Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
elfu 10
Wareverse vipi pesa ishatolewa ndugu?
Toa taarifa polisi umfungulie kesi ya madai,.pia toa namba yake kamili usaidiwe kumsaka. Najua atafunga line lakini tutampata kupitia simu alizopigiwa au kupiga hivi karibuni. Akiwa mwaaminifu atakurudishiia japo kidogokidogo.
Safi sana.............
Kuna mtu pia aliwahi nirushia pesa kwa makosa.... baada ya kumpigia alinijibu shombo vibaya mno.....
Ila yeye ana bahati baada ya kugundua makosa na kulia lia nilimrushia robo tatu....
Ni vyema kujibu watu vizuri hujui ni kwa nini ametumia muda wake na salio lake kukutafuta
Mwanaasha Hamis ni hatari sana muogopeni!
Ni leo, majira ya saa saba nilikuwa namtumia MTU pesa yake nikakosea namba, badala ya 071513 nikaandika 071523, nikatuma pesa.
Sikustuka mpaka mwenye hiyo namba aliponipigia Simu akawa ananiuliza wewe ni nani? Huwa ninaamini mtu anayenipigia ndiye hupaswa kujitambulisha hivyo hata alivyouliza unakaa wapi nilimjibu duniani.
Binti akakasirika sana akakata simu. Nilipogundua kukosea kutuma pesa na kumpigia binti simu loo!, binti kawa mkali. Anasema hanirudishiii wala nini, anadai nimemjibu vibaya.
Nikamuomba akate anayotaka anirushie itakayobaki binti kagoma, anasema 'Asante kaka kwa kunitumia pesa, Leo nakula chips Kuku na soda'. Nikamuuliza unakaa wapi, naye amejibu 'nakaa duniani' eti anataka nijifunze.
Kwahiyo leo Mwanaasha anakula chips Kuku na soda kwa pesa yangu.
Ni hayo tu kwa sasa.