Mimi naona wewe na familia yako inabidi mjaribu kumuelewa jamaa nini kinachomfanya acheleweshe harusi.
Kaa nae chini kwa utulivu kabisa muulize vipaumbele vyake katika maisha yake, na katika hivyo vipaumbele harusi ni kipaumbele cha ngapi?
Itakua rahisi kuwaelezea hata familia yako kwamba jamaa kasema ana moja mbili tatu anataka atimize halafu ndo mtafunga ndoa.
Mwambie "baby mi sikulazimishi tufunge ndoa mapema, ila nataka tu kujua vitu gani unataka kuvitimiza ndo moyo wako utaridhia kufanya harusi, angalau hata nyumbani nikiulizwa niweze kuwajibu kitu cha maana."
Sent from my SM-G570F using
JamiiForums mobile app