Hata ndoa inaweza kuvunjwa ikiwa kuna tatizo au kosa kubwa limefanyika.
Kuvunja uchumba sio tatizo wala kuvunja ndoa sio tatizo.
Watu wenye Akili zao humu wanashangaa sababu za kuvunja huo uchumba mliodumu nao Kwa muda mrefu. Yaani sababu ya kuvunja huo uchumba uliyoitoa haina kichwa wala miguu.
Kosa umefanya wewe,
Bado mtoto wawatu kajishisha kakuomba Radhi licha ya kumkosea, kumdhalilisha na kumtia aibu, lakini wewe bado Kwa Akili yako ndogo huoni kwamba wewe ndio unashida.
Kama ulikuwa haumpendi na haujafanya maamuzi ya kumpenda, huo muda uliompotezea huoni umefanya dhulma?
Alafu Wanawake wakiwazingua mnaanza kupiga mayowe kuwa Wanawake ni wabinafsi,
Kuna ubinafsi zaidi ya huo ulioufanya?
Hapa tunajadili, najua inaweza kuwa ni Stori tuu uliyoileta, sidhani MTU mwenye Akili anaweza kufanya hivyo. Labda punguani