Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Patriot3
HIvi unaona ni sahihi kuahidi na kutoa tarehe ya kulipa mahari...halafu upate dharura na usipileke taarifa kuwa hamtakuja kwasababu mmepata dharura?
Hii ni sawa?
Alipaswa aombe ahirisho.
Lakini jamaa badala ya kuomba kusogeza mbele alikuja kuanzusha uzi jf kama vile ufahari flani...tusifagilie ujinga huu wakuu wangu...tuwe wanyenyekevu dunia ni katili sana ikianza kukulipa kisasi...wanaita karma
Vijana wanadanganyana sana sana
 
Naheshimu sana michango yenu na napenda kuishia hapa. Kwangu mimi, kuwajali watu wengine walio katika shida ambazo ninazimudu ni ibada kwangu. Ndoa ikishindikana leo, itafanyika kesho. Kama si kwa huyu basi ni kwa mtu mwingine. Sina shaka! huyu mahusiano yetu hayatakuwepo tena. Nimeyavunja rasmi this morning. Nitajipa nafasi, si kwa lengo la kukua maana nimekua na akili imekomaa haswa. Imani yangu ni kwamba nitakutana na mtu mwenye mtazamo ule ninaoutaka, ikitokea hajapatikana wala hakuna shida. Ninaishi na nitaishi kwa kuwajalii wengine.
Idiot!
Life has a funny way of making you deal with what you make other go through.
Siku utampata binti umempenda mnaenda kufunga ndoa umealika ndugu na jamaa na binti hatotokea kanisani. You will someday feel what she felt .
 
😂😂😂

Kusaidia Watu bila Akili nako ni upunguani.

Ndio maana Manzoni nikakuambia wewe bado haujakua Kiakili, ndio maana hata hujui maana ya Familia.
Familia ndio kitu cha Kwanza Kwa mwanaume na Mwanamke mwenye utimamu wa Akili.
Huwezi sema unasaidia wengine ATI Kwa kisingizio cha ibada huku ukivunja ahadi na Binti uliyekaa naye kwenye mahusiano muda mrefu.

Unajiangalia wewe pekeako Kwa sababu wewe ni mbinafsi.
Hauangalii ni muda gani umempotezea Binti WA watu tena Bora yeye angekuwa amekukosea Ila wewe ndio umemkosea,
Yeye kakasirika ndio maana akakumaind lakini Kwa vile wewe unakiburi hukutaka kujishusha na kuomba Radhi.

Ninyi ndio wale wanaume wa humu JF ambao mnapenda muonekano Kwa nje ni Wema Kwa kuwajali watu wa nje(marafiki ikiwemo wa JF) Kwa kujifanya mnamichango ya kistaarabu kumbe ndani ni Mbwa mwitu.
Si unaona, huku unajifanya mstaarabu Sana unapotoa comments zako lakini unayoyafanya Huko kwenye Maisha halisi mfano Kwa hiyo Mchumba wako ni ushenzi uliopitiliza.

Hata kama utaamua ku-move on muombe Msamaha hiyo Mrembo wa Watu, ili uendelee na Maisha yako Kwa Amani.
Kumpotezea mtoto wa Watu muda na kupeana ahadi na viapo kisha kuvivunja Kwa sababu za kijinga ni usaliti wa Hali ya juu.
Na Dawa ya wasaliti inafahamika,

Ni hayo tuu.
Take this, "uchumba si ndoa". Ahadi ni makubaliano yanaweza yasiwe na certification pia kwahiyo yanaweza kuvunjika.
 
Idiot!
Life has a funny way of making you deal with what you make other go through.
Siku utampata binti umempenda mnaenda kufunga ndoa umealika ndugu na jamaa na binti hatotokea kanisani. You will someday feel what she felt .
Idiot!!
Sikiliza rafiki, mahusiano ni makubaliano. Makubaliano yasipkwenda sawa, hayana budi kuvunjika. Tuache mihemko isiyo na tija. Si ugomvi wala hakuna aliemlazimisha mwingine kuingia kwenye shida fulani mpaka tuzungumzie karma.
 
Naheshimu sana michango yenu na napenda kuishia hapa. Kwangu mimi, kuwajali watu wengine walio katika shida ambazo ninazimudu ni ibada kwangu. Ndoa ikishindikana leo, itafanyika kesho. Kama si kwa huyu basi ni kwa mtu mwingine. Sina shaka! huyu mahusiano yetu hayatakuwepo tena. Nimeyavunja rasmi this morning. Nitajipa nafasi, si kwa lengo la kukua maana nimekua na akili imekomaa haswa. Imani yangu ni kwamba nitakutana na mtu mwenye mtazamo ule ninaoutaka, ikitokea hajapatikana wala hakuna shida. Ninaishi na nitaishi kwa kuwajalii wengine.
We jamaaa una mambo ya kimaku maku sana asee![emoji848][emoji848]

Yaan liuzi umelileta mwenyewe, watu wamekupa ushauri mzuri sana, ila we kutokana una nia ovu na kiukweli hukumpenda huyo dada, unajifanya eti umeuvunja uhusiano! Which is absolutely irrelevant !!

