Amenichumbia lakini hataki Ndoa

Amenichumbia lakini hataki Ndoa

Pole sana kwa changamoto, jitahidi tu kumsisitiza ili muweze kufunga ndoa siyo vizuri kuishi bila ndoa hiyo ni dhambi kwa Mungu.
Hiyo dhambi imeandikwa wapi, ina maana sisi tunaotorosha tutahukumiwa na moto wa jehanamu kisa tu hatukufunga ndoa, imeandikwa wapi ni dhambi
 
Tunaishi kwa amani na upendo kwakweli anajali hatukosi mahitaji ila niko insecure

Hili sasa ndio tatizo la wanawake wengi,,,, hapo unachotaka ni security na wala sio ndoa,,kwasababu kama ni ndoa tayari umeshalipiwa mahari...

Na wanaume wakilipa mahari ndio wengine huwa imeisha hio,, Wanawake mkipata hiko cheti(Security), huwa mnakuwa watu wa hovyo sana..

Nashauri na kuomba jamaa ako aendelee na moyo huo huo wa kukaza hilo swala la kipuuzi,,kama amekamilisha tamaduni(mahari + barua)..haina haja ya hayo mengine.
 
Hayo ndio maamuzi ya kiume. Shukuru walau mahari wazee wamekula Sasa wewe unataka nini kingne Maana Kama mume unae. Tunza ndoa yako bidada na Mungu awajalie muzae nke na ndume.

Anataka shamra shamra akalingishie mashosti[emoji1787]
 
Kwani akikuoa nini kinaongezeka? Kashalipa mahari, na wewe tayari unatumikia majukumu ya ndoa, shughuli imeisha hapo.
Subiri siku ya siku usikie kaoa mwanamke mwingine, utupiwe virago.

Anataka waingie kwenye madeni kisha aanze Kumnunia jamaa

Sisi tulishakubaliana 4 years itumikie kwanza tuone Kama unastahili

Na hii ina apply kwa wote

Au nasema uongo ndugu zangu
 
Habari za asubuhi wakuu wote wa JF na hongereni kwa shughuli mbalimbali za kujenga taifa.

Kilichonileta kwenu asubuhi hii ni kunisaidia mawazo ya hili nalopitia kwa sasa, mimi na mwenza wangu tuna miaka mitatu sasa tunaishi pamoja na ni mwaka mmoja wa kuchumbiwa.

Kama mjuavyo, desturi zetu za Kiafrika baada ya mahari mnaulizwa tarehe ya Ndoa ndivyo ilivyokuwa na kwetu pia ila mwenzangu aliomba ajipange sababu hakuwa vizuri kwa kipindi hicho hivyo wazazi walimkubalia.

Sasa napata maswali mengi kutoka kwa wazazi na ndugu wakiniuliza ndoa lini mpaka nakosa majibu sababu nikimuuliza mwenzangu ananiambia nina haraka gani nisubiri.

Kilichonifanya nije kwenu ni kuomba ushauri je niko sahihi kuendelea kutumikia majukumu yangu ya ndoa kwa mgongo wa kuchumbiwa au nimechutama choo cha kiume?
Pole
 
Kama mnaishi vizuri we enjoy tu achana na maswali yao.

Wanaume wakikumbushiwa sana mambo ya Ndoa wanakasirika.
 
Back
Top Bottom