Ameniomba hela ya chai; nimemrushia buku na 200 ya kutolea amekasirika!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Salaam!

Katika kusaka faraja murua, juzi kati nilikutana na mdada mmoja hivi murua kabisa. Zoezi la kubadilishana namba likaenda vizuri.

Leo asubuhi na mapema kaniomba hela ya chai; nami, kwa kuzingatia bei halisi ya maandazi huku kijijini ambayo ni tshs 100, nikamrushia buku na mia mbili ya kutolea. Nilifanya hivyo nikiamini kuwa maandazi saba na kikombe cha chai atapata.

Ajabu ni kuwa alipopokea aliniuliza kama mara tatu hivi kuwa nimemtumia au la. Nilipomwambia kuwa ndiyo nimemtumia 1,200 ili apate buku ya chai, hajajibu chochote na hapokei simu mpaka muda huu. Nikafikiri labda amepatwa na ugonjwa kumbe taarifa za kiintelejinsia zinasema ni mzima wa afya tu.

Kuna nini hapa?!!!
 
Mkuu umefanya niwe na usiku murua kabisa😂😂
 
wewe ni katiliwa kijinsia
 
Safi sana, kumbe Wanaume wenye misimamo bado tupo?

"Win win situation" ya China ndiyo inaendana na filosofi ya "HAKI SAWA".
 
Wewe ni Mkuu wa Vikosi vya watu Bahili zaidi Duniani 😂😁
 
 
Upewe Maua yako mkuu
 
Kwenye kikao cha wanaume utakuwa msemaji mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…