Amekataa kunirudishia pesa niliyoituma kimakosa, kisa nilimjibu jeuri

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
15,771
Reaction score
14,294
Mwanaasha Hamis ni hatari sana muogopeni!

Ni leo, majira ya saa saba nilikuwa namtumia MTU pesa yake nikakosea namba, badala ya 071513 nikaandika 071523, nikatuma pesa.

Sikustuka mpaka mwenye hiyo namba aliponipigia Simu akawa ananiuliza wewe ni nani? Huwa ninaamini mtu anayenipigia ndiye hupaswa kujitambulisha hivyo hata alivyouliza unakaa wapi nilimjibu duniani.

Binti akakasirika sana akakata simu. Nilipogundua kukosea kutuma pesa na kumpigia binti simu loo!, binti kawa mkali. Anasema hanirudishiii wala nini, anadai nimemjibu vibaya.

Nikamuomba akate anayotaka anirushie itakayobaki binti kagoma, anasema 'Asante kaka kwa kunitumia pesa, Leo nakula chips Kuku na soda'. Nikamuuliza unakaa wapi, naye amejibu 'nakaa duniani' eti anataka nijifunze.

Kwahiyo leo Mwanaasha anakula chips Kuku na soda kwa pesa yangu.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Hesabu sadaka umetoa hiyo.. (kama hii story ni ya kweli lakini)..:biggrin:
 
Yaani we umenifanya nicheke kwa nguvu looh! Asa c umempa mwenyewe

cjampa nimekosea halafu,wakati ananpigia alishazitoa,na nilivyopiga Tgo wamethbitisha alishazitoa kwa hyo alishaamua.Nimemwambia nitaskitika sana ukikosa thawabu kwa kitu kidogo akajibu,Yuko tayari akose thawabu kwa ajili yangu.Anasema sirudishi sirudishii mkaka una nyodo sana wakati hatufahamiani
 
Hahahahaaaa!!!kitu cha kusikitisha ila nimejikuta nacheka...pole ndugu
 
hivi tanzania kuna mwanaasha hamis wangapi???kama ulidhani unamuumbua kwa kutaja jina na namba yake imekula kwako!sidhani kama kuna mtu hapa ameiona hiyo hatari ya mwanaasha,umekosea mwenyewe,umejibu vibaya...na hiyo ndio stahili yako
 
Nna uhakika ulivopokea ungeongea naye vizur. Pesa yako ungeipata Ila kiburi chako kimekuponza.

Hata ingekuwa mimi nisingekupa. Yaani umekosea nakupigia simu unaleta kujua.

Mi nasema hela yako iliwe tu hakuna namna tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…