi?
 
I can bet huyo mtu kweli anadaiwa. Ila tu kwa sababu ya kuishi kimazoea hawezi jua deni limetoka wapi mpaka aambiwe.
 
Huu upumbavu tulizoea kusikia huko Congo na Burundi.
Sikutarajia kama nchi yetu itafikia huku.
Sasa kama jumuiya ya madola na nchi hisani zilizokuwa zikisuport Budjet yetu kwa misaada zimejitoa, tutegemee nini? Hivi mpaka kufikia hatua ya kuuza hazina ya shahabu ilikusuport miradi ya ndani unazani ni mchezo mkuu.? Kiufupi TUNAANGAMIA KIUCHUMI.
 
Back
Top Bottom