Amenichumbia lakini hataki Ndoa

Amenichumbia lakini hataki Ndoa

Ni jambo la kumwambia mwenzio una hiki na kile kinachopelekea nisifikilie kufunga pingu za maisha
Hahahaha! Mwengine hata ukimuambia kazi bure,habadiliki,na anakujibu kuwa mimi ndo fulani, siwezi kubadilika,nipo kama nilivyo,utafanyaje kama wewe mwanaume?
 
Zungumza nae, mpe timeframe /deadline yako

Kisha Acha kumkumbushia ndoa

Tafuta pesa tengenezq kesho yako.

Yaani kuwa busy na kesho yako kuliko mchwa .........(sasa sio unawekeza halafu mlivyo na kiherehere unaweka na jina lake)

Hakikisha hubebi mimba.........ukibeba kwisha habari yako!!!!!

Narudia hangaikia kesho yako....


Kama takupenda mtaendelea na stage ya pili

Kama bado anafuta kila mmoja atalala mbele!!!!
Acha kumdanganya mwenzio, mchakato wa kutolewa mahari unainvolve kuandikishina na kila pande inabaki na nakala. Mahari inahalisha ndoa ya kimira na inatambulika.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Habari za asubuhi wakuu wote wa JF na hongereni kwa shughuli mbalimbali za kujenga taifa.

Kilichonileta kwenu asubuhi hii ni kunisaidia mawazo ya hili nalopitia kwa sasa,me na mwenza wangu tunamiaka mitatu sasa tunaishi pamoja na ni mwaka mmoja wa kuchumbiwa.

Kama mjuavyo, desturi zetu za Kiafrika baada ya mahari mnaulizwa tarehe ya Ndoa ndivyo ilivyokua na kwetu pia ila mwenzangu aliomba ajipange sababu hakua vizuri kwa kipindi hicho hivyo wazazi walimkubalia.

Sasa napata maswali mengi kutoka kwa wazazi na ndugu wakiniuliza ndoa lini mpaka nakosa majibu sababu nikimuuliza mwenzangu ananiambia nina haraka gani nisubiri.

Kilichonifanya nije kwenu ni kuomba ushauri je niko sahihi kuendelea kutumikia majukumu yangu ya ndoa kwa mgongo wa kuchumbiwa au nimechutama choo cha kiume?
Kimila nabkisheria za nchi yetu tayari hiyo ni ndoa.
Habari za asubuhi wakuu wote wa JF na hongereni kwa shughuli mbalimbali za kujenga taifa.

Kilichonileta kwenu asubuhi hii ni kunisaidia mawazo ya hili nalopitia kwa sasa,me na mwenza wangu tunamiaka mitatu sasa tunaishi pamoja na ni mwaka mmoja wa kuchumbiwa.

Kama mjuavyo, desturi zetu za Kiafrika baada ya mahari mnaulizwa tarehe ya Ndoa ndivyo ilivyokua na kwetu pia ila mwenzangu aliomba ajipange sababu hakua vizuri kwa kipindi hicho hivyo wazazi walimkubalia.

Sasa napata maswali mengi kutoka kwa wazazi na ndugu wakiniuliza ndoa lini mpaka nakosa majibu sababu nikimuuliza mwenzangu ananiambia nina haraka gani nisubiri.

Kilichonifanya nije kwenu ni kuomba ushauri je niko sahihi kuendelea kutumikia majukumu yangu ya ndoa kwa mgongo wa kuchumbiwa au nimechutama choo cha kiume?
Kimila na kisheria hiyo tayari ni ndoa
 
Kilichonifanya nije kwenu ni kuomba ushauri je niko sahihi kuendelea kutumikia majukumu yangu ya ndoa kwa mgongo wa kuchumbiwa au nimechutama choo cha kiume?
If you can get free milk, why keeping a cow? Hahahaha RIP Lwakatare
 
Mabinti wa kichaga ukiwachekea hujengi aisee
 
Ushaolewa tayari...sema unataka sherehe tu.
 