Utakuja kuandamwa na minuksi mpaka uombe poo! Shauri yako
 
Idiot!!
Sikiliza rafiki, mahusiano ni makubaliano. Makubaliano yasipkwenda sawa, hayana budi kuvunjika. Tuache mihemko isiyo na tija. Si ugomvi wala hakuna aliemlazimisha mwingine kuingia kwenye shida fulani mpaka tuzungumzie karma.
Kibaka kweli wewe.
Ndiyo yasipokwenda sawa yanavunjika lakini hakikisha hayafiki hatua ya kusababishia wengine maumivu.

Hauwezi kuyaelewa vizuri maumivu mtu anayoyapitia bila na wewe kupitishwa kwenye situation hiyo hiyo.
Na hiyo ndiyo kazi ya karma.
 
Yaani unapanga kupeleka mahari halafu unahairisha na unapoambiwa uombe msamaha unasema unakorogwa kichwa? Dada wa watu kapewa ishara muhimu sana kuwa wewe hufai lakini maskini ameshindwa kuitambua. Wewe huna tofauti na Magufuli kitabia na ndoa yako itakuwa kama ilivyokuwa yake.
Jiwe tena hahaha
 
Mapenzi mkuu. Husababisha upofu. Majuto ni mjukuu. Ila upo sahihi kabisa. Kuna mwingine namjua aliamua kujilipia mahari mwenyewe. Yaani bwana alikuwa anasuasua (ila walikuwa wanaishi na demu) basi demu akatoa fedha akandaa ndugu wa kule kwa bwana wakapeleka mahari. Mwanaume alikuwa ni mtu wa kujirusha hivi, handsome fulani hivi, demu akakolea mno. ndoa ilifungwa lakini ugomvi ukawa hauishi. Na kila walipokuwa wanagombana jamaa anawaambia marafiki zake, ''kwanza alijioa mwenyewe huyu''.
Teh teh teh[emoji16][emoji16]

Wanawake kazi tunayo[emoji848][emoji848]
 
Take this, "uchumba si ndoa". Ahadi ni makubaliano yanaweza yasiwe na certification pia kwahiyo yanaweza kuvunjika.

Hata ndoa inaweza kuvunjwa ikiwa kuna tatizo au kosa kubwa limefanyika.

Kuvunja uchumba sio tatizo wala kuvunja ndoa sio tatizo.

Watu wenye Akili zao humu wanashangaa sababu za kuvunja huo uchumba mliodumu nao Kwa muda mrefu. Yaani sababu ya kuvunja huo uchumba uliyoitoa haina kichwa wala miguu.

Kosa umefanya wewe,
Bado mtoto wawatu kajishisha kakuomba Radhi licha ya kumkosea, kumdhalilisha na kumtia aibu, lakini wewe bado Kwa Akili yako ndogo huoni kwamba wewe ndio unashida.

Kama ulikuwa haumpendi na haujafanya maamuzi ya kumpenda, huo muda uliompotezea huoni umefanya dhulma?

Alafu Wanawake wakiwazingua mnaanza kupiga mayowe kuwa Wanawake ni wabinafsi,
Kuna ubinafsi zaidi ya huo ulioufanya?

Hapa tunajadili, najua inaweza kuwa ni Stori tuu uliyoileta, sidhani MTU mwenye Akili anaweza kufanya hivyo. Labda punguani
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.

Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.

Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.

Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Kaza mzeebaba usipelekeshwe weka misimamo mapema😎
 
Ila wewe mbona ishu yako ndogo ..mimi kuna mwana yeye sio tu aliahirisha ila hata manzi ake hakumwambia..Kikeni huko wamejiandaaa kishenzi mavyakula na vilaji kama unavyojua wachaga!.. e bwana eeh!!. Mshkaji hakutokea kabisaaaaaa wala manzi ake hakumwambia kitu yan ilikua bonge la soo na aibu kwa dem..ndugu jamaa walishajaa kupokea mahali na kumwona jamaa ila ikawa tee!!.

Wanawake sas wasivyo na akil wakat mwingine, manzi aliporud dar wakaendelea kuishi na mshkaji..sijui waliyamaliza vp? 😂😂😂
Hii ndio sababu kuu inayothibitisha maneno kuwa “usimwamini mwanamke kamwe kamwe”
 
Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.
Hili sio jukumu lako. Jukumu la Mshenga, tena siku hiyo hiyo ya kupeleka mahali husika, katika mazungumzo ya hapa na pale ya kujiweka sawa kabla ya kukabidhi mahali ndio anaweza chommekea hilo swala.

Wewe cha kufanya mueleze huyo mpenzi wako awajulishe wazazi wake kuwa kuna ugeni utakuja Siku fulani mwezi fulani kuleta Mahali.
Kuna binadam wengine wana historia ndefu sana katika maisha yetu. Niliamua kumusaidia na sikuona sababu ya huyu mpenzi wangu kupaniki na kuomba tuachane. Leo anaporudi na masharti ya kwamba niombe msamaha nyumbani kwao, naona kama ananikoroga kichwa tu.
 
Ila huyo mwanamke hana akili pamoja na kumuaibisha bado kajileta mfyuu zake
Numbisa nyie wanawake ni viumbe vya ajabu sana…yani mwanamke anaweza kukugeuka muda wowote ule! Yani mtu amefanyiwa kitendo kama hicho bado amerudi kwa mwanaume na kuwaacha solemba ndugu zake
 
Back
Top Bottom