Amenichumbia lakini hataki Ndoa

Sawa bwn
Ila namtahadharisha cheti si kila kitu
Kikubwa amani ndani
 
Hahahahah ukweli mchungu, mchawi cheti tu kwahio cha kuomba ni wakahidhinishe tu kama mahari ishalipwa hamna tatizo
 
Wewe mwambie hapa tunafunga ndoa ama mie nasepa zangu. Jipe thamani mwenyewe kwanza. Miaka mitatu anasasambua mbususu tuu hataki kufunga ndoa hayupo serious
Unapomwambia hilo mwanaume mwenye pesa zake unatarajia nini😅??? Tembea tu mlango uko wazi haipiti wiki atakuja mwenzio humu humu
 
Huwa napata mashaka sana napoona mwanamke msisitizo wake unakuwa kwenye cheti cha ndoa,natafakari kwa upana sana,anataka kufanyia nini hiko cheti? Ukiona mwanamke msisitizo wake umuoe apate cheti cha ndoa,huyo wa kupiga chini fasta.
😅😅😅😅😅😅 mwanamke anataka security ya child support na nyumba
 
Ukwel daima fitina kwangu mwiko...

Hapo mwana anakula bure tu..tena bila kero kwa mgongo wa pete ya uchumba..hahahah..mwamba hatar snaa
 
Hakuna shida kwani ulimpa Amani na furaha mwenzio kwa kumtimizia hitaji lake
 
Ile ni demo ya Ndoa 😅 sema huwa tamu sana kama mwanamke sio msumbufu unamzalisha kisha unamuoa akiwa na watoto wake kabisa 😅
Kwa hiyo mkuu miaka yote unaishi na Mwanamke bila ndoa haufanyi ibada kwenda msikitini au kanisani kwa sisi Waislamu mwenzi mtukufu inabidi urejee kwenu kwa sababu unaisabiwa mzinifu hata kama kakulipia mahari acheni kuhalalisha jeusi kuwa nyeupe.
 
Kwa hiyo mkuu miaka yote unaishi na Mwanamke bila ndoa haufanyi ibada kwenda msikitini au kanisani kwa sisi Waislamu mwenzi mtukufu inabidi urejee kwenu kwa sababu unaisabiwa mzinifu hata kama kakulipia mahari acheni kuhalalisha jeusi kuwa nyeupe.
Heheheh hamna bana hizo ni dhana potofu tu! Hamna cha uzinifu sababu nadhiri iko moyoni mungu anaelewa
 
Wap kwenye biblia wameandika tukafunge ndoa au nioneshe fungu hata moja wametaja flan aliemda kanisan au kwa kiongozi wa dini akafungishwa ndoa? Haipo na haijawahi kuwepo hizi ni sheria nje ya Biblia dini zimejitungia
Acha ukuda wewe.

Sasa kama haipo hivyo haimaanishi asiende kufunga ndoa kanisani. Anachotaka ni uhalali wa kutambulika kisheria.

Kwaiyo kama haijaandikwa kwenye biblia so akaushe tu asililie ndoa?

Punguza ujuaji, msaidie ushauri kwa situation aliyofikia sio kuleta vitu nje ya tatizo linalohitaji ufumbuzi.
 
Ndoa ni pande mbili kukutana na kupeana baraka na kukubaliana tu. Ndio maana hata ukienda kufunga ndoa iwe popote Msikitini ama Kanisani lazima uulizwe kama pande zote zimeafiki. Haya mambo ya kupewa cheti ni kuiga tamaduni za wenzetu tu. Bi dada kama una baraka za Wazazi wako tulia. Kama wazazi wako wanataka kurindima ukumbini hapo kuna kipengele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…