Amekataa kunirudishia pesa niliyoituma kimakosa, kisa nilimjibu jeuri

Amekataa kunirudishia pesa niliyoituma kimakosa, kisa nilimjibu jeuri

hivi tanzania kuna mwanaasha hamis wangapi???kama ulidhani unamuumbua kwa kutaja jina na namba yake imekula kwako!sidhani kama kuna mtu hapa ameiona hiyo hatari ya mwanaasha,umekosea mwenyewe,umejibu vibaya...na hiyo ndio stahili yako

asante bwana Mc tilly,Mimi nimeona nishiriki na wanajukwaa kuhusu kilichonikuta Leo naona we we umepanic kweli na unatoa povu jingi,sawa ni mtizamo wako.Ila hujatenda sawa kumbuka Mzee Ben pale jangwan aliongea kama wewe tu.
 
Kwa jina hilo ulilolitaja atakuwa ni mkazi wa Mgomeni bila shaka.
 
nipe hiyo namba yake nimpe jamaa yangu wa tigo tumkomeshe wizi
 
Wewe jamaa una akiri sana, lazima kuna watu watatuma buku tano tano za kutosha ili kufanya research.
 
Amekutibu,next time utajifunza kujibu vizuri.
Fedhuli dawa yake jeuri.
 
asante bwana Mc tilly,Mimi nimeona nishiriki na wanajukwaa kuhusu kilichonikuta Leo naona we we umepanic kweli na unatoa povu jingi,sawa ni mtizamo wako.Ila hujatenda sawa kumbuka Mzee Ben pale jangwan aliongea kama wewe tu.

oooh sorry nilisahau kukupa pole,pole mkuu!ila si umesema hela yenyewe atakula chipsi yai maana yake ni kidogo si ndio mkuu???mezea tu ndio maisha hasara zipo tu!
 
oooh sorry nilisahau kukupa pole,pole mkuu!ila si umesema hela yenyewe atakula chipsi yai maana yake ni kidogo si ndio mkuu???mezea tu ndio maisha hasara zipo tu!

yeye ndo alisema atajula chips na Kuku Leo.mwanaisha Hamid ni Hatari sana
 
ni leo,majira ya saa saba nilikuwa namtumia MTU pesa yake nikakosea namba badala ya 071513... nikaandika 071523... nikatuma pesa.sikustuka mpaka mwenye hiyo namba aliponipigia Simu akawa ananiuliza wewe ni nani? huwa ninaamini MTU anayenipigia ndiye hupaswa kujitambulisha hi vyo hata alivouliza unakaa wapi nilimjibu,duniani.binti akakasirika sana akakata Simu,nilipogundua kukosea kutuma pesa na kumpigia binti simu loo!binti kawa mkali snasema hanirudishiii wala ni ni anadai nimemjibu vibaya.Nikamuomba akate anayotaka anirushie itakayobaki binti kagoma anasema,asante kaka kwa kunitumia pesa Leo nakula chips Kuku na soda.nikamuuliza unakaa wapi Naye amejibu nakaa duniani eti anataka nijifunze.kwahiyo Leo mwanaasha anakula chips Kuku na soda kwa pesa yangu.ni hayo tu kwa sasa.

nipe namba yake huyo mwanaasha
 
amekukomesha...safi..uache kujibu watu vibaya
 
Tutamkomesha. yeye kama anajua matawi sisi tunajua mizizi halafu tunachimba wenyewe.
 
Back
Top Bottom