Kuna wenzake walicheza sana ukumbini tena kwa gharama kubwa sana ya kukodisha huo ukumbi wa kuchezea,lakini leo hii Ndoa zao mashaka matupu!! Amshukuru Mungu kwa kila Jambo!!
Dah!...Mungu atulinde
 
Nataka Ndoa ya kanisani kwa mahari tu am insecure
Kimsingi una haki ya kutakiwa kuolewa kwa ndoa ya kanisani. Kwa mimi naakuunga mkono. Kama vipi zungumza na jamaa mfanye tafrija ndogo tu ambayo mtaweza alika watu hata 60 tu kutoka kila upande.

Chakula kiwe simple bajeti iwe ndogo sana. Kama ni kumbukumbu basi picha za studio zitafanya kazi maana mkipiga picha za location eg. Bustani, na zile za Groom & Bride kwaajiri ya kiweka sebuleni zoezi linakuwa limekwisha vema kabisa.

Ndoa zipo za haraka zile ambazo unaandikisha na kufunga ndani ya wiki.
 
Sli la nyumbani naloulizwa ni kama jamaa amekua teyari mpk kulipa mahari kwanini amekua mzito kwenye kumalizia ndoa hata kama kwa sherehe ndogo tu ya watu wa karibu ameamua kukaa kimya
Wewe ukizungumza nae kuhusu hili anakwambia sababu ni kitu gani hadi amechuna kufanya ndoa na sherehe?!

Pengine ni ugumu wa maisha na hana uwezo binafsi wa kufanya hiyo kitu na pengine mbaya zaidi ni kuwa familia na nduguze hawawezi mchangia gharama.
 
Kwenu ilifukuzwa
We sasa unataka mwenzako aje jutia. Badala ya kushauri azungumze na mwenzake vizuri unaanza story za yeye kurudi kwao.

Wanawake wa siku hizi sijui mpoje yaani wepesi sana kufanya maamuzi ambayo ukija kaa chini baadae unakuja kujiona ulitumia akili za kisichana kwenye mambo ya kiutuuzima. Unajuaje labda jamaa anajipanga kimya kimya kwasababu hali yake sio nzuri kifedha?!

Sometimes Wanaume tunakuwa kimya ni kwasababu ya aina ya wanawake tulio nao. Unakuta sio mwanamke ambaye ni mshauri mzuri na pia sio muelewa hata unaposema uketi nae chini mzungumze kiutuuzima anakuwa si mtu ambaye ni co-operative, ni mtu wa kulaumu na kukusomea list ya mahitaji au changamoto. Ila sio mwanamke ambaye atakuwa partner kiuchumi.
Mtu kama huyu unakuwa unamuona kama mwanao au mtoto mdogo kiasi kwamba akikwambia jambo zito kama ndoa ambalo linahusiana na fedha tena zaidi ya milioni 10 unabakia tu kumwambia angojee maana hata ukimuelekeza si mtu ataekupa positive contribution ya mawazo wala idea au hata kujiongeza atabakia kutumbua macho na kukwambia we ndo mwanaume.
 
Ni kweli. But u are between a hard rock and a stone right now. Uko kwenye position mbaya sana. I wish ungekuja kuomba ushauri kabla ya kuanza kuishi nae (baada ya mahari). Mimi ningekushauri kwa herufi kubwa; USIANZE KUISHI NAE,HADI BAADA YA KUAPA KANISANI.
Ila sasa umeshakosea pakubwa sana. Yaani ulipo sasa ni kuomba Mungu tu hilo la kwenda kuoa mwingine lisitokee, you dont have much to do zaidi ya kusubiri "neema" zake huyo mwanaume awiwe kukuoa.
Kwa kifupi kaaanza kazi bila mkataba.
 
Nitajie fungu hata moja kwenye Biblia linalosema tufunge ndoa kanisan au serikalini?
Watu wote kwenye biblia walipolipa mahali tayali ilihesabika ndoa
Dhambi ni kuishi na mtu hajakulipia mahali ila kama umelipiwa wewe ni mke wa mtu sio mchumba
Mahari ni jambo la kitamaduni. Kiimani kufunga ndoa ni kuweka agano la Kiroho na mtu.
 
Kuna ndoa tatu ndg
1. Kanisan
2. Serikali
3. Kimira
Hii ya tatu inahusisha upokeaji wa mahali kwa maandishi na zote zinatambulika kisheria

Huyu ni mke wa mtu aache ujinga na tamaa za vigelegele
Kimira [emoji777]

Kimila[emoji3581]
 
Back
Top Bottom