Amekataa kunirudishia pesa niliyoituma kimakosa, kisa nilimjibu jeuri

Amekataa kunirudishia pesa niliyoituma kimakosa, kisa nilimjibu jeuri

Safi sana.............

Kuna mtu pia aliwahi nirushia pesa kwa makosa.... baada ya kumpigia alinijibu shombo vibaya mno.....

Ila yeye ana bahati baada ya kugundua makosa na kulia lia nilimrushia robo tatu....

Ni vyema kujibu watu vizuri hujui ni kwa nini ametumia muda wake na salio lake kukutafuta
 
Toa taarifa polisi umfungulie kesi ya madai,.pia toa namba yake kamili usaidiwe kumsaka. Najua atafunga line lakini tutampata kupitia simu alizopigiwa au kupiga hivi karibuni. Akiwa mwaaminifu atakurudishiia japo kidogokidogo.
 
hahaha naona umeamua kubadili heading eee ... kwa kweli umemdhalilisha mdada wa watu, umemkosea na bado umemsema vibaya kwenye hii thread ...
mpigie simu umwombe msamaha
 
Anasema nimesema namshtaki kwa hyo atanishtaki yeye,Ila uzuri kanirejeshea pesa yangu sina matatizo na mwanaisha tena walionicheki wameshindwa. tens.walionibeza limewashuka
 
Wareverse vipi pesa ishatolewa ndugu?

Kwa kuwa ameshaitoa, watakachofanya ni kublock tigo pesa account yake, kisha account itakapowekwa kiasi kinachofika thamani tajwa then watakurudishia(reverse). Kwa sasa kuwa mpole
 
Hahaaaa......"muwoweeeeee" naona nyote ni "wacheshi" mna match vizuri
 
Toa taarifa polisi umfungulie kesi ya madai,.pia toa namba yake kamili usaidiwe kumsaka. Najua atafunga line lakini tutampata kupitia simu alizopigiwa au kupiga hivi karibuni. Akiwa mwaaminifu atakurudishiia japo kidogokidogo.

huwezi amini ndugu kuna MTU kamwambia Yuki front page jf kazirudisha zote
 
Huwezi jua kiongozi pengine ni mwanzo wa mahusiano murua ile tunaita a blessing in disguise
 
Safi sana.............

Kuna mtu pia aliwahi nirushia pesa kwa makosa.... baada ya kumpigia alinijibu shombo vibaya mno.....

Ila yeye ana bahati baada ya kugundua makosa na kulia lia nilimrushia robo tatu....

Ni vyema kujibu watu vizuri hujui ni kwa nini ametumia muda wake na salio lake kukutafuta

Hiyo ya kumrudishia robo tatu kama chai vile.................:majani7::majani7::majani7:
 
Mwanaasha Hamis ni hatari sana muogopeni!

Ni leo, majira ya saa saba nilikuwa namtumia MTU pesa yake nikakosea namba, badala ya 071513 nikaandika 071523, nikatuma pesa.

Sikustuka mpaka mwenye hiyo namba aliponipigia Simu akawa ananiuliza wewe ni nani? Huwa ninaamini mtu anayenipigia ndiye hupaswa kujitambulisha hivyo hata alivyouliza unakaa wapi nilimjibu duniani.

Binti akakasirika sana akakata simu. Nilipogundua kukosea kutuma pesa na kumpigia binti simu loo!, binti kawa mkali. Anasema hanirudishiii wala nini, anadai nimemjibu vibaya.

Nikamuomba akate anayotaka anirushie itakayobaki binti kagoma, anasema 'Asante kaka kwa kunitumia pesa, Leo nakula chips Kuku na soda'. Nikamuuliza unakaa wapi, naye amejibu 'nakaa duniani' eti anataka nijifunze.

Kwahiyo leo Mwanaasha anakula chips Kuku na soda kwa pesa yangu.

Ni hayo tu kwa sasa.

Kwanza ww ni chama gani labda nianze na hapo kwanza
 
Back
Top Bottom